KERO Waziri wa Elimu, tunaomba msaada wako. Shule binafsi bweni hawataki tuone watoto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
.....hadi tumefikia kusema hayo tumeona mengi sana...kuna mzazi mwenzetu nusura apoteze mtoto kisa ameugua wakampeleka dispensary jirani na shule wakamuacha anatibiwa hapo....siku 6 mtoto amekaa mwenyewe hospital bila wazazi kujua .....msg ikaja ya bill mtoto akiwa anapewa rufaa ....mzazi anastuka anaenda shule mtoto hayupo.....amepewa tena rufaa....kwa nini hawatoi taarifa ? Kosa kutowaona kabisa kama jela au wapi !!
Kwa suala kama hilo upo sahihi wanakosea. Ila kwa suala la kumuaona mtoto tena wa sekondari kila mwezi bila sababu ya msingi halina mashiko.
Kama ni mgonjwa sawa.
 
Salaam na heshima kwako Mh Waziri Elimu Prof Mkenda.

Awali ya yote nawapa pongezi sana kwa jitihada zenu kuboresha elimu tangu msingi hadi sekondari..hongera sana awamu hii pongezi kwa Mama Samia.

Wazazi tuna malalamiko hasa kwa shule binafsi za bweni shulw msingi na sekondari....kwa nini hawataki na wamefuta utaratibu kutembelea watoto mwisho mwezi ? Kwa kitu gani wanachosoma iwe hakuna ruhusa kuona watoto kujua afya zao na maendeleo yao ?

Naomba Mh Waziri ingilia kati suala hili tumeongea na shule binafsi bila mafanikio naona kila shule wanajiamulia tu, ni haki ya wazazi kuwaona watoto wao mwisho mwezi hata masaa machache.

Asante nakutakia kazi njema
MZAZI
Kwanini mwanao asikae Day tu? Kwanini unapeleka mtoto bweni halafu unataka aishi kwa matakwa yako?
 
Wazazi watatoa watoto wangapi ? Tunaomba Waziri atoe tamko iwe kwa shule zote warudishe utaratibu ule kuwatembelea....hizo biashara zao ni wao..
Mmeshikiwa panga shingoni kwamba lazima wasome hapo?
 
Salaam na heshima kwako Mh Waziri Elimu Prof Mkenda.

Awali ya yote nawapa pongezi sana kwa jitihada zenu kuboresha elimu tangu msingi hadi sekondari..hongera sana awamu hii pongezi kwa Mama Samia.

Wazazi tuna malalamiko hasa kwa shule binafsi za bweni shulw msingi na sekondari....kwa nini hawataki na wamefuta utaratibu kutembelea watoto mwisho mwezi ? Kwa kitu gani wanachosoma iwe hakuna ruhusa kuona watoto kujua afya zao na maendeleo yao ?

Naomba Mh Waziri ingilia kati suala hili tumeongea na shule binafsi bila mafanikio naona kila shule wanajiamulia tu, ni haki ya wazazi kuwaona watoto wao mwisho mwezi hata masaa machache.

Asante nakutakia kazi njema
MZAZI
Wanaficha msione mazingira mabovu tofauti na ada kubwa mnazotoa

Ila yanini unapeleka mtoto bweni?

Kaa na watoto wako bwana,acheni kukwepa ulezi hata kama upo bize kivipi siwezi kaa mbali na watoto wangu,never!
 
Hii ndiyo mada Bora ya mwezi huu....waziri wa elimu angalia hapa najua ukikaa na jopo lako utakuja na suluhisho na watanzania tutakukumbuka kizazi Hadi kizazi
Duh! WaTz bhana! Yan tatizo la mzazi mmoja au la shule moja, tena binafsi; Linamtaka mhashimiwa Waziri wa Elimu aingilie kati kupata suluhisho. Mbona tuko wepesi sana kukuza mambo? Kwani hapo mlipo hakuna Afisa Elimu Mkoa, Wilaya au Mratibu wa Elimu Kata?? Tatizo kidogo tena lililo chini ya uwezo wako mwenyewe Eti unamtaka waziri aingile kati kana kwamba hana majukumu mengine tena ya Kitaifa.
Halafu inafaa ukumbuke ; Mtoto ni wa kwako mwenyewe. Ukiona kuna kutokukubaliwa au ukiona huridhiki na majibu unayopewa na Mkuu wa shule; au kuna longolongo nyingi mbona ni very simple tuu?. Umtake Mkuu wa shule akukabidhi mwanao halafu chap' Ondoka na mtoto wako umpeleke huko ambako wanaruhusu watu kuingia na kutoka shuleni mithili ya nyuki kwenye mzinga wa nyuki.
 
