Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Waziri Ummy: CoronaVirus bado ipo, tuendelee kuchukua tahadhari

Mh Ummy binafsi nakuheshimu sana na sitaki kupoteza imani yangu kwako. Hebu kama wewe hujui korona iko wapi basi ruhusu watafiti watuambie korono imehamia wapi kutoka vituo vilivyotengwa kutoalea huduma ya wagonjwa hao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😂😂😂😂😂😂 vituko vya hii Nchi yetu wakati mwingine unabaki kutabasamu tu kwa kejeli.

Ugonjwa Umepungua Sana yaani wamebaki wagonjwa wanne tu TZ Nzima ila Mipakani huko Kila siku "MADEREVA WA NCHI NYINGINE" wanakutwa na Korona.
 
Kwa hiyo Waziri kwa akili yake anahesabu waliolala kwenye kitanda cha Hospitali. Ni kweli kwamba tuna mawaziri wa aina hii? Kwamba hafahamu wa-TZ wanajifungia nyumbani kuliko kunyanyapaliwa hospitali?
 
Mungu Ameturehemu Watanzania. Mungu ni Mwema. Ee Muumba wa Mbingu na Dunia.... Tunasema Asante kwa Rehema hii KUU katika ardhi ya Tanzania. Asante kwa kutulinda na kutuponya Gonjwa hili Novel COVID - 19

Unataka tukubali kuwa Mungu anatulinda sisi Watanzania tu? Mamilioni wanaokufa na Covid 19 ulimwenguni wao vipi hawapendwi na Mungu aliyewaumba?
 
Acheni Uongo Jamani wakati hapa Mwanza kuna wagonjwa kibao / Uongo uongo mtupu.
 
Unataka tukubali kuwa Mungu anatulinda sisi Watanzania tu? Mamilioni wanaokufa na Covid 19 ulimwenguni wao vipi hawapendwi na Mungu aliyewaumba?
case ni kuwa, hakuna cha bure, ukitaka Mungu akuangaikie lazima umuhangaikie
 
Hivi inawezekana ikawa tumetumia mbinu gani kulishinda hili janga hivi, Kwa mbinu yoyote tuliyotumia kwanini tusi share na ulimwengu ili kunusuru dunia na hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaona walioji lockdown walivyopukutika? Sisi tuliachwa tukapata fresh air.
IMG-20200601-WA0000.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Juzi na jana jamaa zangu wa karibu wawili wamefariki kwa corona na wote eneo moja la Bulyanhulu. Endeleeni kuficha sie taarifa tunazo kwa kile kinachoendelea. Kwa sasa kutoa taarifa ya kifo cha corona huko ni uhaini. Si vizuri kuweka picha zao na majina yao hapa ila mlio na ndugu Kakola Bulyanhulu ulizeni
 
Ugonjwa Umepungua Sana yaani wamebaki wagonjwa wanne tu TZ Nzima ila Mipakani huko Kila siku "MADEREVA WA NCHI NYINGINE" wanakutwa na Korona.
Hahahahahah tucheke tu hakuna jinsi
 
Leo tu watanzania 11 ma dereva wama lori wamekutwa na corona mpaka wa mtukula na wamerejesha nchini, kwa mjibu wa waziri wa afya ya Uganda .....kwahiyo hao wameachiwa tu wajichanganye na raia wengine au?
 
Hawa jamaa ni bure kabisa. Nani mwenye akili timamu atanunua hii kitu - uongo?! Wagonjwa wameisha, wamepona au wamefariki?
 
So kilichotuponya watanzania ni maombi na sala? Sasa tufunge basi na kusali kwa ajili ya dunia. Tuwaombee na wao basi
Mkuu usidharau maombi na sala. Ulimwengu wa roho una nguvu sana katika ku influence ulimwengu kimwili
 
Back
Top Bottom