Yawezekana hali halisi ndani ya Israel ni mbaya kuliko….

Na yule chief Negotiator bwana Ali Shamkhani ambae Israel ilidai aliuawa na mabomu, yupo hai na aendelea uzuri na matibabu chini ya ulinzi mkali.

Huyu ni mmoja wa wataalam wa hali ya juu na ni lazima kwa sasa yupo kwenye hit list ya Israel.
 
Mimi kwakweli bado Iran hawajaniridhisha kabisaaaa
Yaani mtu anaingia nchini kwako kwa kukuvizia na kushtukiza na anaua karibu top level yote ya jeshi pamoja na wanasayansi muhimu kabisa wa kinyulkilia

Nilitegemea Iran itaigeuza Israel kama Gaza
Yaani ilikua ni kumwaga missiles pale kama nvua hadi hao wanaojiita taifa teule wapitie exactly walichopitia wana Gaza

Sitamani kabisa hii vita iishe
Natamani kuiona Irana ikitwanga kabisa kabisa pale Israel mpaka akili ziwakae sawa sawa
Hapo ndio wataheshimiana
 
Hapana, mkuu vita si nzuri na usiombe vita ya kutupiana makombora ya balistic na mashambulizi ya angani na F-35s.

Iran walikuwa "naive" (walijiamini kupita kiasi) baada ya kudanganywa na Trump kwamba waendeleee na mazungumzo bila kung'amua kuwa ule ulikuwa ni mtego au trap kwamba wachukulie kila kila Ok na wale target wote waendelee na maisha wakti wako vitani, ndo maana kazi ikawa rahisi kwa Israel kwa kutumia tracking software kwenye simu zao.

Musrael humpati kwenye teknolojia na kuanzia zile pagers hadi mtandao wa WhatsApp target zao walikuwa nazo sambamba.

Pili, ni mbinu ya "infiltration" kupenyeza majasusi na wale raia wa Iran (insiders) ambao wamefanikisha kuua ADS za Iran kwanza kabla ya mambo mengine, hivyo Iran kuja kugundua ADS zimepatwa, kukawa hakuna jinsi isipokuwa kufanya plan B ambayo imechukua muda lakini waliweza kuanza kurusha makombora mengine.

Muundo wa jeshi la Iran ni tofauti kidogo kwani kuna jeshi na kisha kuna jeshi la ukombozi IRGS ambalo baadae ndilo lilochukua kazi.

Hivyo wamekubali kuwe na ceasefire na sie wengine kuunga mkono ceasefire kwa mstakabali za amani ya mashariki ya kati.
 
Stress na frustrations tu za vin'gora na kwenda kwenye shelters tena halafu baada ya DK 10 mnaambiwa ni decoys au intercepted mrudi muendelee na shughuli zenu baada ya DK kadhaa tena mnatakiwa mrudi kwenye shelters tena.
 
Nakubaliana na wewe, Iran pamoja nakukaa kwenye vikwazo zaidi ya miaka 30 lakini bado ameweza kuwa strong na kusimama na superpowers.

Nafikiri labda ndio maana hawa watu hawataki wale jamaa akina Ayatollah na watu wake waongoze Ile nchi, inaonekana jamaa akili zinafanya kazi, wakiachwa wanaweza kuwa hatari sana siajabu wakawa mojawapo ya superpower.
 
Ile sauti inatisha sana mkuu ni kama starring yuko peke yake msituni halafu kamera inahamishiwa kwingine unaona msafara wa maadui wa kutosha na kale ka sauti wanakuuujaaaaa.
 
Wewe uko Igalula unaongea mambo ya Israel..!!!

Uharibifu mkubwa uliofanywa Iran hauwezi kuonekana kwa sababu vyombo vya habari vya kigeni hiviko Iran lkn uharibifu ni mkubwa sana kwenye kambi za kijeshi na maeneo mengine nyeti.

Israel wameepuka sana kushambulia makazi ya watu tofauti na Iran.
 
 
Israel imeipiga marufuku Al Jazeera kuripoti kutoka ndani ya ardhi yake.

Na kutokana na military censorship iliyopo, yeyote atakayerusha habari za hiyo vita bila idhini, anajihatarishia kifungo jela.
Kwann hawataki habari zao zirushwe!
 
Watagwee mara ngapi
 
Mkuu nakuelewa vizuri sana
Tatizo ni kwamba Israel anajiona njia pekee ya kutatua changamoto zake za kikanda basi ni kutembeza kichapo

Sasa ili ifikie mahali atambue kwamba kichapo sio njia nzuri ni lazima na yeye achapwe bara bara kabisa

Na kiukweli mi nina maoni tofauti sana japo siipendi Iran haswa ku utawala wake wa kisharia
Lakini nadhani Iran wakiwa na nyukilia adabu itakuwepo pale mashariki ya kati...., shida zikitokea zitakua zinamalizwa na meza ya mazungumzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…