Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Sasa hivi tuna kundi la vijjana wavivu wapendwa kitonga. Wanataka wapate wenza wawasidie kulea familia, wakati huo huo wanataka wapate heshima ya mwanaume ndani
Huwezi kupata heshima hiyo, mifano tunayo Mingi mitaani, ni shida tunajua ila watu wanataka kujitoa ufahamu
 
Kwa hiyo wewe unafikiri Samia alitoka nje nyumbani kwao kwenda kutafuta kazi au aliitwa tu na kuambiwa kaa hapa ule mema ya nchi?

Vipi mme wake anajivunia na ana furaha ya kutosha sababu mkewe ni Rais?

Kwahiyo Samia, from familia ya billionaire Kizimkazi 😅, kwao hawakutaka awe goli kipa wakamtafutia kazi ila Wewe usiye hata na urithi wa uchawi unataka binti yako awe goli kipa? utakua sio mzima.

Mme wake anajivunia hajivunii mimi na wewe hatujui. Ulitaka mme wake ajivunie mke goli kipa badala ga Rais? Mme wa hivyo ni zwazwa.

Ukitoka familia maskini utaona umaskini ni kawaida. Ukitoka familia ya Kati utaona kuwa na hela ni jambo la kawaida.

Probably umekua mazingira ya ugoli kipa kwako ugoli kipa ni kawaida and I strongly believe unaandaa mwanao awe goli kipa Bora kwa mme wake na mkeo ni nyanda zaidi ya Onana.

Kwetu ugoli kipa ni mwiko. Mwanamke hawezi kuwa goli kipa na ni mwiko kuoa goli kipa. Mimi nawewe can't see eye to eye. I rest my case.
 
Wewe ndiyo hujielewi kabisa

Hapa tunazungumzia wanawake walioajiriwa siyo wanaofanya kazi za kuosha vyombo au kufua nguo nyumbani, hata kuna mjumbe amekufafanulia hapo juu kuwa siongelei kazi za usafi nyumbani wewe bado unawaza kazi hata za kupika nyumbani nazo unaita kazi
Mkuu
Embu nitafutie sehemu Robert Heriel Mtibeli alipoandika hapa tunazungumzua wanawake walioajiriwa?

Embu nionyeshe sehemu uliposema kwamba Mke wako atafanya kazi lakini si za kuajiriwa?
Si wewe ulisema kazi ni kula, kulala na mazoezi ya viungo?
 
Ana comprehension disorder. Kama ni billionaire wajiulize kwanini alikubali kuolewa mke wa pili na hakutaka kukaa nyumbani kuwa goli kipa?

Ujinga wanadhani tumemjua Samia juzi kumbe na sisi tuna file lake lote. Hizo story zao za vijiweni won't cut it here.
baada ya kuona kaandika ujinga kakimbilia hoja ni wanawake walioajiriwa lakini mtoa mada hajasema hivyo kwamba ni wanawake waajiriwa tu kasema kufanya kazi

nimeachana nae huenda pia umri unasumbua.
 
WENGI WANAOTAKA WAKE ZAO WASIFANYE KAZI WANAUPEO MDOGO WA KUFIKIRI ALAFU NI WABINAFSI

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Chizi sio lazima uokote Makopo, kuna Chizi Fresh ambao ndio wengi wapo kundi hili tena wengine wasomi. Alafu kuna ambao ni Chizi Maarifa hawa wengi ukiwaona kwa mbali unaweza kudhani wako timamu lakini ukiwatazama kwa ukaribu ni wendawazimu.

Unakuta kajamaa kametoka familia Maskini, kameoa kutoka Familia Maskini. Kanafanya kazi iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri lakini pato lake kwa mwezi hata Milioni moja halifiki.
Lakini ukikasikiliza mawazo yake kuhusu uchumi na mahusiano utabaki kuona kalivyo na upeo mdogo.

Yaani kisa umenunua mwanamke kwa bei ya jumla(kutoa mahari) labda shilingi milioni nne. Basi Mwanamke huyo ambaye sasa ataitwa mkeo unasema asifanye kazi kisa umemuoa.

