Waziri Jafo abadili gia angani, afuta maamuzi yote ya wasimamizi wa uchaguzi kuwaengua wagombea. Wagombea wote ruksa kushiriki uchaguzi

Atasema watu waangalie mandishi na sio maneno maana atasema alinukuliwa vibaya. Hakuna kushiriki huo upuuzi ili waendelee vizuri na maamuzi yao.
 
Naona mwaka tu waliandika 2910 kwa hiyo hata taarifa yake si ya kweli.
 
Jafu amsikilize Baba lao, akiwasikiliza Wananchi atapoteza ugali.
 
Jiwe laLumumba litakua limepiga simu
 
Leo tarehe 11/11/2019 waziri wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (Tamisemi) Kaja na mapya tena, kwa maelezo yake na nyaraka alizotoa leo kupitia ofisi yake kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, kaja na igizo lingine kuwa yeye jana alinukuliwa vibaya, waandishi wa habari hawakumuelewa kuwa wagombea wote waliopita na ambao hawakuwa na sifa wote warudishwe na washiriki uchaguzi huu utakaofanyika 24/11/2019 . Leo anasema watakaoshiriki uchaguzi huo ni waliomba nafasi hizo na wakapitishwa. Pili waliokata rufaa na rufaa zao zikakubaliwa, hivi huku kubadilika badilika kwa kauli za waziri wa Tamisemi nini kinamsumbua? Mbona anaaibika sana maskini.Wapinzani kaeni chonjo hiki kigeugeu cha Jafo inatafutwa mbinu ya kuwaingiza mkenge kura ziibwe plus maagizo kutoka juu.
 
Hatukumuelewa tu
Alisema waliochukua na kurudisha fomu kisha wakakatwa na kukata rufaa watarejeshwa kwenye mchuano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…