Wakiweka masaa 3 kumuona mara moja mwezi inatosha sana hasa afya akili watoto hasa wa kike....
Issue toa mtoto wako,
Wabongo mna shida, unajua kabisa shule ina shida, unapeleka mtoto wako halafu unataka ubadili utamaduni wao,
Kama unataka kumuona daily mpeleke kayumba
 
Jumamosi na jumapili ni siku ya watu kusali sio kuzurura visiting day kwa watoto
Kwamba watoto wote au wazazi wote wanaabudu siku zote mbili? Ambae hawezi kufika jumamosi afike jumapili au kinyume chake.
 
Huo upuuzi wa shule kujiona wana mamlaka kwa watoto kuliko wazazi wao hata siukubali.

Kuna shule mzazi haruhusiwi hata kuona darasa analosoma mtoto, mimi nikajisemea hamnijui. Nimeenda naona watoto wamekaa wanne hadi watano kwenye bench, yaani nalipa ada mtoto kakalishwa kwenye bench tena watano. No way! Wanarecruit watoto wengi hadi wanashindwa kuwahandle, hiyo biashara hakuna.. mwalimu mkuu akapewa ultimatum, ahakikishe kila mtoto ana kiti na meza yake.
 
Issue toa mtoto wako,
Wabongo mna shida, unajua kabisa shule ina shida, unapeleka mtoto wako halafu unataka ubadili utamaduni wao,
Kama unataka kumuona daily mpeleke kayumba
Nakazia hoja.
1. Haiingii akilini kamba mzazi alienda kwa hiari yake kuomba Fomu ya maombi ili mtoto wake akubaliwe kujiunga na Shule hiyo. Labda hata mtoto alifanyiwa Usaili (Interview)
2. Mzazi alipokea Fomu / Barua ya masharti ya kujiunga (Joining Instructions) na shule hiyo na kutia saini baada ya kukubaliana na maelekezo husika.
3. Mojawapo ya Maelekezo ni namna na ni lini mzazi/mlezi anaweza(sio lazma) kumtembelea mtoto wake.
Sasa:
1. Inakuwaje mzazi au mlezi huyo huyo anakiuka kile alichokubali mwanzoni kabla mtoto hajapokelewa shuleni hapo??
2. Baadhi ya Wazazi/Walezi wengi hawaoni uzuri wa Utaratibu wa kuwaona watoto wao. Wazazi / Walezi wanashindwa kutambua kwamba Shule ni Taasisi au ni Jumuiya na sio Familia. Yale mzazi anayofanya kwenye Familia na mtoto/watoto wake huko familiani asiyalete Shuleni. Lazima suala la Usalama wa maisha ya wakaao hapo liwekewe kipaumbele. Itakuwaje kwa mfano katika utaratibu huo mbovu kabisa wa kuingia na kutoka kiholela Shuleni, mtoto wako ukasikia ametekwa na wasiojulikana? Mkuu wa shule atauficha wapi uso wake endapo atatokea mhuni mmoja kati ya wale wanaoingia na kutoka hovyo akaweka sumu au kitu chenye madhara kwenye chakula cha watoto au maji ya kunywa na kuwadhuru watoto?
Kama mzazi uliuamini Uongozi wa Shule hadi ukakabihi mtoto wako, basi endelea na imani hiyo kwani hata watumishi wa shuleni hapo ni wazazi pia.
Kitendo cha kufika-fika mara nyingi hapo shuleni kina madhara makubwa. Kwa mfano likitokea la kutokea e.g. kuzuka kwa moto, watuhumiwa wa kwanza ni wale wanaofika-fika mara nyingi hapo shuleni kwani hakuna ukaguzi kwa wazazi/walezi/wageni waingiao na kutoka hapo shuleni.
Tena Watoto wana ile Tabia ya "kusemelea" na wengine huongeza chumvi ili hoja yao ikubaliwe. Utamsikia mtoto anasema: "...... ngoja mama aje nita "kusemea".
Hiyo Tabia ni Tabia ya Umbeya. Je, itakuwaje mtoto anamwambia mama yake (naamini wazazi Me ni mara chache sana kuendekeza Tabia hiyo) kwamba mwl. x & y wa hisabati au Fizikia (Mathematics & Physics) hawanipendi n.k.? Hii si italeta chuki baina ya shule na wazazi?
 