Ukiulizwa kwa nini asifanye kazi? Huna hoja ya maana hata moja zaidi ya kutokujiamini, ubinafsi na ukandamizaji kama sio unyanyasaji.

Unamwambia mkeo asifanye kazi au asimiliki kipato kingi tena inafikia hatua kwa uzuzu wako unamhujumu mkeo na kumuwekea vikwazo ili asifanikiwe. Ati unaogopa atakunyanyasa ati atakuwa jeuri. Chizi weeeh!

Mkeo asifanye kazi, unapesa za kumhudumia mahitaji yake yote?
Alafu wengi wenye mtazamo kama huu unakuta Wake zao hata mafuta ya kupaka hawana, nguo wanazovaa mtumba, tena bora mtumba lakini ziwe nyingi. Lakini hata pesa ya kuwanunulia wake zao nguo walau kila mwezi nguo moja au mbili hawana. Mke kapauka, kazeeshwa. Yaani hatamaniki tena. Kila siku kumlisha mkeo Maharage kazi kujambajamba. Alafu unakuta jitu linasema linahudumia mke. Alafu halitaki mkewe afanye kazi. Ili angalau pesa ya kubadilisha chakula hapo nyumbani iwepo sio kila siku ugali na mchicha au maharage. Nyama na samaki mpaka sikukuu. Familia inapitisha Wiki hata maziwa hakuna. Alafu ulivyo chizi unaona sawa tuu. Alafu ukijaribu mtandaoni huku ooh! Mwanamke asifanye kazi utadhani umemudu mahitaji yake. Mwehu wewe!

Watoto wako ada zenyewe zinakusumbua, lishe yenyewe hawali. Utapiamlo na kifaduro kinawasumbua. Watoto mpaka imefikia hata uwezo wa kufikiri hawana Kwa sababu kila siku unawalisha chakula kingi cha wanga kama ugali, mihogo, maandazi na maujiuji ya nafaka. Ilhali kiafya watoto chini ya miaka 20 wanatakiwa kula protein nyingi kuliko kundi jingine la chakula ili miili yao ijengwe vyema. Vyakula vya protini ambavyo vinatakiwa viwe vingi katika mlo wenu hapo nyumbani ni Samaki, nyama, maharage, maziwa, mayai n.k.
Lakini kwa vile kipato chako ni duni huwezi kuhudumia hivyo. Alafu kwa vile tayari unakifaduro cha ubongo huoni kama unahitaji usaidizi na kwa ubinafsi wako unataka watoto wako nao wakose lishe kama wewe ulivyokosa. Ati mke asifanye kazi au asikusaidie majukumu. Kwa huduma gani unazotoa mwehu wewe!

Haya, mshahara wako wenyewe haukutoshi kutunza Wazazi wako.
Alafu hutaki mkeo asifanye kazi. Hivi unafikiri wazazi wake mwanamke watahudumiwa na kutunzwa na nani kama sio huyo mke wako. Mbuzi wewe.

Pesa yako hata milioni moja haifiki kwa mwezi. Unataka wadogo wa mkeo wahudumiwe na nani?
Unataka ile nyumba ya wazazi wa mkeo ifanyiwe ukarabati na nani kama sio mkeo.

Alafu haya machizi Fresh hapohapo unayasikia yakisema, usijenge Ukweni, mara Usitoe pesa Ukweni. Alafu hapohapo unayakuta yanazuia Wake zao wasifanye kazi. Hivi kama sio Ushetani na laana hizo ni kitu gani? Hivi kuna ubinafsi na ukatili wa kutisha zaidi ya huo?

Bado umfulishe na kumfanyisha makazi mengi bila kumpa lishe bora. Zaidi ya hapo umpige kisa ameona mambo sio mambo na umemgeuza msukule wake hapo.

Embu acheni Upumbavu wenu.
Ni mara elfu Mwanamke asioelewe au awe single Mother alee Watoto wake kitabutabu kuliko kuishi na mwanaume mwenye Ushetani wa namna hiyo.

