Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin aionya Iran kuwa ikithubutu kujibu shambulizi la Israeli huo ndiyo utakuwa mwisho wake!

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin aionya Iran kuwa ikithubutu kujibu shambulizi la Israeli huo ndiyo utakuwa mwisho wake!

Sasa nimeelewa kumbe hii fire exchange sio baina ya Iran na Israel, badala yake ni US na Iran
Vyovyote vile utakavyoelewa ila Iran asithubutu kujibu.

Mpaka muda huu ni mtuhumiwa so cha kufanya ni yeye kukaa kimya kusubiri uamuzi wa mahakama.
 
Vitisho navyo ni moja ya Silaha nzuri ya kumtia Uoga adui ili asikudhuru!
Kabla ya Iran kuishambulia Israel mara mbili ilionywa,ilitishwa lakini hatimaye ilirusha makombora kuelekea Israel!
Kwa hiyo hata sasa tusishangae Iran ikirusha makombora tena kuelekea Israel.
 
Bado mnasema Israel ndo Taifa Lenye Nguvu...
Anakupiga Mtu halafu onyo anatoa Mwingine Ole wako umrudishie 🤣🤣..
Ina maana anajua Ukimrudishia Watu watajua kuwa hana Nguvu 🤣🤣 kama anavyosifiwa
Hii inanikumbusha shule ya msingi dogo wa darasa la tatu anakuja kukupiga kibao sasa rudishia ushuhudie kisago cha mbwa mwizi.
 
Asante sana!
Hapo Zamani Marekani Ilikuwa inakaliwa na Wahindi wekundu au Tunaweza Kuita Red Indian au Red indians..

Na Ilikuwa Ikiitwa Turtle Island Vipi na wenyewe Wanaruhusiwa Kurudi na Kudai Nchi yao kutoka kwa Wamarekani baada ya kukaliwa kwa Miaka zaidi ya 800 bila Wao kuitawala?
Hao wenyewe wa kuitwa Waisrael pale ni kwao au babu yao kiimani naye alivamia tu kama wavamizi wengine wa kizungu marekani wanapopaita kwao ?!
 
Ndiyo, kama Urusi wameonyesha hadi noti ya Brics wakitaka kuondoa utegemezi kwa dola itakua sahihi kuassume kwamba wanahitaji wanachama zaidi katika hili kusudio. Iran hatonyimwa msaada ila hautakua mkubwa au hautakuja kwa wakati
Kwani Tanzania chini ya Umoja wa Afrika hawawezi kukaa kikao na kuonyesha noti yao ya Umoja wao na wakisema itakuwa mbadala wa dollars?
 
Nini kitashindikana kama mlengwa akili zake ni zilezile na mbinu hizohizo?
Mwaka wa ngapi huu US anahangaika na IRAN, Wakati Saddam ilimchukua miaka 13 tu kumsambaratisha.
Kama huoni utofauti wa IRAN na Utawala wa Saddam kijeshi, kiuchumi na kiushawishi na mabadiliko ya uendeshwaji wa mambo duniani sitakua na msaada tena baada ya posti hii.
 
Wala hata vita ya 3 haifiki Iran atakua kesha pasuliwa, simu zinatembea mataifa yote ya magharibi kimya kimya jinsi ya kumalizana nae kabla hajafikia level ya Kim kiduku, Uzuri walikua wanamtafutia sababu nae kwa ujinga kajiingiza mtegoni
amakweli sasa naanza kuamini israel ndo itakayokuwa chanzo cha vita ya 3 ya dunia
A aaa
 
Hatutaki maneno mengi,Iran ijibu shambulizi na si vinginevyo.
Umenikumbusha siku nyingi sana tukiwa shule ya msingi.Wanafunzi wenzetu walipokuwa na ugomvi wa maneno tuliwachukua na kwenda kuwapiganisha uwanja wa dhambi nje ya eneo la shule hadi mmoja apigwe hasa.Kwa ufupi tulikuwa wachonganishi
 
Safari hii iran ifyate mkia tu ili ibaki salama. Ikijibu itadhalilishwa vibaya,
 
Wadau hamjamboni nyote?

Jisomeeni


US defense chief: Iran ‘should not make the mistake of responding to Israel’s strikes’

By Reuters

“Iran should not make the mistake of responding to Israel’s strikes, which should mark the end of this exchange,” Austin says in a statement.
Kiingereza kimekutupa mkuu.. Austin kasema hii iwe mwisho wa kushambuliana na sio Mwisho wa Iran.. sawa sawa
 
Waliambiwa na nani na sababu ilikuwa ni nini?
Waliambiwa na Mungu wao...sababu wakiwaacha hawatoishi kwa amani.

Tuletee wewe historia inayoonyesha Israel haikuvamia hapo middle east
Wala hata vita ya 3 haifiki Iran atakua kesha pasuliwa, simu zinatembea mataifa yote ya magharibi kimya kimya jinsi ya kumalizana nae kabla hajafikia level ya Kim kiduku, Uzuri walikua wanamtafutia sababu nae kwa ujinga kajiingiza mtegoni

A aaa
Mshachelewa.
 
Back
Top Bottom