Una akili sana mkuuKaria kuwa baba mlezi
kuendekeza ushabiki Kwa Simba ujue utapendwa na Wana Simba na utachukiwa na Wana Yanga.
Mpaka Sasa karia ,TFF ,bodi ya ligi na kamati ya masaa 72 imeshindwa kuendesha Mpira wa Tz kwa kufuata kanuni na sheria mlizojitingia wenyewe ,mmekuwa mkiendesha Mpira kwa kuongozwa na mihemko .Hata kiongozi wa bodi ya ligi amekiri wazi kushindwa kutumia kanuni na akaomba hekima na busara zitamalaki zaidi.
Pia Kuna baadhi ya vigogo wa nchi wanatumia madaraka yao vibaya wanasahau wao ni viongozi wakubwa sana wanategemewa na wananchi wote sio kundi la wanachama wa klabu Fulani ya Mpira wa miguu wanayoshabikia Kwa leisure wanayopata kwa madaraka wanayoshikilia iliwatosha wao kuwa wasuluhishi migogoro ya mpira yanapojitokeza badala ya kushangilia timu hizi za Yanga na Simba zinapoonyeshana ubabe.
Kama kweli Karia ataipa ushindi Simba point 3 na kuipa Simba ubingwa wa ligi na kuinyang'anya Yanga point 15 ,Karia atapandikiza chuki kwenye tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu zinazoweza kuzalisha fujo michezoni inayoweza kukimbiza wadhamini ambao imetumika jitihada kubwa kuwapata na wadhamini wakijitoa ligi yetu itakosa mvuto na tutarudi kule kule kwa timu kushindwa kumudu gharama za kuendesha timu zao kwenye mechi za ligi hata za mashindano ya Africa.
Itasaidia Nini kama ikabaki Simba peke yake anakuwa bingwa na peke yake ndiye awakilishe nchi kwenye mashindano ya Afrika hapo tutakuwa tunaenda mbele au tunarudi nyuma.
Karia na TFF yake wasitumie ubabe katika kuongea na Yanga katika suala hili la mechi ya Derby ,Karia kubali kuwa mpole tumia busara kupunguza jazba za Yanga maana ukweli hakuna udhibitisho kuwa Yanga alihusika kuwazuia Simba wasifanye mazoezi maana police walikuwepo hakuna aliyekamatwa kwa kuwafanyia simba fujo kusema tu mabaunsa wa Yanga waliwazuia simba he mabaunsa wanatambulika na TFF katika uongozi wa Yanga mbona Police wamekataa hakukukuwa na fujo yoyote Wala hakukuwa na tishio lolote la usalama ila kinachojulikana wazi Simba aliogopa kupeleka timu uwanjani baada ya wachezaji wake nyota 3 Camara,chemalone na kagoma kuwa majeruhi.
Simba sasa ipo tayari kucheza Debi sababu wachezaji wao wote wamepona Yanga Sasa wanagoma kucheza wanaona wataonekana wanabuluzwa na Simba na TFF hivyo.
Kinachotakiwa kauli za kubezana zinyamizishwe timu zishauriwe vizuri TU zicheze kwa maendeleo mapana ya soka letu.
Hizo ni aibu tu ndizo zinazowasumbua viongozi na nyie Mashabiki. Hizi taarabu mnazoimba hazitawasaidia.Kama Karia na TFF yake wana huo ubavu wapange tarehe ya mchezo, waikate Yanga points na waishushe daraja
Hata CAS hatuna imani nao ndo maama msimu huu tumejitoa mashindano ya kimataifa.Kwakuwa mamlaka zinazo simamia kabumbu la Tanganyika zinatenda dhulma na hamziamini mimi nashauri MUACHE KUSHIRIKI MASHINDANO YA AINA YOYOTE YANAYOSIMAMIWA NA HIZO MAMLAKA.
Ujinga ni hali ya kutokuwa na maarifa au ufahamu wa jambo fulani.Hizo viashiria wamezisema wapi mkuu?
Mwisho unajisikiaje kutaja neno ujinga pale unapojenga hoja yako?
Wapenda michezo wasiyofungamana na upande kilio chao kikubwa ipo kwenye haya ya mwisho kwenye hoja yako.Ujinga ni hali ya kutokuwa na maarifa au ufahamu wa jambo fulani.
