Una grievances zako binafsi nadhani na Tundu Lissu....
Hujaona kitu kimoja katika hii "very well directed movie" wanayofanya CHADEMA ambayo mimi na naamini na wengine wameona....
Nimemsikiliza Nyalandu Lazaro mwanzo mwisho. Nikamsikiliza Dr MayRose Majinge naye mwanzo mwisho na mwisho nikamtazama na kumsikiliza Tundu Lissu mwanzo mwisho...
Kwa hakika kabisa, TUNDU LISSU ameshapita hata kabla ya kura kupigwa. Hii kitu ndivyo ilivyokuwa planned...
Hotuba yake tu inaeleza na kuthibitisha kila kitu hata namna ilivyopokelewa na kuamusha hisia za wajumbe....
Ni hotuba ambayo si ya kunyenyekea kuomba kura kwa wajumbe. Ni hotuba iliyobeba "authority" ndani yake kama vile tayari keshathibitishwa kuwa mgombea rasmi ili hali yuko kwenye mchujo...
Na ni hotuba ambayo moja kwa moja ikishambulia SERA na UTAWALA wa CCM chini ya Bwana John Pombe Magufuli. Ni picha inayoonesha kuwa Bw. Nyalandu na Dr MayRose ni wasindikizaji tu....!!
Nyalandu ni mtu mzuri na anaweza kuwa Rais. Lakini ktk uchaguzi wa mwaka huu 2020 hafai, hatawez. Huyu hawezi purukushani za kupambana na CCM. Ni kwa sababu CCM wenyewe wana mgombea mtukutu na mpenda Shari...
Huyu anapaswa kupambanishwa na mtu wa aina ya Tundu Lissu. Wagombea legelege wasiojiamini hawawezi kupambana na CCM hii na mgombea wao. Tundu kaonja mauti. Haogopi lolote. Huyu anafaa. Ni jasiri sana. Ana uelewa sana wa mambo mengi....!
Hii ndiyo tofauti ya wagombea hawa watatu....
Kwako wewe huyu bwana TL siyo "presidential material". Ni sawa na haki yako kabisa kumtazama na kum - describe kwa jinsi hiyo japo hujatoa sababu zote kuunga mkono hoja yako hiyo....
Lakini watoto wa mjini wanasema " .....usiyempenda kaja, yuko hapo anabisha hodi mlangoni mwako..."