Duh! WaTz bhana! Yan tatizo la mzazi mmoja au la shule moja, tena binafsi; Linamtaka mhashimiwa Waziri wa Elimu aingilie kati kupata suluhisho. Mbona tuko wepesi sana kukuza mambo? Kwani hapo mlipo hakuna Afisa Elimu Mkoa, Wilaya au Mratibu wa Elimu Kata?? Tatizo kidogo tena lililo chini ya uwezo wako mwenyewe Eti unamtaka waziri aingile kati kana kwamba hana majukumu mengine tena ya Kitaifa.
Halafu inafaa ukumbuke ; Mtoto ni wa kwako mwenyewe. Ukiona kuna kutokukubaliwa au ukiona huridhiki na majibu unayopewa na Mkuu wa shule; au kuna longolongo nyingi mbona ni very simple tuu?. Umtake Mkuu wa shule akukabidhi mwanao halafu chap' Ondoka na mtoto wako umpeleke huko ambako wanaruhusu watu kuingia na kutoka shuleni mithili ya nyuki kwenye mzinga wa nyuki.
Sawa mkuu nimekuelewa
 
.....hadi tumefikia kusema hayo tumeona mengi sana...kuna mzazi mwenzetu nusura apoteze mtoto kisa ameugua wakampeleka dispensary jirani na shule wakamuacha anatibiwa hapo....siku 6 mtoto amekaa mwenyewe hospital bila wazazi kujua .....msg ikaja ya bill mtoto akiwa anapewa rufaa ....mzazi anastuka anaenda shule mtoto hayupo.....amepewa tena rufaa....kwa nini hawatoi taarifa ? Kosa kutowaona kabisa kama jela au wapi !!

Toeni watoto boarding schools. I understand wazazi wapo busy ila wengi wanapelekea watoto boarding kama sifa.
 
Salaam na heshima kwako Mh Waziri Elimu Prof Mkenda.

Awali ya yote nawapa pongezi sana kwa jitihada zenu kuboresha elimu tangu msingi hadi sekondari..hongera sana awamu hii pongezi kwa Mama Samia.

Wazazi tuna malalamiko hasa kwa shule binafsi za bweni shulw msingi na sekondari....kwa nini hawataki na wamefuta utaratibu kutembelea watoto mwisho mwezi ? Kwa kitu gani wanachosoma iwe hakuna ruhusa kuona watoto kujua afya zao na maendeleo yao ?

Naomba Mh Waziri ingilia kati suala hili tumeongea na shule binafsi bila mafanikio naona kila shule wanajiamulia tu, ni haki ya wazazi kuwaona watoto wao mwisho mwezi hata masaa machache.

Asante nakutakia kazi njema
MZAZI
Mpeleke mtoto wako shule za serikali zipo nyingi sana na zinatoa elimu bora tu.
 
Duh! WaTz bhana! Yan tatizo la mzazi mmoja au la shule moja, tena binafsi; Linamtaka mhashimiwa Waziri wa Elimu aingilie kati kupata suluhisho. Mbona tuko wepesi sana kukuza mambo? Kwani hapo mlipo hakuna Afisa Elimu Mkoa, Wilaya au Mratibu wa Elimu Kata?? Tatizo kidogo tena lililo chini ya uwezo wako mwenyewe Eti unamtaka waziri aingile kati kana kwamba hana majukumu mengine tena ya Kitaifa.
Halafu inafaa ukumbuke ; Mtoto ni wa kwako mwenyewe. Ukiona kuna kutokukubaliwa au ukiona huridhiki na majibu unayopewa na Mkuu wa shule; au kuna longolongo nyingi mbona ni very simple tuu?. Umtake Mkuu wa shule akukabidhi mwanao halafu chap' Ondoka na mtoto wako umpeleke huko ambako wanaruhusu watu kuingia na kutoka shuleni mithili ya nyuki kwenye mzinga wa nyuki.
Hii sio tatizo la shule 1 mkuu
 
Back
Top Bottom