Kwa maana nyingine, ujinga ni neno linaloweza kuelezea upungufu wa taarifa au uelewa katika eneo fulani bila kuashiria ukosefu wa akili au uwezo wa kufikiri.
Viashiria vimesemwa kupitia mmoja wa Afisa wa bodi ya ligi lakini hata kwenye taarifa ya Bodi ya ligi ilitaja kuwa kuna matukio ambayo yalihitaji uchunguzi ambao ungeweza kuchukua muda.
So walau mngeipa lawama Bodi ya ligi kwa kusema itatoa ratiba ya mechi haraka iwezekanavyo ilihali haijatoa majibu ya uchunguzi wa hivyo viashiria.
Sasa Yanga wao hawalalamikii hilo.Wapenda michezo wasiyofungamana na upande kilio chao kikubwa ipo kwenye haya ya mwisho kwenye hoja yako.
Lazima bodi itoe taarifa ya uchunguzi wao kuhusiana na sababu za kuhairisha mchezo kabla ya kupanga tarehe nyingine tofauti na hapo wanakosa uhaminifu tena.
Nafikiri bodi ya ligi wakitoa majibu ya uchunguzi kuhusiana na sababu ya kuhairishwa kwa mechi hakuna anayeweza kukataa mechi kuchezwa tena.Sasa Yanga wao hawalalamikii hilo.
Kulalamikia hilo ni kukubali kuwa mchezo upo ila kwanza mtupe mrejesho wa huo uchunguzi.
Kulalamikia hilo ni kukubali kuwa TFF na Bodi ya ligi ipo sahihi kuahirisha mechi kupitia kanuni ambazo zinaipa nguvu ya kuwa na hayo mamlaka.
Lakini Yanga hawahitaji majibu ya uchunguzi ili wacheze mechi kwasababu msimamo wao tangu awali umeegemea kwenye maamuzi ya Bodi ya ligi ya kuahirisha mechi.
Sehemu pekee ambayo TFF na Bodi ya ligi watawapa Yanga hoja ya kueleweka ni kama ratiba ya mechi itatangulia kabla ya majibu ya huo uchunguzi.
Yanga ataendelea na msimamo wake ule ule wa Hatuchezi.Nafikiri bodi ya ligi wakitoa majibu ya uchunguzi kuhusiana na sababu ya kuhairishwa kwa mechi hakuna anayeweza kukataa mechi kuchezwa tena.
Kwa wapenda michezo ilikuwa ni busara kuwaombq watoe uchunguzi wao ya kwanini mechi ilihairishwa siyo mashabiki including wewe kusema kuwa wapange tarehe ya mechi nyie mtaleta timu uwanjani, hii ni sehemu ya kuhalalisha bodi kuhairisha mechi bika kutoa taarifa ya sababu.
Tuweni wanamichezo siyo ushabiki hadi penye kuhoji uhalali wa kanuni kutotumika ipasavyo. Leo ipo kwa Yanga na Simba ila kesho hatujui itakuwa na timu zipi.
Yaani mashabiki wamekuwa vipofu hawaoni kabisa hasara waliyopata mashabiki wa mpira waliopoteza muda na pesa kuja hadi Dar kuangalia mpira alafu inahairishwa then wanataka tarehe ipangwe tu bila kuhoji sababu za kuhairishwa awali wala hawajiulizi kama haiwezi kuhairishwa tena kama awali.
Tusipodhibiti haya mambo ya uwazi kwenye michezo yetu itatusumbua sana.Yanga ataendelea na msimamo wake ule ule wa Hatuchezi.
Unajua kwanini?
Kwasababu hata ilipotola taaria ya kuahirisha mechi, taarifa iliyotaja na sababu ambazo zinahitaji uchunguzi.
Yanga hawakutaka kusubiri walichokifanya ni kuiandikia barua TFF na Bodi ya ligi iwape pointi 3 na magoli 3.
Kwa hiyo hilo unaloliwaza kuwa litakuwa ni hitaji la Yanga ili wacheze mechi, haliwezi kuwa jibu la kuwaridhisha kuwafanya wacheze mechi.