Yaliyojiri kesi ya Wabunge 19 waliovuliwa uanachama Vs CHADEMA. Mahakama yaridhia Ubunge wao uendelee wakati kesi ikiendelea
Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Hii nchi ina watawala wa hovyo hatujawahi kupata. Nimemsikiliza spika yaani hadi nimeona aibu .

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Mkuu mle bungeni..tuna maspika galasa ambayo yaako very biased..badala ya kusimamia sheria yanasimamiia matumbo bila kujali mstakabali wa Nchi juu ya mukdha tuliojiwekea.
 
Lema Alivuliwa Ubunge Na Mahakama, Alikata Rufaa Lakini Alifukuzwa Bungeni, Spika Hakusubiri Rufaa Yake Isikilizwe, Wabunge 9 wa CUF Walifukuzwa Uanachama. Walienda Mahakamani Lakini Walitolewa Bungeni, Spika Hakusubiri Kesi Yao Isikilizwe, Je Kwa Kina Halima Sheria Imebadilika?
Umesahau ya Zitto, mbona aliendelea kuw mbunge, ?
 
Wakili Peter Kibatala na Wakili John Malya tayari wapo ndani ya Chumba Cha Mahakama Mbele ya Jaji Mgeta.

Jopo la mawakili wa Chadema lina mawakili wanne Adv. Kibatala Adv. Mtobesya Adv. J. Mndeme Adv. j. Malya Wengine. Kesi namba 16 ya Mwaka 2022, Mdee na Wenzake 18, ilifunguliwa Mahakama Kuu Mbele ya Jaji Mgeta.

Mdee na wenzake 18 Wanawakilishwa na Mawakili Adv Ikupilika Panya, Adv Edson Kilatu na Adv Aliko Mwamanenge. Baadae likaingia Jopo la Mawakili wa Serikali wapo Wanne Wakiongozwa na Wakili Gabriel Mallata.

Mawakili wa Mdee na wenzake wametoa ombi la Mahakama Iweke zuio "Court Injunction"Wasivuliwe Ubunge na Bunge. Wanaomba Kwanza Mahakama itoe zuio la Mdee na wenzake waendelee Kuwa wabunge mpaka pale ambapo Kesi ya msingi Kesi itakapoisha. Baada Wasilisho lao, Mahakama italazimika Kusikiliza Ombi hilo Kwanza kutoka pande zote.

Amesimama wakili Peter Kibatala anachambua kwanza Viapo vyao ambavyo vimesainiwa na Mawakili wao na Wateja (Wakina Mdee)
  1. Viapo havionyeshi waapaji (Wakina Mdee) Wameapa wapi.
  2. Waapaji hawajataja Dini zao katika Viapo vyote
  3. Ombi lao la kubaki na ubunge halijaelekezwa kwa yoyote kati ya wadaiwa (Mdee na wenzake)
  4. Katika maombi yao hawasemi kama wanataka kuendelea kuwa wanachama wa Chadema ila wanataka kuendelea na ubunge tu.
Mawakili wa CHADEMA wanaendelea Kuchambua Viapo na Kutaja Mahitaji ya Kisheria na sifa zinazohitajika katika Viapo wakiwa na Lengo Kuweka Zuio la awali, preliminary Objection (P.O) Mahakama isikubali Kupokea Maombi yao ya kesi.

Mawakili wa Halima Mdee na wenzake kwa pamoja na Mawakili wa Serikali Wanafanya (Re-joinder) Wanasimama kujibu hoja za Jopo la Mawakili wa Chadema Kuhusu hitilafu katika Viapo na Mapungufu yake katika ufunguaji wa Kesi.

Majibu ya wakili wa Halima Mdee na wenzake 18
  1. Wamesema hawajataja dini lakini kiapo kinajieleza
  2. Wahusika wanaoombewa amri wametajwa kwenye Viapo
  3. Wamekubali baada ya kuelekezwa na Mahakama kwamba inaongeza jambo jipya
  4. Kuhusu kumuunganisha Speaker au Katibu wa Bunge, amri zilizoombwa zimeombwa na wahusika ambao wapo kwenye Maombi yaani Chadema, NEC (tume ya Uchaguzi) na Mwanasheria Mkuu
  5. Kuhusu kwamba NEC ina ulinzi wa Katiba chini ya ibara ya 74(12), hakuna sehemu ambayo wao wameombwa kuchunguza NEC
  6. Kuhusu kwamba hakuna hatari yoyote inayopelekea kutolewa kwa amri iliyoonyeshwa na waleta maombi, wamesema hii ni amri ya upande mmoja na kwenye hayo maombi ya amri hiyo; wameomba kwamba wasitolewe kama wabunge wa viti maalum Kwamba wadaiwa wanajua kwamba watatolewa kuwa Wabunge.

Pia, soma=> Wabunge 19 viti maalum CHADEMA wafungua kesi. Bunge lasema linasubiri uamuzi wa Mahakama kuu

Moto unwaki
 
Hao ni mawazili na manaibu wake huko badae
 
Hii nchi ina watawala wa hovyo hatujawahi kupata. Nimemsikiliza spika yaani hadi nimeona aibu .

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

Ni kinyaa kitupu ukisikiliza anachosema. Huwa najiuliza imekuwaje tunaongozwa na watu wajinga wa kiwango hiki. Cha ajabu watu wanaofanya haya wanajiita ni wasomi!

Nilichogundua baada ya ccm kupoteza ushawishi kwa umma na kuamua kutumia vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti, kumetokea ukiukwaji mkubwa wa sheria, na hali inazidi kuwa mbaya labda CDM ifutwe au wakubali kutawaliwa na ccm kwa mabavu. Na tabia hii ya ukiukwaji mkubwa wa sheria itachukua muda mrefu hadi hali halisi kujirudia.
 
Back
Top Bottom