Wizi wa catalytic converter kwenye magari 'Masega'


Sidhani kama ni kweli nemc ni vilaza hata kama ningekuwa mimi nisingeruhusu hizo sheria hapa Tanzania, hayo ni mambo ya Ulaya, USA na Japan kwa sasa, hata Uchina wenyewe bado wanaruhusiwa ku polute mpaka 2030, sisi bado hatujafikia huko tukianza mambo ya green economy sasa hivi tutakuwa fukara wa kutupwa,hatuwezi kumudu, green economy ni expensive sana na siyo kwa nchi zinazoendelea kama sisi, ...
 

Haha unajiandaa kulinda masega kumbe
Unakuja kupata gari technology ishabadilika..
Hakuna tena masega..
 
Si masega tu hutolewa,mafundi wasio waaminifu,hubadilisha kitu chochote Cha thamani na kukuachia chakavu,feki au kibovu.
Cha msingi Ni kuwa na fundi/mafundi waaminifu..
 
Ina maana kutoka kwa maji inaweza kuwa ishara ya masega kuwepo?
 
Ukilinda masega utapigwa vitu vingine ambavyo huvijui.Cha msingi miezi miwili kabla ya kununua gari jifunze kila kitu kilichopo kwenye gari pamoja na kazi/matumizi yake,athari kikikosekana,etc.Nakumbuka mara yangu ya kwanza kununua pikipiki sikuwa najua kuendesha,sasa nilienda kununua mbali na nyumbani kama kilomita 200 hivi.Sasa nilimtafuta mtu anaejua kuendesha ili anisaidie kuileta nyumbani.

Mwenye duka akaitoa kwenye box na kuifunga kisha yule dereva akaweka mafuta na kuniambia kuwa tuanze safari.Nilishangaa sana kwa sababu tulikuwa hatujaweka oil!Nilivyomuuliza kuhusu hilo ndiyo akaenda kununua oil.Maana yake tungeendesha pikipiki kilomita 200 bila oil na tungeua injini.Pona yangu ni kuwa kabla ya kwenda kununua hiyo pikipiki nilijifunza kwanza kila kitu kuhusu pikipiki.
 


Nimekupenda bure.. bado hujapata gari ila unajua hadi kupress bush... sikutegemea kusikia hilo neno kwa mdada.. nakumbuka kuna chalenge ilitolewa kwenye party moja kwa wadada 20 wenye magari.. atakaepatia kucheki oil ya gear box anapata zawadi laki 3... wote walishindwa walipofunguliwa bonet ya gari zao
 
Aisee thank you mi nishawahi kufanya kazi garage so kuna vitu kiasi najua,jua😀😀 , huwezi kunipiga sana mzinga.
 
Duh km 200 bila oil aisee,bora uligundua hilo mapema. Ni kweli ni muhimu atleast upate basics za vitu muhimu kwa chombo chako. Ila mafundi bana utambana wee ila atakupiga kwe spares ukiwa hapo hapo hutaamini.
 
Hapa siwezi kukubaliana na wewe, kuna wadau mwanzo wamesema kazi yake kubwa ni kupunguza emission ya gas chafu ili kupunguza uchafuzi wa mazingira. Ndo maana watu wamekua wakitumia magari bila hata kufahamu kama wamepigwa...

You are right.

Ist ilianza kuwa nzito na kukosa nguvu kabisa kwenye kamlima kadogo tu au kuovateki.

Fundi wangu kumpelekea akasema hiyo ni cataristi/conveta imeshajaa na kuziba. So engine 'haipumui' vizuri, ndo maana inakosa nguvu kwenye mpando. Solution: kuiondoa. Nikamjibu "go ahead mwanangu, fanya mambo".

Akafungua eksozi, akaingiza kinondo kirefu na kulichokonoa sega lote likatoka (unga hivi).

Akarudishia eksozi. Akafunga. Akanambia tekenya gari twende mlima fulani.

Gari ikawa na nguvu zaidi ya mpya!!! Power to the fullest. Kuovateki ni sekunde sifuri!

It has been a year now down the line mpaka leo mkoko uko na power kama lote!!! Difference ya mlio ni very minimal. Huwezi kunotice labda hadi usogelee eksozi kwa karibu sana.

Hao wanaosema eti kuondoa sega gari inakosa nguvu, wanaongea cha kusikia kwenye vijiwe vya kahawa.

This is on my own real experience. Not kuhadithiwa na wajuaji.
 
Hii kuna fundi aliniambia kuwa wanatoa huo unga wanaenda kuuza na una bei sana ndio nimeanza kuelewa sasa
 

Masega jina la Kitaalamu ni Catalytic converter.

Halafu siyo brevis tu ambayo inaibiwa hiyo kitu.

Kazi yake ni kupunguza exhaust gases zingine ambazo zinatoka na moshi kama Nitrogen Dioxide, Hydrocarbons na kuconvert carbon monoxide kuwa carbon dioxide.
 
Hapa siwezi kukubaliana na wewe, kuna wadau mwanzo wamesema kazi yake kubwa ni kupunguza emission ya gas chafu ili kupunguza uchafuzi wa mazingira. Ndo maana watu wamekua wakitumia magari bila hata kufahamu kama wamepigwa....
Baada ya hayo masega gari huwa inafungwa Oxygen sensor. Unajua kazi yake?

Ulaji wa mafuta lazima uwe affected sababu hiyo ndio sensor inapima content ya Oxygen iliyopo kwenye moshi na signal yake huwa inatumika kuamua ni mafuta kiasi gani yaingine kwenye engine.
 
