Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Yaani kusema ukweli Chadema hamna sera zenye mashiko. Mambo mnayobeza leo ni hayo hayo mliyokuwa mnapigia kelele. Magufuli ametekeleza karibu yote, nakumbuka mwaka 2016 walipoona Magufuli anatekeleza hayo waliyokuwa wanayapigia kelele wakadai eti ameigilizia ilani ya Chadema.

Ziko wapi hoja zenu za ufisadi, rushwa, nchi kutokuwa na ndege, upatikanaji wa maji safi na salama, masoko ya uhakika kwa wakulima n.k.
Leo hoja zenu zimejificha kwenye haki na uhuru wa mwananchi, hoja ambayo kwa mtanzania wa kawaida siyo rahisi kukuelewa.

Wananchi wakawaida hasa waishio vijijini wanahitaji vitu vinavyoonekana Kama barabara, huduma za afya, maji safi na masoko ya bidhaa zao za kilimo. Mtu Kama huyo ukimwambia haki na uhuru sidhani Kama atakuelewa.
 
Hoja za kipumbavu kabisa. Utawala wa ujerumani na waingereza hata ungekuwa wa kimalaika, bado tusingeukubali sababu ni ukoloni, ukoloni ni kitu ambae hakuna anaweza kukikubali, hata iweje.

Marndeleo ya watu yataletwa na vitu, au hamuini jinsi maendeleo ya watu yanavoweza kuletea na umeme wa kutosha na wa bei nafuu toka Rufiji, huo ni mfano mmoja tu.

Hili xenge halina hoja, ni kubwabwaja utumbo tu, linakera sana!
 
Magufuli yuko sahihi, TL kupewa nafasi ya urais kwa sasa is premature. Sina tatizo na TL kiwa rais but anahitaji kujijenga na kujiandaa kwa nafasi hiyo. Sijwahi kupiga kura, but TL akibadilika comes 2025 nikiwa hai naweza kupiga kura kwa mara ya kwanza na nitampa kura yangu TL. Hata hivyo si jambo kuangalia upepo kwa maandalizi ya 2025
Hapo ndo unapofeli mzee....Yaani kama magufuli ameweza kuwa rais kwa miaka hii mitano, basi nchi hii mtu yoyote anaweza kuwa rais hata Mimi na wewe
 
[SUP]Ninachojuwa wengi huwa wanaenda kushangaa tu na kuona wasanii waliokuja hapo. Kwenye kupiga kura hawatakuwa wengi hivyo.[/SUP]
 
Kwani kujaa kwa watu kwenye mkutano ni ishara ya kumpa kura ? Wengine wameenda kushangaa aliyepigwa risasi bado yupo hai? .... Huwajui wasukuma wewe tuulize sisi msukuma anapelekwa pilisi ukimuuliza vipi anakujibu ndoho tabu , yaani hakuna shida ..... Wasukuma wepesi wa kukubali juuu juu ila subiri kwenye vitendo ndio utachoka ngome ya ccm ni kanda ya ziwa subiri october utaamini haya ninayokwambia hata leo nilikuwepo Mwanza yaliyotokea ni ya kawaida sana ni jmati tu kama wa mkutano wa injili wa mwl mwakasege ... october sio mbali utaona
 
Huyu mtu anajuwa mpaka anakera

Nimecheki video ya hotuba yake mpaka nimetamani kulia machozi jamaa ameshangiliwa mwanzo wa hotuba mpaka mwisho kwa muda wa karibia dakika 50

Kweli watu wamechoka na wanataka mabadiliko.
Wanashangilia nini?
 
Tundu Lissu Mwanza;
Viwanja vyote vya ndege vilianzishwa na Waingereza isipokuwa KIA, Songwe na Chato.
Reli inayokuja Mwanza ilijengwa na Waingereza.
Reli ya Tanga hadi Arusha ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya Kati ilijengwa na Wajerumani.
Reli ya TAZARA ilijengwa na Nyerere kwa msaada wa Wachina.

Bandari ya Mwanza ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari ya Kigoma ilianzishwa na Wajerumani.
Bandari zote kubwa za bahari ya hindi zilianzishwa na Wajerumani.

Hata ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na Wajerumani na baadae ikaboreshwa na Waingereza.

Kwanini tuliwakataa Waingereza na Wajerumani?
Ni kwa sababu utawala wao haukuwa wa haki.

Oktoba mwaka 1968 Mwalimu Nyerere alichapisha andiko lake liloitwa Uhuru na Maendeleo.

Mwalimu alisema, Uhuru na Maendeleo ni kama Kuku na Yai. Hupati Kuku bila Yai na hupati Yai bila Kuku. Hupati maendeleo bila Uhuru na hupati Uhuru bila maendeleo. Maendeleo lazima yahusishe watu. Vitu kama barabara, majengo makubwa, reli nk sio maendeleo, bali ni nyenzo za kutuletea maendeleo. Hakuna maana kama tunajenga mabarabara halafu raia wanakamatwa hovyo kwa sababu ya kumuudhi mtu mwenye madaraka.

Lissu akaendelea.
Sikatai kuwa ujenzi wa barabara ni jambo zuri. Sikatai ujenzi wa reli ni jambo zuri.
Lakini utawala wa haki ni muhimu kuliko hayo yote.
------------------------------------------------------------------------------------------------------

Rais wa Marekani, Ronald Reagan aliwahi kusema maneno kama hayo. Akaongeza kuwa Raia wa Marekani ana thamani kubwa kuliko mabarabara ya ghorofa na silaha za Nyuklia. Kwa sababu hayo yote yapo kwa faida ya Raia wa Marekani, na sio kwamba Raia wa Marekani yupo kwa faida ya hivyo vitu.
Theodore Roosevelt naye alisema; haki za Mali na haki za binadamu zinakwenda sawa. Lakini ikitokea haki hizi zinapihana basi haki za binadamu zipewe kipaumbele. Kwa sababu Mali zipo ili zimnufaishe binadamu, sio binadamu azinufaishe mali.

