Wengi wanahoji wake wa Spika Job Ndugai, na kuona mmoja amesahaulika


Huwezi kuingiza dhana ya ndoa kwa mtu ambaye ameshafunga ndoa kanisani hiyo ndoa yenu inakuwa null and void..
Mimi nimefunga ndoa kanisani halafu nikamtelekeza huyo mwanamke bila talaka ,nikamchukua mwanamke mwingine hata kama tukiishi miaka zaidi ya ishirini na kuzaa watoto kisheria hiyo haitambuliki hata kwa kutumia dhana ya ndoa kwani sheria imekataza hilo suala embu tafadhali soma tena hiki kifungu na ukielewe vizuri
 

Attachments

  • Screenshot_20250807_231330_Chrome.jpg
    228.1 KB · Views: 18
Suppose, chakula, hapiki, nguo hafui, na hakuchangia hata senti still atakuwa na umiliki? na hivi niulize suppose mke naye amejenga nyumba na mume hakutoa hata sent je mke akifa mume atakuwa mrithi wa hiyo nyumba ya marehemu mkewe?

Je, unayo hukumu ya Mahakama inayothibitisha kwamba umewahi kumshitaki mke wako kwa kosa la kushindwa kukupikia chakula kwenye ndoa yenu??
 
Mtu kama ndugai kuumwa hadi kuwa india lazima alishaandika urithi huku nyuma wasisumbuane

Ulikuwa unamaanisha kaandika wosia kiingereza will.
Hilo litakuwa jambo jema ila kuna taratibu za kufuata za kuandika wosia .
Sio kila wosia unakubalika mahakamani .
Mahakama ikiona wosia haujakaa vizuri unatupiliwa mbali
 

Sikia, huyo Job Ndugai tayari walishatengana muda mrefu Sana na huyo Mwanamke wake wa kwanza, walikuwa hawaishi pamoja tena. Je, unataka kusema kwamba Job Ndugai alikuwa Hana haki ya kujitafutia Mali zake baada ya kutengana na huyo Mwanamke wake wa kwanza??


Hizo Mali ambazo Job Ndugai amechuma pamoja na huyo Mwanamke wa pili, Je, huyo Mwanamke wake wa kwanza zinamhusu nini hata kama aliwahi kufunga ndoa na Job Ndugai??????
Hapa ndipo suala la Dhana ya Ndoa inapoingia kwenye Hoja hii.

Please elewa vizuri scenario ya Kesi hii
 
Suppose, chakula, hapiki, nguo hafui, na hakuchangia hata senti still atakuwa na umiliki? na hivi niulize suppose mke naye amejenga nyumba na mume hakutoa hata sent je mke akifa mume atakuwa mrithi wa hiyo nyumba ya marehemu mkewe?

Ndio manake kuna kesi moja ya ajabu sana .
Kuna tajiri alifariki akaacha mali nyingi sana pamoja na mke na watoto.
Sasa mali zile zote ndugu wa.marehemu wakaona azirithi mjane (mke ) wa marehemu .Mali nyingi za maana maghorofa ,mashamba ,maduka .
Sasa yule mke wa marehemu katika kuishi akapata mzee mwenzake yule mzee alikuwa hana kitu naye kafiwa na mke wake.
Sasa yule mjane wa marehemu tajiri na yule mzee wakaamua kufunga ndoa tena kanisani.

Sasa yule.mwanamke tajiri naye akafariki yule mume wake mpya akafanya taratibu za mirathi ya mke wake ambaye mali zake nyingi alirithi kutoka kwa mume wake.
Ndugu wa yule mwanaume wa kwanza tajiri walipinga sana na kwenda kumshtaki yule mzee kwamba hastahili kurithi mali za yule mama kwani zilikuwa za mwanaume mwingine ndugu yao
Kesi ikasikilizwa ikaonekana yule jamaa ni mume halali wa yule mama so anastahili kurithi mali zote za mke wake .

Sasa hivi Yule mzee tajiri na kaoa tena mwanamke mwingine kupitia mali alizorithi kutoka kwa mke wake
 

Hiyo ni sahihi kabisa, Mahakama iliamua vyema kabisa.

Kisheria, umiliki wa Mali za Chumo la Ndoa kwa kawaida hubaki kwa Mwanandoa aliyebaki hai, kwa kiingereza Hali hiyo huitwa The Right of Survivorship. Mwanandoa anayetangulia kufa kisheria anahesabiwa kama "AMEUKIMBIA URITHI."
Hivyo Basi, kwenye suala hili, Marehemu Job Ndugai kisheria anahesabika kwamba AMEUKIMBIA URITHI, kwa hiyo Mali zake za Chumo la Ndoa (endapo kama zipo) umiliki wake utahamia kwa Mwenza wake aliyebaki hai ambaye alichangia jasho lake kwenye upatikanaji wa Mali hizo.
 

