Waziri Nape Nnauye asema bei ya internet imeshuka wakati wa Rais Samia ukilinganisha na Machi 2021

The only person who can trust this guy is an individual with a mental disorder..................
 
Hizi porojo, zamani 35,000 nilikuwa napata GB 30 Tigo, sasa hivi napata 19. Elfu 50 ilikuwa GB 50 sasa hivi kwa bei ileile almost unapata nusu yake GB 27.

Hizi ni hesabu rahisi kuzielewa kuliko majedwali yake aliyoyaweka kisiasa.
Huyu jamaa bure kabisa....is he okay?...
 
Muongo.

Angalia idadi ya vifurushi ndio ujue kama unafuu upo ama la??

Wahuni wanatupeleka peleka.
 
Mambo kama haya ndiyo yanayofanya baadhi ya watu wahisi kuwa,hata kile kinachoitwa ruzuku ya mafuta,hakitolewi bali watakuja kutuletea vijedwari kama hivi wamefunga funga maandishi yao na kusema hiyo ndiyo Ruzuku ya mafuta.
 
Mlamba asali kumtoa kwenye huyu inahitaji minimum force.
 
Duu we jomba
 
Ni kweli, March 2021 alikua bado hajaanza kulamba aslani. Ukilamba asali huwezi kujua shubiri wanayopitia wananchi
 
Napata hasira sijui kwanini tu, nikisikia kiongozi yeyote serikalini akitoa hotuba hasa inayowalenga wanaNchi wa hali ya chini ( wanyonge )
 
Compare na mwaka jana? Ndio vifurushi vimeshuka sasa hivi, kuna kipindi 1000 ilikuwa ni mb 300 tu ila sasa hivi 1000 ni mb 550 kwa Tigo, pia Airtel niliona 500 unapata mb 300. Hapa naongelea vifurushi halisi sio ofa.

Ila compare na awamu ya 4 bado vipo juu, awamu ya 4 ilikuwa 1000 unapata 1GB, 500 500mb etc.

Chengine wamejitahidi kwenye internet za majumbani, sasa hivi maeneo mengi kuna coverage za Fiber, Adsl na satelite internet, na bado usambazaji unaendelea kwa kasi.
 
Uliyeandika hapa bila shaka ni Mzanzibari huwezi kukosoa chochote kutokana na kuota dodo
 
Huenda Kuna vifurushi vya walamba asali,

Hivi niliyekuwa napata 9.5GB kwa Tzs 10,000 lakini Leo napata 4.5GB kwa Tzs 10,000 kumbe ndo kushuka hivi, hakika kuvimbewa ni dhambi.
 
Yuko sahihi maana hata Bei za internet Tanzania ziko Chini kuliko Nchi jirani ila husikii malalamishi ya kijinga [emoji116]
Umelinganisha na uchumi wao na Un Employment rate yao au ni kupost tu? Eti huskii malalamishi? Wakati Kenya mwezi wa 8 Rais Uhuru ameagiza garama za kupiga simu zishushwe Kenya, baada ya tafiti kuonesha calling rate ipo juu sna, kupiga simu kume pungua snaaa. Akamteua, Ezra Chiloba kushughulikia.
 
I remember 2008/2009 tunanua mb20 kwa 500..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…