Mwanaume elewa kuwa kama wewe unavyopenda na kuhitaji kuhudumia Wazazi wako ndio hivyohivyo mkeo naye anataka wazazi wake wahudumiwe.

Na ndio maana Watibeli Hawatoi Mahari kwa sababu inaharufu ya manunuzi au biashara ya binadamu kwa visingizio vya kishetani.

Hutaki mkeo afanye kazi alafu ukiombwa pesa ya kuwasomesha wadogo zake unapiga yowe na kulalamika. Wewe mwehu nini.

Na mimi nawaambia Wanawake hasa Watibeli ni lazima wafanyekazi. Kufanya kazi ni amri ya kila kiumbe ili kiwe huru na kujitegemea chenyewe. Binadamu asiyefanya kazi ni mfu.
Mtu mwenye akili na Mwanamke kamili na mke mwema hujisikia aibu na fedheha kumtegemea mumewe kwa kila kitu.

Mimi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Uliweza kuandika paragraph chache sana ila umeandika paragraph nyingi inaonesha kuna mwana kamchukua dada ako alaf anampausha 😂😂.

By the way upo sahihi kama huna kipato kikubwa mruhusu mke wako afanye kazi msaidiane.

Pia omba radhi haraka iwezekanavyo milioni nne sio ndogo.Mimi ntaoa kwa mahali ya alfu tisini na mia mbili tu.Tafadhali usinitengeneze mazingira magumu 😁
 
Kwahiyo Samia, from familia ya billionaire Kizimkazi 😅, kwao hawakutaka awe goli kipa wakamtafutia kazi ila Wewe usiye hata na urithi wa uchawi unataka binti yako awe goli kipa? utakua sio mzima.

Mme wake anajivunia hajivunii mimi na wewe hatujui. Ulitaka mme wake ajivunie mke goli kipa badala ga Rais? Mme wa hivyo ni zwazwa.

Ukitoka familia maskini utaona umaskini ni kawaida. Ukitoka familia ya Kati utaona kuwa na hela ni jambo la kawaida.

Probably umekua mazingira ya ugoli kipa kwako ugoli kipa ni kawaida and I strongly believe unaandaa mwanao awe goli kipa Bora kwa mme wake na mkeo ni nyanda zaidi ya Onana.

Kwetu ugoli kila ni mwiko. Mwanamke hawezi kuwa goli kipa na ni mwiko kuoa goli kipa. Mimi nawewe can't see eye to eye. I rest my case.
Wapi walimtafutia kazi wewe? Hivi yule Rais wa Zanzibar sasa unafikiri amewahi kutafutiwa kazi?

Kuna tofauti Kati ya kutafutiwa kazi na kuitwa tu unaambiwa kaa hapa kula mema ya nchi.

Mke kukaa nyumbani siyo lazima awe gorikipa, anaweza kukaa nyumbani na akafanya kazi na computer yake remotely! Wewe umekariri kufanya kazi lazima upande daladala

Pia hizo kanuni ulizojiwekea wewe na familia yenu siyo sheria ya nchi kwamba lazima kila mtu azifuate, ziishi wewe, usilazimishe kila mtu

Na kama huna uhakika kama mmewe ana furaha au hana sababu mkewe ni Rais basi nakushauri upunguze hiyo sauti ya subwoofer yako
 
Mwanamke ni pambo hatakiwa kufanya kazi yeyote zaidi yakumburudisha mume wake.

Ukishamuoa mwanamke amebadili koo, kutoka ukoo wao kuja upande wa mume, ndio maana wengine hubadili mpaka majina ya wazazi wao.

Baada yakumuoa apaswa kufata Sheria na taratibu za upande wa mumewe, hayo yakuhudumia ndugu zake sijui wadogo zake nimambo ya ziada. Mnapooana jukumu kubwa nilakuangalia familia yenu nyinyi wawili nakujenga mpango mkakati wa watoto wenu baadae waishije. Kila mtu akianza kuhudumia nakutoa kipaumbele kwao hapatakua na familia tena.

Kila mtu ajenge kwao, Kila mtu awe anatuma hela kwao, kwenu nyie wawili mtapajenga lini?.