Naomba nikujibu kwa kifupi sana .
Ndoa yakikristo ni ishu nzito .
Ukioa kikristu ukiona umeingia chaka mwanamke hakufai fanya juu chini hakikisha unafight hadi upate talaka kutoka mahakamani. Ni ishu ngumu ila siku hizi zinatoka
Kinyume chake ni kifungo hautakuwa huru na wala mali zako hazitakuwa huru hadi huyo mwanamke afe.
Ikitokea umetangulia wewe kufa huyo mwanamke mwenye ndoa ya kikristo anaweza kuamua kudai na itabidi apewe mali zako zote ulizoacha na mahakama.
Mkataba wa ndoa si suala la.mchezo ,tatizo wa bongo wengi wamezoea kuoa na kuacha hovyo hovyo na wanawake wengi wanaowaoa na kuwaacha kienyeji hawajielewi hawafatilii haki zao .
Kisheria huwezi kuwa kwenye mkataba wa ndoa ya kikristu ukaingia kwenye mkataba mwingine eti kwa kutumia dhana ya ndoa

Embu msikilize huyo kabudi kidogo
 

Mahakama ni za Sheria na Ushahidi.

Kwenye suala hili la Marehemu Job Ndugai kuna ushahidi wa wazi kabisa kwamba huyo Mwanamke wake wa kwanza tayari walishatengana muda mrefu Sana, kila mmoja alikuwa anaishi kivyake na Wala hapakuwa na ushahidi wowote ule wa kwamba Watu hao walikuwa wanachuma Mali zao kwa pamoja Mara baada ya kutengana.
Hivyo Basi, huyo Mwanamke wake wa kwanza Hana Haki kabisa ya kuweza kudai mgawanyo wa Mali za mirathi ambazo Job Ndugai alizichuma Mara baada ya kutengana kwao.

Zile Mali walizochuma wote kabla ya kutengana ndio pekee ambazo anaweza kudai mgawo wake
 
Kwa Watanzania wanavyopenda vitu vya kurithi utakuta Dkt Fatuma naye anakimbilia mahakamani kudai mali za Ndugai ziwe zake wakati hajazaa naye hlf akijua kbs Bi Stella ni mke halali wa Ndugai na amezaa naye watoto watatu.
Kwahiyo kama hajazaa naye hapaswi kupewa urithi toka Kwa mmewe?
 

Ukitengana tu na mke hilo lipo hata kisheria na bado atatambulika kama mke rasmi.
Mke ataachwa kwa hati ya talaka mahakamani.
Kuna mzee tulikuwa tunaishi naye jirani alitengana na mke wake akamfukuza kabisa yule mwanamke akarudi Kwao .
Yule mzee akabaki na watoto wake 2 aliozaa na mwanamke mwingine ambaye hawakuoana wala halikuwa haishi naye .
Huyo mwanamke ambaye alimuoa na kumfukuza hakuwahi kuzaa naye.
Yule mzee alipomfukuza Yule mwanamke akamchukua mwanamke mwingine wakawa wanaishi kama mke na mume ila hawakufunga ndoa.
Sasa yule mzee akaja kufariki nakuambi yule mwanamke alikuja kurudi na kudai mali ,yule mzee aliacha nyumba kesi iliendeshwa mahakamani mwisho hukumu ikatoka mahakama ikamtambua yule mwanmke aliyefukuzwa kama mke halali wa ndoa wa yule mzee akamilikishwa nyumba ya yule mzee .
Hadi sasahivi yule mwanamke anaishi kwenye hiyo nyimba ya huyo mzee na ameolewa hapo anaishi na mwanume mwingine wale watoto wa yule mzee wameamua kuondoka wenyewe kwenye hiyo nyumba mahakama iliamuru wana haki ya kuishi hapo wakitaka ila sio kuirithi hiyo nyumba .
Mke anaachwa kwa hati ya talaka sio kutengwa ukimtenga mke bado anahesabika kama mke wako
 

Je, una elimu ya kiwango gani hasa wewe? Je, una elimu yoyote ile ya Sheria hata kwa level ya Foundation Course???

Nakushauri Usome kuhusu masuala ya HAKI za Mali za Chumo la Ndoa (Matrimonial Property) katika Sheria ya Ndoa pamoja na Sheria za Usimamizi wa Mirathi.

Kwa kawaida, kila Kesi huwa inaamuliwa kutokana na facts zilizopo katika Kesi husika.

"No research no right to speak."
By Mao Zedong
 




Poa.
 

Poa.

Namshukuru Allah kwa Neema ya Uislam.
 
Je, unayo hukumu ya Mahakama inayothibutisha kwamba umewahi kumshitaki mke wako kwa kosa la kushindwa kukupikia chakula kwenye ndoa yenu??
Ikiwa mke anafanya kazi ya kuajiriwa ambapo anaondoka saa 11 alfajiri na anarudi saa tatu usiku jumatatu to jumamosi hivi kwa mazingira haya itahitajika hukumu ya mahakama🤣😂 na hapo kuna dada wa kazi na ambapo mume ndiye anayemlipa🤣😂
Hata watoto wanajua mama yao hapikagi, hafui🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…