Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

Duu! Sasa imekuwa kama CCM na CDM. Wacha tuone mwaka huu utakavyoisha
 
Uhuni wa TFF utapingwa Kwa njia zozote Sasa hao TFF kama wana uweZo waisushe Yanga daraja

Karia afurahie awe na amani akiisusha Yanga daraja

TFF ina upande kwenye hii kesi yaani ni sawa kupeleka kesi Kwa hakimu amfunge mwanae wa pekee

Bodi ya ligi na TFF walisema sababu za kuhairisha mechi ni uvunjifu wa usalama ambapo watu wenye taaluma za usalama police walikanusha kuwa tarehe 8 March hapakuwa na uvunjifu wa amani

Kuhusu Rushwa, TAKUKURU walikanusha kutambua rushwa yoyote kwenye huo mchezo

TFF wameinyonga Yanga na Karia alionesha kuiunga bodi ya ligi na Simba mkono

TFF waligomea kusikiliza kesi na kuichelewesha maksudi ili kukwamisha Yanga kupata haki Yao ili siku 21 zipite na Yanga asipate haki yake, huu ni uhuni wa wazi wa TFF

Kuna tetesi TFF Kwa mkono wao walijipenyeza CAS na kuishawishi iikandamize Yanga

Sasa TFF kama wanaweza wakaishushe Yanga daraja au waikate points 15 tuone

Huu ni muda wa Yanga kuonyesha ukubwa wake
==

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS] kuhusu kesi yetu namba CAS 2025/Α/11298.

CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa.

Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Uongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhulma.

Aidha, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuujulisha Umma kuwa, msimamo wa Klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko palepale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.

Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
View attachment 3325134
Na wasishiriki kima hao....waache vitisho
 
Lakini Ndugu hebu tujadili kidogo?

Yanga hataki kucheza mechi yake na Simba kisa ni Uonevu wa TFF na bodi ya Ligi si ndio? Je uonevu huo ni wa ndani ya uwanja au nje ya uwanja?
Nawasubiri waje na majibu hapa
 
😂😂🤣🤣 Uko sahihi sana Kiongozi. Sasa wenye akili mmefika 3.
Hapana kiurahis tuu hvyo wafke 3 mpaka anaewafanyia uchunguzi wa kitabibu. kubwa la maadui zunguporii aseme maana mwanzo uchunguzi alifannya yeye na akathibitishaa kapata wawili tuu.au wewe ni haji kama we haji basi nakukubalia wamefka3 😂😂
 
Mkuu
Mbereko Fc tarehe 8 mliitumia Bodi yenu hiyo hiyo kukimbia mechi! Halafu leo mnataka tena Bodi yenu hiyo hiyo ipange mechi! Kisa golikipa wenu Mousa Camara amepona majeraha yake!!

Yaani huku kudekezwa sasa imekuwa ni too much! Mkija uwanjani na timu yenu ya tia maji tia maji, tayari Kamati ya waamuzi nayo inakuew imeshawaandalia waamuzi wenu special wa kuchezesha mechi zenu tu! Tatu Malogo, Kepha Kayombo, na Japhet Smart! Na wakichezesha tu mechi zenu; lazima ushindi upatikane kwa namna yoyote ile.
Mkuu umesha sikia shabiki wasimba akiomba tarehe ya mechi au kuzungumziia habari ya mechi na yanga
 
🤣🤣🤣.wanaona AIBU
sasa tuone kama gsm atakubali kupata hasara.
maana hakuna kombe litakalotoka wala zawadi ya mshindi
Akili zako zinakwambia GSM anasubiri faida siku yanga wakiwa mabingwa?
 
karia wewe waache tu.mbo
Akili zako zinakwambia GSM anasubiri faida siku yanga wakiwa mabingwa?
🤣🤣🤣🤣.kwa hyo Gsm ana kisima cha hela cha kuigharamikia yanga?
 
Siasa ya CCM ndio imefikisha hapa michezo.
Nikikumbuka enzi zile nipo kijana na wakina Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Suleiman Nyambui, walivyokuwa wanaipaisha Tanzania, leo hii Simbu anapambana hata Ikulu haimuoni zaidi ya kuona Simba na Yanga tuu, napata sababu ya kuendelea kupambana CCM ife ili nchi ipige hatua kwenye kila nyanja na kila sekta.
 
Mtakula mlipopeleka mboga. Msomali ana kesi fifa...unawezaje timu Moja kudhamini timu 8 za ligi kuu...hii ndio ubaya ubwela..tuheshimiane kuanzia Sasa. Mtaieleza Dunia kwanini mliinyima timu mnayocheza nayo kutofanya mazoezi uwanja tajwa kama kanuni na Sheria zinavyoelekeza,, na pia mtaiambia Dunia kwanini timu yenu inadhamin timu nane za ligi kuu ambayo inatoa mwanya mkubwa wa upangaji wa matokeo..
Alivunja sheria zipi za TFF na kwa nini TFF walimpa huo udhamini?
 
Game itachezwa tu, sisemi kwasababu nafurahi kilichotokea siku iliyopangwa game au naichukua Yanga--hapana.

Viongozi wanazuga tu ionekana walikazani mzuri kwa mashabiki zao. Ila raisi akisema chezeni tarehe fulani na mimi nitawawekea mzigo kwa mshindi wa Derby. Itaitwa Derby ya samia.

Kuna vitu unaona kabisa haviwezi tokea bongo, hasahasa kwa hizo team mbili.
 
Hapa timu yangu Yanga wamezingua kabisa. Peleka timu tuwanyoe hao, soka litaongea.
 
Uhuni wa TFF utapingwa Kwa njia zozote Sasa hao TFF kama wana uweZo waisushe Yanga daraja

Karia afurahie awe na amani akiisusha Yanga daraja

TFF ina upande kwenye hii kesi yaani ni sawa kupeleka kesi Kwa hakimu amfunge mwanae wa pekee

Bodi ya ligi na TFF walisema sababu za kuhairisha mechi ni uvunjifu wa usalama ambapo watu wenye taaluma za usalama police walikanusha kuwa tarehe 8 March hapakuwa na uvunjifu wa amani

Kuhusu Rushwa, TAKUKURU walikanusha kutambua rushwa yoyote kwenye huo mchezo

TFF wameinyonga Yanga na Karia alionesha kuiunga bodi ya ligi na Simba mkono

TFF waligomea kusikiliza kesi na kuichelewesha maksudi ili kukwamisha Yanga kupata haki Yao ili siku 21 zipite na Yanga asipate haki yake, huu ni uhuni wa wazi wa TFF

Kuna tetesi TFF Kwa mkono wao walijipenyeza CAS na kuishawishi iikandamize Yanga

Sasa TFF kama wanaweza wakaishushe Yanga daraja au waikate points 15 tuone

Huu ni muda wa Yanga kuonyesha ukubwa wake
==

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS] kuhusu kesi yetu namba CAS 2025/Α/11298.

CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa.

Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Uongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhulma.

Aidha, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuujulisha Umma kuwa, msimamo wa Klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko palepale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.

Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
View attachment 3325134
Uto..chalii.jpg
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom