Mahakama Kuu, masijala kuu ya Dar es Salaam, imetoa ruhusa kufunguliwa kwa kesi ya jinai dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Joseph Luambano ametoa ruhusa hiyo kwa maandishi leo kujibu hoja ya aliyekua Mbunge wa Ubungo, Saeed Kubenea.
Awali, Kubenea alifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni lakini ikaondolewa kutokana na mapungufu kadhaa ya kisheria. Mahakama kuu ilitakiwa kutoa mwongozo ikiwa mtu binafsi anaweza kufungua kesi ya jinai dhidi ya Makonda. Kufuatia maamuzi hayo ya mahakama kuu sasa Kubenea amepewa haki ya kufungua shauri la kesi ya jinai dhidi ya Makonda.
Makonda anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kukiuka haki za binadamu, matumizi mabaya ya madaraka, na kuvamia kituo cha habari cha Clouds. Pia anatuhumiwa kwa kudhulumu haki ya kuishi ya watu mbalimbali, madai ambayo yalitolewa na serikali ya Marekani, na kumuweka katika orodha ya watu wasioruhusiwa kuingia nchini humo.
Malisa GJ