Mwanamke akikubali kuolewa basi ajue na atambue anaenda kufata taratibu na Sheria za mumewe kama hayupo tayari basi asikubali kuolewa.

Sisi wengine tunaamini hata kama niko wrong basi mwanamke anafaa kunisikiliza na kutii nilichokisema.

Ndio maana Koo nyingine wanaume hawali chakula sehemu Moja na wanawake jiulize Kwa nini?. Hili nikuwafunza watoto wakiume na kike Kila mtu kujua majukumu ya baba yake na mama yake niyapi , na namna mwanamke anavyopaswa kumtii na kumuandalia chakula mumewe.

Majukumu yamwanamke ndani ya nyumba yanafahamika na majukum ya mwanamme ndani ya nyumba yanafahamika, Sasa ukitaka kila upande uingilie majukumu ya nwenzake hapatotosha, ndio maana familia nyingi zinaparaganyika Kwa Kila upande kuona unaweza kuhimili kufanya majukumu ya mwenzake.

Kila mtu aishi nakufanya yale ambayo anatakiwa kufanya nakutekeleza majukumu yake.

Nakipindi unaoa au kuolewa basi mwenzi wako ajue lengo ni nini hasa, mimi nikitaka kuoa basi lengo nimke wangu aagalie watoto basi, mengi kama yakija basi niyaziada. Lakini lengo kuu lazima hata yeye alifahamu Kwa mantiki kwamba anaolewa kuja kuwa mama wa nyumbani.
Mwanangu umeandika kitu pow kwa 100%
Afu we ntibeli tukuambie jambo moja
Shida ya wanaume Sio kazi/pesa ya mkeo
Hatuna shida nazo wala mipango nazo
Shida inakuj pale ambapo atashindwa kutumiza MAJUKUMU YAKE kwa kigezo cha kutafuta hela
 
Kwani akifanya kazi hawezi kuwa pambo au kumburudisha mumewe?

Kuna wanawake wanaofanya kazi na bado ni warembo kuliko wanaokalizwa nyumbani.
Hoja yako haina mashiko
Kuna office moja nawasaidia biashara zao kiufundi 99% ya wanawake mle ndani wanatembea na staff wenzao tena wengine wamepata kazi kwa kutembea na mabosi wao na wana pete za ndoa kabisa,huo ni mfano mmoja wapo ambao naujua kabisa.
Omba sn unifikie huko mkuu things are worse at the moment huko maofisini
 
Mkuu
Embu nitafutie sehemu Robert Heriel Mtibeli alipoandika hapa tunazungumzua wanawake walioajiriwa?

Embu nionyeshe sehemu uliposema kwamba Mke wako atafanya kazi lakini si za kuajiriwa?
Si wewe ulisema kazi ni kula, kulala na mazoezi ya viungo?
Wewe acha kunipotezea muda wangu

Mimi NIMESEMA NIKIJA KUJAALIWA NA MUNGU kuwa bilionea MKE WANGU SITAKI AFANYE KAZI YOYOTE HATA KUPIKA TU, KAZI YAKE KUBWA NIMESEMA ITAKUWA NI KULA, KULALA NA KUFANYA MAZOEZI.

KAMA UNAPENDA KUENDELEA NA MALUMBANO ENDELEA ila mimi huo ndiyo msimamo wangu na usianze kunisumbua eti nikutajie nani hafanyi kazi kwani umenilipa chochote au hata kuninunulia tu bando?

Na nimesema nikija kuwa Bilionea, sijasema nikiwa milionea, hujiulizi kwanini nimesema hivyo?

Kama hujawahi kuona mtu asiyefanya kazi basi subiri niwe bilionea utamuona mke wangu kwa mara ya kwanza
 
Wapi walimtafutia kazi wewe? Hivi yule Rais wa Zanzibar sasa unafikiri amewahi kutafutiwa kazi?

Kuna tofauti Kati ya kutafutiwa kazi na kuitwa tu unaambiwa kaa hapa kula mema ya nchi.

