Waziri Jerry Silaa ana kitu, atafika mbali, abarikiwe

Pole sana Kwa kupoteza nyumba, Fungua case court sasa udai HAKI Yako,
Achana na hilo tapeli/fisadi.
Naona unasoma maandiko yake, lakini bila shaka umeamua tu kumvumilia. Binafsi sina uvumilivu wa namna hiyo.
 
Mtu unaambia watueti tumuombee!! Huu upuuzi huwa mnautoa wapi wa kuwapangia watu wamuombee nani??
Bora mngesema tuliombee taifa,yaani mtu mmoja akijipurukusha kimakiki watu mnakaa wazima wazima kindezi!!
MATATIZO ya ardhi yanahitaji mifumona taasisi Bora sio mtu mmoja na makamera mia...ujinga mtupu
 
Mifumo haijengwi na waziri inajengwa na rais, waziri ni mtekelezaji tu. Kama waliopita hawakutilia maanani, unataka huyu alie teuliwa juzi afanye nini? Overnight kuwe na mifumo? Be serious

Acha aende field maana humo kuna mengi. Wala haiti watu , ila kutokana na shida za ardhi watu humfuata wenyewe. So far program yake ni the best. Maybe hayuko perfect 100% lakin anafanya kitu. Hao the rest kwenye wizara zao wanao fuata mifumo wamefika wapi?
 
 
Tajiri yule alipoambiwa atoe vitu vyake na kumkabidhi mhusika Mali yake,

Alisema kuwa Eti Hana pa kwenda na kumwambia waziri anaonaje wakiongozana Ili waongee kidogo pembeni,

Jambo Hilo liliamsha hasira ya Waziri na kuamuru vyombo viondoke naye.
Kwanza nina njaaa🤣🤣🤣🤣
Kuna watu matapeli sana.
 
Apite na majimbon kwake wananchi wanatesek sana kitunda kinyantila brabara hazipitiki akikaa sehem moja tu huk wizarani hawez kutatua chngamot za wananch wake
 
kumbuka wapika majungu na fitina ni watu wana nguvu kweli...wana uwezo wa kubadilisha jambo zuri na kuwa baya.

watendaji wazuri wote Serikalini hufitiniwa na kuzushiwa mambo ya uongo ili tu watolewe.
kinacho hitajika hapa ni Kiongozi aliye mteua /wateua kubaini ukweli na uongo na pia kuwa na msimamo wa kuwaamini viongozi wachapa kazi sio kufuata maneno ya fitina na majungu.

Majungu na Fitina ndio kikwazo kikubwa sana kwa watendaji wetu. hili ni tatizo kubwa sana hapa Bongo.
kuna mawaziri hawataki misuguano na watu kwajili ya kuogopa kutolewa na wengine ni majasiri kama waziri wa ardhi ilimradi anasimamia haki yeye liwalo na liwe.
big up Waziri wa Ardhi.
 
Tena nasikia kumbe Mmasi ana kesi ya Jinai ya kugushi nyaraka za umiliki wa hiyo nyumba huko Mahakama ya Wilaya toka mwaka jana kesi iko Mahakamani!!
 
N
Tanzania tumewapa wanasiasa mamlaka kubwa mno na ndio maana wanafanya watakavyo kwani wanajua wao wapo juu ya sheria na kwa bahati mbaya sana sisi wananchi tunawaunga mkono! Slaa hawezi kuwa mbadala wa mahakama hata rais hawezi kuwa mbadala wa mahakama kama ulivyoandika! Hamjui haki zenu na mtaendelea kudhulumiwa sana watanzania.
 
M
aha ndio mwamuzi wa mwisho wa mgogoro wowote hata makampuni huenda mahakamani kuishtaki serikali endapo inavunja mikataba pasipo utaratibu. Mgogoro wa ardhi baina ya pande mbili hutatuliwa mahakamani na sio wizarani!
 
M

aha ndio mwamuzi wa mwisho wa mgogoro wowote hata makampuni huenda mahakamani kuishtaki serikali endapo inavunja mikataba pasipo utaratibu. Mgogoro wa ardhi baina ya pande mbili hutatuliwa mahakamani na sio wizarani!
Kila mgogoro wa Aridhi una historia yake,sasa kabla ya kumlaumu Waziri ebu fanya kwanza utafiti wako,maana wengine hadi maamuzi ya Mahakama kuu kuhusu huo mgogoro tumeyasoma humu,na ndiyo maana tunaona Waziri yuko sahihi kabisa kulibalasa lile Tapeli kwenye Nyumba ya Marehemu!!
 
Waziri aliambatana na commissioner wa ardhi husika, Mmassy akaleta documents na mke wa marehemu akaleta documents.

Document ya Mmassy inaonyesha marehemu alisaini kumuuzia Mmassy nyumba tarehe ambayo muuzaji alikuwa kaburini, amezikwa tayari.

Na Hadi waziri anakuja pale, Mahakamani ilishaamua kuwa mmiliki halali ni family ya marehemu, Mmassy Akaenda kuweka pingamizi.

Hadi hapo, waziri ana mamlaka kumtoa Mmassy kwenye nyumba hiyo kufuatana na mmiliki halali tayari anafahamika, na Mmassy ana kesi ya kughushi hati na mkataba wa mauziano.

fazili
 
Kwanza nina njaaa🤣🤣🤣🤣
Kuna watu matapeli sana.
Hilo tapeli lilitaka likamnunulie chakula waziri hoteli kubwa Kisha limwandikie cheque kumzima.

Nijuavyo, commissioner wa ardhi ana HAKI ya kupitia document na Kutoa uamuzi wa nani mmiliki halali Kisha atakayeona hajatendewa HAKI ndiye aende mahakamani.

Matajiri hutumia mahakama kudhulumu HAKI ya maskini, anapora kiwanja chako, anatengeza hati fake kupitia wezi wenzie watumishi wa ardhi, anajenga nyumba, Kisha anakwambia uende mahakamani.

Sasa, waziri na team yake, wakigundua Hilo site, Wana HAKI ya kubomoa nyumba ya tajiri na kumkabidhi mwenye HAKI, Kisha tajiri ndiye akashtaki wizara Kwa kumbomolea.

Migogoro mingi, watumishi wa ardhi wanahusika, nashauri waziri angekuwa anawafuta KAZI hao watumishi wanaohusika kutengeza hati fake Ili waadhibiwe sambamba na wavamizi.
 
Apite na majimbon kwake wananchi wanatesek sana kitunda kinyantila brabara hazipitiki akikaa sehem moja tu huk wizarani hawez kutatua chngamot za wananch wake
Tupambanie KATIBA mpya Ili waziri asitokane na wabunge.

Hapo mkabeni shati mbunge wa viti maalum akaimu vizuri nafasi ya mbunge awapo katika utumishi wa nje ya Bunge Kwa nafasi ya Uwaziri.
 
Kongole kwake
 
Kongole kwake
Yaani commissioner wa ardhi waende site, wakute mtu amejenga kimabavu kwenye eneo la mwingine,

Wajiridhishe na kuhakikisha document kuwa aliyejenga nyumba amevamia, commissioner wa ardhi anao uwezo wa kuamuru nyumba ibomolewe, mwenye kiwanja halali apewe HAKI yake,

Huyo mvamizi ndio aamue kwenda mahakamani au la.

Waporaji ardhi wamekuwa wakitumia mahakama kama kichaka Cha kuchelewesha HAKI.

Waziri asonge mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…