Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Kukubali kwa wapinzani kuingia tena kwenye uchaguzi huu watakuwa wenyewe hawajitambui. Ila natambua wapinzani ( au kwa lugha nzuri "vyama mbadala"), ni watu wenye uelewa mpevu pengine hata kuliko hawa watu wa serikali na chama chao. Hapo Jafo anawakilisha tu maamuzi geugeu toka kwa bosi wake. Yote ya kijinga yalofanyika ya kuwaengua wagombea wa upinzani haikuwa jambo la bahati mbaya bali liliratibiwa toka juu.( wewe unayetaka udhibitisho wake endelea kuganda hapo ukisubiri).
Kwa mfano hai (ingawa sitataja Nina wahusika ila ni ndani ya Babati mjini) hao wanaoitwa wasimamizi wadogo ambao ni watendaji wa mitaa(tambua hiyo ni serikali), kuna mmoja alifuatwa usiku wa SAA sita baada ya muda wa pingamizi kupita akalazimishwa kusaini barua ya pingamizi, tena hata waloweka mapingamizi wenyewe hawakuwa na habari kwani ni majina yao tu yaliwekwa bila wao kuhusishwa.
Kwa mantiki hiyo Jafo anapokuja na kete ya kufuta utenguzi wa kijinga ulofanywa, ni janja tu ili ulimwengu uone kwamba kuna chaguzi za vyama vingi nchini. Ila tukumbuke ile kauli au niseme amri walowahi kupewa wakurugenzi...mshahara nikulipe mimi,....halafu usimame utangaze mpinzani kashinda, utakuwa na akili kweli wewe!!! Hapohapo tusisahau watendaji wote wa kata waliitwa madhabahuni na kuhimizwa na kuagizwa waloagizwa, ambao hao wote ndo wenye dhamana ya kutangaza matokeo ya chaguzi zetu.
Kwa maana hiyo endapo mamlaka ikifanikiwa kushawishi wapinzani kurejea, hakika hiyo kete ya mwisho ya kutangaza matokeo itakula kwao tu.
 
"Mkurugenzi Nikupe Gari, nikulipe mshahara halafu Unamtangaza mpinzani kashinda................"kauli hii itafanya kazi baada ya mbinu ya kupita bila kupingwa kugonga mwamba.
Hizo nikauli zinazotakiwa zifutwe kwanza ili upinzani warudi
 
Unashangaza sana...kumbe ndiyo maana CCM tunafanya mikutano popote pale huku wapinzani wakikatazwa baada ya wananchi kumkubali JEMBE au siyo?
 
Wewe unaishi wapi ambako hakuna mtaa wala kitongoji wala kijiji ndio maana hujui hata uchafu uliofanyika huku duniani ambao umeratibiwa na chama na serikali! Au unamaliza hewa tu!!!
 
Maelekezo ya kuruhusu wagombea wa upinzani walioenguliwa kushiriki uchaguzi ni sawa na mtego wa panya, wakikubali tu wamenasa! Wakishinda CCM itakwenda mahakamani kudai ukiukwaji wa kujaza fomu na ushahidi wa wazi wanao! Kwishney, mahakama itatoa uamuzi kulingana na sheria na si maelekezo ya waziri Jafo. Kwa sasa upinzani unamwachia mpira waziri Jafo azunguke nao uwanjani na apige danadana kwa raha zake pia asione aibu kufunga goli kwa chenga za Zizo hata kama goli liko wazi, na hapo atapata ushindi wa kishindo utakaoweka historia nchini.
 
Chadema haita shiriki na wana ccm hatushiriki pia.. tuache shughli zetu kupiga kura ambazo mmesha piga.? Pambafu sana nyie
Kama wewe ni mwana CCM, basi umenifurahisha. Kumbe sio vibaya kuwa CCM
 
Sasa tumuamini nani,anasema ukweli,
Wewe umewaruhusu lakini katibu wako mwenezi,yule aliyedumaa,alisema wameondolewa kwa ajiri ya ujinga wao tu!
Yaani tangu tupate Uhuru,wagombea wa upinzani wamekuwa wajinga wote!Ila wa CCM wote wanaakili!
Katika vituo vyote,ni wa upinzani tu ndio wamekosea kujaza form! Wa ccm wote wamepatia!
Ghafla waziri ameruhusu wale "wajinga" wote waendelee!
Madudu haya!kweli chama LA wana mmekaribia kufa
 
ikuo [emoji654] Mwenyekiti wa tume angeteuliwa na wananchi sawa, sasa unataka kuniambia kuwa mwenyekiti wa tume hakujua kabla kauli ya jafo?
 
Huu uwongo wa Zitto tumeuzoea na tushampuuza kazi yake ni kuzusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…