Mke kukaa nyumbani siyo lazima awe gorikipa, anaweza kukaa nyumbani na akafanya kazi na computer yake remotely! Wewe umekariri kufanya kazi lazima upande daladala

Pia hizo kanuni ulizojiwekea wewe na familia yenu siyo sheria ya nchi kwamba lazima kila mtu azifuate, ziishi wewe, usilazimishe kila mtu

Carry on. Not worth my time.
 
Wewe acha kunipotezea muda wangu

Mimi NIMESEMA NIKIJA KUJAALIWA NA MUNGU kuwa bilionea MKE WANGU SITAKI AFANYE KAZI YOYOTE HATA KUPIKA TU, KAZI YAKE KUBWA NIMESEMA ITAKUWA NI KULA, KULALA NA KUFANYA MAZOEZI.

KAMA UNAPENDA KUENDELEA NA MALUMBANO ENDELEA ila mimi huo ndiyo msimamo wangu na usianze kunisumbua eti nikutajie nani hafanyi kazi kwani umenilipa chochote au hata kuninunulia tu bando?
sasa mkuu. Kwanini unakuwa muongo kusema kwamba tunajadili waajiriwa wakati hakuna sehemu ipo specify kwa hilo.

soma tena mada kwa utulivu.
 
Nasema hivi katika watoto 3 wa mwanamke anayefanya kazi ofisi tofauti na mume wake 1-2 si wa bwana wake.
Akapime DNA atarudi amevimba
😂😂😂😂Nipo huku labda wabibi kuanzia miaka 50 kwenda mbele ila hawa kushuka chini wanachezewa sana hizi safari ...Mara kukumbatiana yaani huku watu wana makoloni yao mapya
 
Mleta mada bado mtoto asilaumiwe,mada zake toka nilipoujua umri wake siku hizi nasoma heading tu.

Usually elimu ya maisha kila mtu huipata automatically jinsi umri wa kukaribia majukumu fulani unapofika,ni kusema kijana akiwa aged 27-30 (umri danganyifu wa tamaa za ujana wenye ndoto nyingi za mahusiano bora na mazuri,ambazo mara nyingi huwa ni uwongo ) siyo rahisi mimi niliye 40 na niko full experienced ku-paste chochote kwenye ubongo wake hadi akija kufika hiyo 40 ndiyo anakutana na yale aliyoambiwa akiwa 27....

Ndiyo anakuja kugundua anhaa,kumbe wakati ule bro alikuwa na maana hii?nae atapambana kwa namna yake atachomoka au atapotea hivi ndivyo maisha yalivyo so mleta mada apewe muda.
 
Mleta mada bado mtoto asilaumiwe,mada zake toka nilipoujua umri wake siku hizi nasoma heading tu.

Usually elimu ya maisha kila mtu huipata automatically jinsi umri wa kukaribia majukumu fulani unapofika,ni kusema kijana akiwa aged 27-30 (umri danganyifu wa tamaa za ujana wenye ndoto nyingi za mahusiano bora na mazuri) siyo rahisi mimi niliye 40 ku-paste chochote kwenye ubongo wake hadi akija kufika hiyo 40 ndiyo anakutana na yale aliyoambiwa akiwa 27....

Ndiyo anakuja kugundua anhaa,kumbe wakati ule bro alikuwa na maana hii?nae atapambana kwa namna yake atachomoka au atapotea hivi ndivyo maisha yalivyo.
Na ni post nyingi anazopost huwa ni utumbo tu, siku nyingi namfuatilia ana EGO kubwa sana na hajijui
 
sasa mkuu. Kwanini unakuwa muongo kusema kwamba tunajadili waajiriwa wakati hakuna sehemu ipo specify kwa hilo.

soma tena mada kwa utulivu.
Soma tena msimamo wangu, achana na mambo ya mada

Mimi Mungu akinijaalia kuwa bilionea sitaki mke wangu afanye kazi yoyote hata kupika tu, kazi yake kubwa itakuwa ni kula kulala na kufanya mazoezi.

Na hakuna wakunibishia hata huyo mke mwenyewe
 
Back
Top Bottom