Duh kwahiyo yakiondolewa hakuna madhara??
 
Mkuu mbona gari zote zinatumia oxygen sensor na ni lazima, usitake kuniambia kwamba oxygen sensor inawekwa kureplace hayo masega.

Naomba tu nikufumbue ufahamu wako, gari yako ikiwa na hayo masega na oxygen sensor ikafa, moshi wake utakaotoka huko sio wa nchi hii.

Mfumo wa engine na combustion lazima uwe na oxygen sensor na kuanzia gari za mwaka 1996 manufacturers walilazimika kutumia secondary oxygen sensor kwa ajili ya ku monitor ufanyaji kazi wa masega. Sasa ukishatoa hayo masega oxygen sensor ina monitor kitu gani kama sio kuibia watu tu.

Tusi ingizwe chaka na mfundi kanjanja jamani

Sent from my Redmi S2 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mbona gari zote zinatumia oxygen sensor na ni lazima, usitake kuniambia kwamba oxygen sensor inawekwa kureplace hayo masega...

Kwa hiyo kazi yake ni kumonitor tu. Aiseeee.


Na mimi ngoja nikuambie hivi. Kwenye live Data za Oxygen sensor kuna fuel trim za kila Oxygen sensor iliyopo kwenye gari lako.

Hizo asilimia za fuel trim ndio zinatell kwamba ni kwa muda kiasi gani injector nozzle inakuwa wazi ili kuruhusu mafuta kuingia kwenye engine na ECU ndio inayocontrol kwamba hizo injectors ziopen kwa muda kiasi gani.

Sasa hata hiyo fuel trim ya sensor ya pili ikiwa nje ya range(mathalani ikiongezeka) gari inakula mafuta vibaya mno. The same thing kinatokea kwa mtu aliyetoa masega.

Halafu unasema eti ukitoa masega Oxygen sensor itakuwa inamonitor nini? Hivi unajua kwamba gari zingine kitendo cha kutoa masega unakuwashia taa ya check engine?

Pia ninapofanya Diagnosis nikiletewa code ya Secondary Oxygen sensor, mawazo mawili ambayo huja kichwani haraka ni ama sensor ina shida au masega yana shida. Na ndio uhalisia sababu hivyo votu vinafanya kazi pamoja.

Halafu unadhani kwanini secondary sensor ikifa gari inatoa sana moshi? Unajua kwanini moshi unatoka mwingi? Then kwanini useme hiyo sensor inamonitor tu na haina kazi nyingine?

Next time siyo kila mtu unayepishana naye mawazo ni kanjanja.
 
Duh kwahiyo yakiondolewa hakuna madhara??

Mkuu, in my own real experience, kwenye ist yangu sikunotice any deficiency in terms of engine power. Power iko vile vile. Utofauti kidogo sana ni muungurumo tu kwenye eksozi gari inapokuwa idle kwenye silence.

Labda kuhusu fuel consumption kuongezeka ndo sina uhakika coz sijawahi kufuatilia hili, mie ni mtu wa maspeed!!

Watu wengi sana wameibiwa hayo masega ila wanaendelea kutumia magari yao pasipo kugundua chochote wala kuhisi.

N.B: Hiyo catalysti conveta ikishajaa/ikishaziba, walai utaiondoa tu ama kureplace. Maana gari inakosa nguvu kabisa kwenye mpando au kuovateki. Utakanyaga accelator hadi mwisho lakini hata mwenye baiskeli atakuacha mlimani.

Wanasema gari ikishazidi umri wa miaka 10, katalysti converter inakuwa inakaribia kuziba/kujaa at any time onwards. Kureplace by using eksozi used ni kuharibu pesa tu coz unapochukua used eksozi unakuwa hujuwi catalyst yake nayo inakaribia kuziba ama bado. Uhakika labda ni kureplace kwa eksozi mpya.
 
Mkuu mbona gari zote zinatumia oxygen sensor na ni lazima, usitake kuniambia kwamba oxygen sensor inawekwa kureplace hayo masega...

Mkuu, unamaanisha kwamba ukishaondoa masega then oxygen sensor inakuwa useless?
 
Kwa hiyo kazi yake ni kumonitor tu. Aiseeee...
Oxygen sensor inayosababisha moshi mwingi ni kwenye mfumo wa fuel pump.

Sio hiyo ya kwenye catalyst convertor. Labda ungeniambia kuna uwezekano wa kupata misfire ningekuelewa.

Wewe umesema masega yakitolewa basi mtu anafungiwa oxygen sensor, naona unahamisha dishi. Unamfungia sensor ya nini wakati zinafanya kazi kwa pamoja na catalyst convertor?

Nipe shule wewe ambae unazijua vizuri hizo oxygen sensor.

Unakuta kunangari ina oxygen sensors hadi 4, je zinatumikaje?

Usikimbilie impact ya kufa oxygen sensor lazima iharibu mfumo wa mafuta au kusababisha moshi mwingi. Kuna nyingine zinawekwa ili kuhakikisha efficiency katika combustion ama exhaust system.

Sent from my Redmi S2 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, unamaanisha kwamba ukishaondoa masega then oxygen sensor inakuwa useless?
Yes

The only impact inayoweza kutokea sababu ile ni sensor ukiitoa itawasha taa ya engine. Na magari yenye mfumo huo ni kuanzia 1996 kuendelea.

Sensor hiyo kazi yake ni kumonitor efficiency ya catalyst converter sasa kama hayo masega yametolewa itafanya kazi gani?

Sent from my Redmi S2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…