Zambia: Hakainde Hichilema atangazwa mshindi wa Urais

Mzee una chuki binafsi tu, kweli huelewi kwanini ni rahisi upinzani kushinda Urais kuliko bunge?

Zanzibar ina majimbo 50 ila kura za Urais hazizidi 500,000 lakini Dar Es Salaam ina majimbo 12 ina kura zaidi ya million 2. So unaweza ona jinsi urban votes huwa zinaubeba upinzani. Kwa mahesabu tu ukiweza kushinda urban centers zote Tanzania unapewa Urais asubuhi tu licha ya votes za maporini. Mfano jimbo la Mbagala lina kura zaidi ya laki 2 lakini majimbo ya kondoa huko mtu anashinda kwa kura elfu 15!!

Hata Raila odinga huwa anashinda Mombasa Nairobi na Kisumu.... Kwisha habari ndio maana licha ya kina uhuru kuzoa kura maporini huko unakuta hazitoshi mtu anaambulia 50% na anapewa Urais!! Same to Chamisa au Bobi wine ni urban votes tu hakuna uchawi mwingine.

Unadai wabunge wa upinzani wanashindaga..... Mkuu hta huyo Zitto 2010 bila intervention ya JK jimbo lilikua limeenda. Mie nilikua Ujiji pale CHADEMA tulishinda ubunge ila CCM wakadai kura zirudiwe kuhesabiwaeeh bwana eeh kura ziliongezeka ghafla na matokeo yakapinduliwa. Zitto muda huo yupo kaskazini naye upepo umemgeuka kaokolewa kwa directive ya JK otherwise angekua nje ya bunge toka 2010. Hakuna mpinzani analala nyumbani siku ya uchaguzi afu aamke atangazwe mshindi wote wanakesha na kuvutana mashati na polisi hadi mabomu yapigwe ndio anatangazwa.

Kma Mkapa mwenyewe anakiri tume huru ndio suluhu alafu ww unadai wapinzani wana baseless claims then utakua una chuki binafsi tu.
 
Vyama vyote vya upinzani Tanzania havijui kuendesha siasa, ila vinajua sana kulalamikia tume. Siasa zinaanzia kwenye grassroots, huwezi kupata kura za watu wasiokufahamu; vyama vya upinzani viko kwenye maeneo fulani ya nchi tu.
Hapana hapa sio kweli toka CHADEMA ni msingi ianze (Maana walau kimetapakaa zaidi) Hakuna kata haijafikiwa nchi hii na kwa takwimu za Serikali za mitaa 2014 utaona CCM iliambulia mitaa 60% pekee (Plus mapingamizi yaliyopelekea kupita bila kupingww) toka 99% ya 2009. Sasa kma mitaa 40% iliwapa upinzani na ni 2014 unadhani miaka 7 baadae yaani 2021 hyo mitaa na vijiji haviifaham upinzani??

Sahivi kuna mitandao na Tv kila kona huhitaji physical presence ndio watu wakujue.... Mimi nimeenda remote areas sana za nchi hii wana uelewa na mambo yanayoendelea duniani kuliko enzi zenu za 95 walipotegemea Radio Tanzania. So Hta Mbowe akitoa statement trust me hta kule kwetu Nyarubanda au Matyazo watapata habari ndani ya dakika 10.

Ukitaka kuprove hilo angalia kampeni za lissu mkoani muitikio wake...... kuna majimbo ya CHADEMA yanayoratibu grassroots ndio maana licha ya figisu za CCM, CHADEMA bado ilisimamisha wagombea vijiji na mitaa zaidi ya 95% huku bara. Kma sio kuenguliwa na tume kutokua huru nadhani tungepata jibu kamili la grassroot.
 
Marekani malalamiko?? Si mahakama zipo na zilikubali hadi kura zirudiwe kuhesabiwa na kma huridhiki una haki ya kupinga mahakamani!! Huwezi linganisha na Afrika kwa lolote lile hku hta kupinga mahakamani hairuhusiwi.

Unadai wanachagua watu 550!! Mbona hta sauzi huo mfumo upo mnapigia kura chama sio mtu then mwenye wabunge wengi ndio anachagua Rais na wabunge wake. Ina maana watu mnapiga kura indirectly na ndio maana mara zote anayeshinda kwa kura za raia anashinda na electoral college votes. Na mfumo uliwekwa ili majimbo yenye kura nyingi yasiburuze majimbo madogo maana ule ni muungano!!

