evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,989
- 9,948
Kwenye comment yangu hiyo nimeainisha Mambo mawili:
1. Dhana ya Ndoa
2. Chumo la Ndoa.
NB: Muunganiko wa Ndoa siyo Ubia wa Kibiashara Wala siyo suala la muunganiko wa Watu wawili kwa lengo la kumiliki Mali kibiashara. La hasha!
Suala la Dhana ya Ndoa limeingizwa kwenye Sheria ya Ndoa makusudi kabisa kwa lengo kusimamia mgawanyo wa Mali (chumo la ndoa) wakati wa wachumba kuachana au mgawanyo wa mirathi pale 'mchumba' mmojawapo anaporariki.
Huwezi kuingiza dhana ya ndoa kwa mtu ambaye ameshafunga ndoa kanisani hiyo ndoa yenu inakuwa null and void..
Mimi nimefunga ndoa kanisani halafu nikamtelekeza huyo mwanamke bila talaka ,nikamchukua mwanamke mwingine hata kama tukiishi miaka zaidi ya ishirini na kuzaa watoto kisheria hiyo haitambuliki hata kwa kutumia dhana ya ndoa kwani sheria imekataza hilo suala embu tafadhali soma tena hiki kifungu na ukielewe vizuri