Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

Yanga yatoa msimamo: Yaitupilia mbali CAS, Yagoma kurejea kamati za ndani, Yasema haitacheza mechi ya derby

Simba atopeteza point hapo katikati yanga atamuacha zaidi ya point 4 hivo kufanya derby kua pointless!!! Hio siku yanga wapeleke hata yanga queens tu
 
Simba atopeteza point hapo katikati yanga atamuacha zaidi ya point 4 hivo kufanya derby kua pointless!!! Hio siku yanga wapeleke hata yanga queens tu
Yanga wenyewe hili hawana uhakika nalo ndo maana wanagoma goma--- ila mpira ni 90

So lolote linatokea🤣
 
Mtakula mlipopeleka mboga. Msomali ana kesi fifa...unawezaje timu Moja kudhamini timu 8 za ligi kuu...hii ndio ubaya ubwela..tuheshimiane kuanzia Sasa. Mtaieleza Dunia kwanini mliinyima timu mnayocheza nayo kutofanya mazoezi uwanja tajwa kama kanuni na Sheria zinavyoelekeza,, na pia mtaiambia Dunia kwanini timu yenu inadhamin timu nane za ligi kuu ambayo inatoa mwanya mkubwa wa upangaji wa matokeo..
TFF na washirika wake huo ujasili hawana wathubutu uone

Sent from my 23021RAAEG using JamiiForums mobile app
 
Uhuni wa TFF utapingwa Kwa njia zozote Sasa hao TFF kama wana uweZo waisushe Yanga daraja

Karia afurahie awe na amani akiisusha Yanga daraja

TFF ina upande kwenye hii kesi yaani ni sawa kupeleka kesi Kwa hakimu amfunge mwanae wa pekee

Bodi ya ligi na TFF walisema sababu za kuhairisha mechi ni uvunjifu wa usalama ambapo watu wenye taaluma za usalama police walikanusha kuwa tarehe 8 March hapakuwa na uvunjifu wa amani

Kuhusu Rushwa, TAKUKURU walikanusha kutambua rushwa yoyote kwenye huo mchezo

TFF wameinyonga Yanga na Karia alionesha kuiunga bodi ya ligi na Simba mkono

TFF waligomea kusikiliza kesi na kuichelewesha maksudi ili kukwamisha Yanga kupata haki Yao ili siku 21 zipite na Yanga asipate haki yake, huu ni uhuni wa wazi wa TFF

Kuna tetesi TFF Kwa mkono wao walijipenyeza CAS na kuishawishi iikandamize Yanga

Sasa TFF kama wanaweza wakaishushe Yanga daraja au waikate points 15 tuone

Huu ni muda wa Yanga kuonyesha ukubwa wake
==

Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutaarifu Umma kuwa umepokea majibu kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS] kuhusu kesi yetu namba CAS 2025/Α/11298.

CAS imeielekeza Young Africans Sports Club kurudi kwanza kwenye Kamati za ndani za Soka ili kushughulikia kesi yetu kabla ya kurudi kwao kwa ajili ya hatua za rufaa.

Lakini kutokana na uonevu, uvunjwaji mkubwa wa kanuni na upendeleo wa dhahiri kwa baadhi ya timu unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka Tanzania, Uongozi wa Young Africans Sports Club hauna imani na hauko tayari kupeleka shauri hilo kwenye Mamlaka ambazo zinatenda dhulma.

Aidha, Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuujulisha Umma kuwa, msimamo wa Klabu yetu juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu Msimu huu uko palepale kuwa hatutashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.

Wanayanga wote, watakuwa tayari kuipambania haki yao kivyovyote vile ili kukomesha dhulma na uvunjwaji mkubwa wa kikanuni unaoendelea kufanywa na Mamlaka za soka kwa maslahi mapana ya maendeleo ya soka nchini.
View attachment 3325134
Wamekurupuka kama walivyokurupuka kwenda CAS, hii itakula kwao na italeta vurugu kubwa hapo Jangwani. Hersi ana utoto mwingi sana.
 
View attachment 3325186

My Take 1
Yanga kazeni hivyo hivyo

My Take 2
Bodi panga tarehe fuata taratibu zote sisi tutakuja uwanjani tupate point za buuuuuure kabisa
Mbereko Fc tarehe 8 mliitumia Bodi yenu hiyo hiyo kukimbia mechi! Halafu leo mnataka tena Bodi yenu hiyo hiyo ipange mechi! Kisa golikipa wenu Mousa Camara amepona majeraha yake!!

Yaani huku kudekezwa sasa imekuwa ni too much! Mkija uwanjani na timu yenu ya tia maji tia maji, tayari Kamati ya waamuzi nayo inakuew imeshawaandalia waamuzi wenu special wa kuchezesha mechi zenu tu! Tatu Malogo, Kepha Kayombo, na Japhet Smart! Na wakichezesha tu mechi zenu; lazima ushindi upatikane kwa namna yoyote ile.
 
Yaani hili sakata la Derby, Simba ilitoa taarifa moja tena paragraph tatu ikatulia, Yanga sijui barua ya 46 hii juu ya hili sakata😂😂
 
Back
Top Bottom