Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Waziri Nape: Natoa siku 7 waajiri kuwalipa Waandishi wa Habari waliofariki kwenye ajali. Tambueni tu leseni zenu ziko kwangu

Tumerudi utawala uliopita? Makampuni binafsi yanataratibu za kuwalipa wanaopata ajali, hao wahusika hawakupanda gari za makampuni yao na hili liwe fundisho kwa waandishi wa habari kwa kupenda chee!

Waandishi hawa wamepata ajali kwenye gari ya serikali, sidhani kama ina bima. Kutokana na gari kuwa si ya mwajiri sijui hapo mwajiri anahusikaje! Mheshimiwa waziri chukua jukumu la kuubeba msiba na malipo majeruhi na waliofariki na si kuonesha ubabe.
 
Umeanza na speed ya pikipiki
Walipwe nini?
Life Insurance au malimbikizo ya mishahara
Ukali wa nini
Viburi hivi sijui
Waliokufa kwenye Hiace mtetezi wao yu wapi? Hawa ndio bora walikuwa harawa zenu au
 
.... serikali inataka kujitoa kimtindo wakati walikuwa wanaenda kuandika habari za serikali na walikuwa wamebebwa na serikali (STL) na sio waajiri! Kwa mfano, suala la bima (ya ajali) hapo inakuwaje? Chombo kilichosababisha ajali ni cha waajiri?

Nimejiuliza sana ilikuaje waandishi wa habari wa vyombo binafsi kuchukuliwa na gari ya serikali? Tufanye ilikua kuna makubaluano japo sijui kitaaluma na maadili kama ni afya kufanya hivyo. Inaondoa kutokuegemea upande au maoni huru wakati wa ku report.

Sasa tuje kwenye BIMA, kama gari ya serikali au hiyo ya abiria zina boma, si hua inajumuisha na walioko kwenye chombo?

Hapa ndio nimejua kwanini ofisini hairuhusiwi kuchukua mtu ambae sio mfanyakazi hadi kwa kibali maalum. Wanasema ikitokea ajali wewe staff uko covered lakini huyo.mwingine ni liability.
 
Vipi kuhusu wale raia wengine waliofariki kwenye ajali hiyo mbona habari zao sijaziona? ingependeza kama nao wangeagwa hapo pia.
Waandishi ndiyo binadamu peke yao

Hawa jamaa kwa sasa kila wanachogusa, kinaenda mrama. Sema ni kwa vile tu wana uzoefu wa manuva na roho ngumu.
Inamaana sasa hivi hakuna kabisa wazee wanaweza sema msifanye namna hiyo, fanyeni hivi, hiyo italeta madhara haya na haya. Hawapo washauri?
 
Mmh. Siku 7? Je, familia zao watakuwa wamemteua Administrator au taratibu hazitafuatwa then familia watalalamika. Terminal benefits zina utaratibu wake....
 
Nionavyo mimi katika mazingira ajali hii ilivyotokea wenye jukumu 'la pekee na la kwanza' la kuwalipa waandishi wa habari ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (maana waandishi wa habari wamefia mikononi mwa ofisi hii) iliyokuwa imewaalika kwenda kufungua miradi ya maendeleo wilayani Ukerewe.

Jukumu la kawaida ni kwa vyombo vya habari ambako hao waandishi walikuwa wakifanya kazi maana wamefariki wakiwa kazini. Ajali isiwe fimbo kwa vyombo vya habari walikokuwa wakifanya kazi hao waandishi wa habari.

Kuna watu wengine pia waliofariki katika ajali hii na hao nani anajukumu la kuwalipa hao ndani ya wiki moja? Kila anachofanya waziri lazima kiwe kimekaa vizuri kisheria, otherwise waziri anaweza kujikuta anatoa maagizo ambayo ni 'ultra vires' au 'arbitrary'.
 
Waziri wa Habari na Mawasiliano ya teknolojia ya Habari Nape Nnauye ni miongoni mwa waliofika uwanja wa Nyamagana kuungana na RC Mwanza, Injinia Robert Gabriel na Waombolezaji wengine kuaga miili ya Waandishi 6 waliofariki kwenye ajali jana...
Huyu mtu hana ufahamu wa nafasi anazopewa. Pamoja na agizo hilo je, serikali imewahi kulipa watumishi wake ktk siku saba? Tabia hii ndo iliyomfanya kuhangaika na uchunguzi wa Makonda badala ya kuangalia uhusiano wa ofisi yake na ngazi zingine.

NI waziri anayehisi kuwa na dhamana ya kulinda wana-habari. Kwa mtindo huo kila waziri atalinda watu wake. Polisi hawataguswa, wakulima hawataguswa, nk.
 
Serikali inalipa mirathi na kiinua mgongo kwa watumishi wake baada ya miaka 2 na kuendelea ,lakini private sector mnataka ilipe ndani ya siku 7.
Shida wanatawala,hawaongozi, hivyo amri sizizo za kufikiri imekuwa sehemu ya utawala wao.AMRI.
 
Najaribu kufikiria kosa la waajiri, wakati waandishi walifia kwenye gari la STL
Hao ndio wanasihasa...!! Wanasema kile wasichokiamini.

Mtu aliyetakiwa kuwa held responsible ni RC Mwanza.....as Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa na kiongozi wa msafara alitakiwa KUHAKIKISHA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VINAWAJIBIKA KWA USALAMA WA MAISHA YA WAANDISHI HAO.

Kuna misafara nyingine haina tija yoyote kabisa. Hivi unabeba Waandishi wa habari wote hao unazunguka nao @ kufungua madarasa ya mkoa wote ili iwe nni? Huyu RC Mwanza angelikasimu hiyo kazi kwa ma- DC kusingetokea hii ajali ya kizembe.

RC MWANZA anapaswa ajiuzulu kwa uzembe huu.
 
Vipi kuhusu wale raia wengine waliofariki kwenye ajali hiyo mbona habari zao sijaziona? ingependeza kama nao wangeagwa hapo pia.
Hii nchi ina ubaguzi wa kijinga sana....!! Wana sihasa ndo shida. WATU 14 WAMEPOTEZA MAISHA LAKINI TUNAONA WANAOZUNGUMZIWA SANA NI WAANDISHI WA HABARI 6!!!!
Hapa ndipo ile hadithi ya kitabu cha ANIMAL FARM(SHAMBA LA WANYAMA) inaposema SOME ANIMALS ARE MORE EQUAL THAN OTHERS!!!
 
Back
Top Bottom