Msipotoshe USA yupo mbali sana kidemokrasia kuliki hapa..... ulisikia Trumo kamtumia biden majeshi yamuweke ndani?? Au polisi wavamia ofisi za Democrats na kupora nyaraka??
 
God bless Zambia
 
Hapa umeandika blah blah nyingi kufurahisha moyo wako tu; hamna lolote - ni pumba tupu

Mkapa hakusema kuwa tume ya uchaguzi ya sasa huipendelea CCM, bali alisema kuwapo kwa tume itakayoonekana huru kutasaidia kupunguza vurugu zitokananzo na uchaguzi. Wewe ni mmoja wa wanaosoma habari kwa kuungaunga maneno kufurahisha moyo wako tu.
 
Duh...!. Hii ya jirani zetu Zambia kali!. Najua kuna Watanzania wengi na haswa wapinzani na wapenda mabadiliko, watafurahia matokeo ya Zambia kwa imani na matumaini kuwa hiki kilichotokea Zambia, "if it can happen in Zambia, then one day it can also happen in Tanzania". Naomba niwaandae kisaikolojia, "Zambia is Zambia na Tanzania is Tanzania" Kwa Tanzania, CCM itatawala mile...!, naomba nisimalizie.
P
 
Hiki ndiyo chama cha Kaunda kilichotawala miaka 27,wapinzani wakakitoa naona wamekirudisha tena ,waliokuwa wapinzani wake wameshindwa kuivusha ZAMBIA 🇿🇲
 
Sidhani kama kuna jipya, ila ni funzo baada ya wapinzani kukiondoa chama cha Kaunda, now kimerudi tena.....so wapinzani wameshindwa kuivusha nchi
 
Jibu facts mzee sio kweli urban votes zinabeba upinzani? Sio kweli Dar ilimpa lowassa zaidi ya kura million 2 ilihali Dar UKAWA ilipata majimbo 9 tu Dar.

Hivi hujiulizi ilikuwaje CUF ilipata wabunge zaidi ya majimbo 20 ile 2010 ila CHADEMA iliyopata majimbo 27 pekee ilipata viti maalum zaidi ya 25 hku CUF ikiambulia chini ya 5??? Meaning ukishinda kwenye majimbo makubwa ya mjini unapata kura nyingi cumulative kuliko ushinde majimbo 20 kwenye pool ya kura laki 2!!

CHADEMA mbunge 1 2020 ila viti maalum 19.... CUF mbunge 1 na ACT wabunge 5 ila viti maalim 0??? Hujiulizi why??

We mzee toka upotoshe JPM yupo hai hauna credibility ya kuwa fact finder zaidi ya mzee wa speculation tu.
 
Hiki ndiyo chama cha Kaunda kilichotawala miaka 27,wapinzani wakakitoa naona wamekirudisha tena ,waliokuwa wapinzani wake wameshindwa kuivusha ZAMBIA 🇿🇲
Hapana.

Chama cha Kaunda kilikuwa kinaitwa UNIP; kiongozi wa UNIP kwenye uchaguzi alikuwa Askofu Mwamba na wala hakupata kura nyingi.
 

Kwa sababu hujui mahesabu ya kura za uchaguzi, upo unabwabwaja tu kutafuta huruma. Yaani hata huji katiba inasemaje kuhusu viti maalumu vya ubunge.
 
Kwa sababu hujui mahesabu ya kura za uchaguzi, upo unabwabwaja tu kutafuta huruma. Yaani hata huji katiba inasemaje kuhusu viti maalumu vya ubunge.
Sio katiba viti maalum ni kura za ubunge tu, tena inatumika D'Hondt method of proportion kwa thresholds ya 5%. Hivyo chama kikivuka overall kura za ubunge 5% inakuwa eligible kupata allocation ya viti maalum based on % ya kura ilizopata vis a vis za washindani wake.

Sasa hao ACT au CUF hawakufika hapo.... Ina maana hata CHADEMA ikiwa runner up majimbo yote bara na ikakosa mbunge wa jimboni bado ina safety net ya wabunge wa viti maalum walau 20!!

Sasa ndio hoja najengea owa hesabu hizo kuwa kura cumulative ndio zinaipa nguvu upinzani kuliko namba za jimbo moja moja. Kura za Mdee tu pale Kawe ni sawa na majimbo 5 ya Dodoma!! Upgrade your maths!!


Get real
 
 
Tume za uchaguzi zikiwa huru
Tume ya uchaguzi ikiwa huru ni raha sana. Hongera kwa Rais aliyeshinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…