britanicca
JF-Expert Member
- May 20, 2015
- 16,295
- 33,994
HakikaTulikubaliana tupo awamu inayotenda haki. Tusihangaike ku-influence kwa namna iwayo yote uamuzi wa mahakama. Tuwaachie mawakili na wanasheria wafanye kazi zao.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HakikaTulikubaliana tupo awamu inayotenda haki. Tusihangaike ku-influence kwa namna iwayo yote uamuzi wa mahakama. Tuwaachie mawakili na wanasheria wafanye kazi zao.
Hii nchi ina watawala wa hovyo hatujawahi kupata. Nimemsikiliza spika yaani hadi nimeona aibu .Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Wahuni/wachawi.Bunge la Mchongo + Spika wa Mchongo = Kikundi cha ..........
Mkuu mle bungeni..tuna maspika galasa ambayo yaako very biased..badala ya kusimamia sheria yanasimamiia matumbo bila kujali mstakabali wa Nchi juu ya mukdha tuliojiwekea.Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Umesahau ya Zitto, mbona aliendelea kuw mbunge, ?Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.
Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.
Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.
Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.
Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.
- Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
- Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
- Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
- Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.
Majibu ya wakili wa Halima Mdee na wenzake 18
- Wamesema hawajataja dini lakini kiapo kinajieleza
- Wahusika wanaoombewa amri wametajwa kwenye Viapo
- Wamekubali baada ya kuelekezwa na Mahakama kwamba inaongeza jambo jipya
- Kuhusu kumuunganisha Speaker au Katibu wa Bunge, amri zilizoombwa zimeombwa na wahusika ambao wapo kwenye Maombi yaani Chadema, NEC (tume ya Uchaguzi) na Mwanasheria Mkuu
- Kuhusu kwamba NEC ina ulinzi wa Katiba chini ya ibara ya 74(12), hakuna sehemu ambayo wao wameombwa kuchunguza NEC
- Kuhusu kwamba hakuna hatari yoyote inayopelekea kutolewa kwa amri iliyoonyeshwa na waleta maombi, wamesema hii ni amri ya upande mmoja na kwenye hayo maombi ya amri hiyo; wameomba kwamba wasitolewe kama wabunge wa viti maalum Kwamba wadaiwa wanajua kwamba watatolewa kuwa Wabunge.
Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu
Subirini aibu nyingine kwa Serikali
Tulieni mnyooshwa, yaanii mtajutaWataumbuka japo watabebwa.
Hii serikali ina penda mambo ya aibu sana.. Na mwanasheria mkuu badala ya kushauri ana tuma mawakili mahakamani kuendeleza aibu.Wataumbuka japo watabebwa.
Hayo mtayajua nyieHawataendelea kuwa wananchama wa CHADEMA isipokuwa wa CCM
Siasa tamu pale unapojua madhaifu ya mpinzani wakoHawataendelea kuwa wananchama wa CHADEMA isipokuwa wa CCM
Kweli tupuSiasa tamu pale unapojua madhaifu ya mpinzani wako
Hao mawakili 8 wa serikali wameungana na mawakili watatu wa kina Mdee kuiomba mahakama iweke zuio ili wateja wao wasiondolewe bungeni.Hao watakuwa wanamuelekeza hakimu cha kufanya kulingana na mtiririko wa kesi.
Hii nchi ina watawala wa hovyo hatujawahi kupata. Nimemsikiliza spika yaani hadi nimeona aibu .
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app