Kwa lugha nyepesi ili mswahili wa kawiada aelewe; ni kwamba, Kujenga miundombinu ya mikubwa huku wananchi wakitegemea mlo mmoja, huku raia wana hofu ya kutoa maoni yao, bado watu wanatekwa, kupotezwa na kuuawa bila uchunguzi, huku miili ya watu inaokotwa halafu serikali inaizika bila uchunguzi...

Asante Mwanza, Asante Tanzania.View attachment 1555631View attachment 1555632
Maneno ya kipuuzi ya kujifariji. Hivyo vyote visingekarabatiwa na awamu ya tano huyo huyo Lissu angesema hawa hawafai kuwepo madarakani kwani wamekubali kila kitu kisifanyiwe ukarabati na matokeo yake kipo vile vile kama kilivyoachwa na wakoloni!!.

Uzuri ni kwamba hao maelfu ya watu ni wenye akili timamu na wenye kupima mchele ni upi na pumba ni zipi.
 
Unahofia MB mbona tupo uchumi wa kati.
Matajiri hawaingii JF. Wote humu kajamba nani ila isikupe presha kijana wa Lissu wa moja hawezi kuwa mbili. Lissu hana hoja anaokoteza tu
Unajifanya kushupaza shingo kumtetea huyo dikteta wako kumbe una njaa Kali kiasi kwamba ku 'view' clip ya sec 5 tano tu unalia na Megabytes.

Inashangaza!
 
Kwahiyo hitimisho kasema atawafanyia nini watu wa Mwanza?
Unataka Rais akufanyie nini ? Au unaona uhuru ni immaterial? Rais hamfanyii mtu kitu watu wanatoa kodi zao ili serikali ifanye kile inachotakiwa kukifanya kutokana na mipango ya nchi...., haya mambo ya mtu kuamua ya kufanya ndio utawala wenyewe huo...
 
Kumjibu kifupi Lisu Ni kuwa Kodi zote na faida za miundo mbinu zilienda kujenga Ulaya sio Tanzania ndio masna tulamkimbiza mkoloni pamoja na kujenga miundo mbinu

Leo faida za miundo mbinu yetu inabaki nchini .Lisu hajui hata historia

Walijenga reli,barabara sawa lakini faida haikubaki nchini!!!

Hotuba yake hopeless

Tulidai Uhuru faida ibaki nchini isiende kujenga ujerumani na uingereza kwa wakoloni
 
Nimeelewa kama tulivyofukuza gonjwa la kibeberu mkabaki kulialia na kupinga ufukuzaji ule
We nae mgumu kuelewa... ndo maana anakwambia kina nyerere waliamua kuunganisha nguvu kumkataa coz hivo ulovitaja vilileta mushkel
 
Maneno ya kipuuzi ya kujifariji. Hivyo vyote visingekarabatiwa na awamu ya tano huyo huyo Lissu angesema hawa hawafai kuwepo madarakani kwani wamekubali kila kitu kisifanyiwe ukarabati na matokeo yake kipo vile vile kama kilivyoachwa na wakoloni!!.

Uzuri ni kwamba hao maelfu ya watu ni wenye akili timamu na wenye kupima mchele ni upi na pumba ni zipi.
kweli uelewa upo tofauti..., visingefanyika kwanini asiseme...
Hivi maendeleo na uhuru na haki ni mutually exclusive... yaani likifanyika moja lingine halifanyiki?
 
Hao wasanii hawapigi kura? kwa nini hawajajitolea kumnadi wenu? ujue uchaguzi huu hakuna msanii anayelipwa na chama, wote wamejitolea kutokana na mapenzi yao kwa JPM.

Maisha yako, wasanii wajitolee kumnadi jiwe, labda kama wametishiwa kutekwa.
 
Kumjibu kifupi Lisu Ni kuwa Kodi zote na faida za miundo mbinu zilienda kujenga Ulaya sio Tanzania ndio masna tulamkimbiza mkoloni pamoja na kujenga miundo mbinu

Leo faida za miundo mbinu yetu inabaki nchini .Lisu hajui hata historia

Walijenga reli,barabara sawa lakini faida haikubaki nchini!!!

Hotuba yake hopeless

Tulidai Uhuru faida ibaki nchini isiende kujenga ujerumani na uingereza kwa wakoloni
Kwa kuongeza waliojenga ni Watanzania tena bure bila malipo stahiki. TL huu ndio mwisho wake hawezi kuwadhihaki Watanzania kiasi hiki. Yeye aende akatulie huko Belgium apumuliwe vizuri kisogoni.
 
Kwani kujaa kwa watu kwenye mkutano ni ishara ya kumpa kura ? Wengine wameenda kushangaa aliyepigwa risasi bado yupo hai? .... Huwajui wasukuma wewe tuulize sisi msukuma anapelekwa pilisi ukimuuliza vipi anakujibu ndoho tabu , yaani hakuna shida ..... Wasukuma wepesi wa kukubali juuu juu ila subiri kwenye vitendo ndio utachoka ngome ya ccm ni kanda ya ziwa subiri october utaamini haya ninayokwambia hata leo nilikuwepo Mwanza yaliyotokea ni ya kawaida sana ni jmati tu kama wa mkutano wa injili wa mwl mwakasege ... october sio mbali utaona

Kwa tume hii isiyo huru ya uchaguzi, unawezaje kutishia wanaume hiyo October?
 
Back
Top Bottom