Kwanini mkuu unatetea Zanzibar kuwa na ardhi bara na wakati sisi haturuhusiwi? mbona unaruhusiwa kumiliki ardhi Dar au Mwanza na siyo Zanzibar? hakuna muungano hapo ni fake na tunanyonywa sn, wanzibari hatuwataki waondoke warudi kwao
 
Siyo fake , tena naona kama hizo alizosema zimebaki kidogo.

Zanzibar walipewa kihalali kabisa ardhi kubwa sana ya kupumzishia mifugo yao wanayoinunuwa bara kabla ya kuisafirisha kuipeleka Zanzibar.
Walipewa kihalali kabisa

Na ilikuwa inatumika kama ranchi

Ya kuwekea mifugo yao

Na vibao vya alama vilikuwepo

Labda kama watu waviondoe

Kwa watu wengine hii siyo kitu kigeni

Ova
 
Uzalendo wa mtu uko moyoni mwake!. Nimeishi UK, nikahamia US, wife na watoto wakabaki kule, mimi nikarejea Bongo kwa uzalendo tuu.



P
Kwanini hutetei maslahi ya bara mara unasifia mafisadi yanafilisi nchi? why zamani hapa JF ulikuwa unasifiwa na wazalendo wote kwanini sahihi watu wanakuona mtu wa ajabu? jitafakari mkuu
 
Kwanza hatumtaki akaongoze Zanzibar si tumemchoka
 
Sishangai, kwa sababu Nchi ina Raia wapumbavu haijawahi tokea, kutwa nzima ni Yanga na Simba unategemea nini? Yaani watu ni Yanga na Simba huku watawala wakiineemeka na keki ya ncni

Wakitoka kwenye Simba na Yanga, na kwenye ushabiki wa CCM, mara ooh CCM ni chama dume, CCM itatawala milele, upinzani hauna impact, hakuna wa kumtoa Tulia pale Mbeya! Unabaki unashangaa na kujiuliza, kama kweli hawa watu wana akili au ni punguani. Hivi CCM kutawala milele au Tulia hata awe mbunge wa maisha, inakusaidia nini?

Hivi muhimu ni kuwa na chama kinachotawala milele na wabunge wa milele au kuwa na chama kinachoweza kuunda Serikali adilifu, serikali bunifu na ilivyo na uwezo wa kusimamia mipango na rasilimali kikamilifu kwa kufuata sheria na taratibu, ili vyote kwa pamoja viisaidie nchi na wananchi kupata maendeleo au mradi tu unachama kinachotawala milele?

Hivi ni muhimu kuwa na wabunge wa milele au wabunge wanaojirambua, wakweli wa nafsi, wasio na unafiki wa kujikomba kwa Serikali ili tu matumbo yao yawe na uhakika wa kushiba huku wakivizia teuzi kutoka kwa watawala?

Wapo watu wengi kwao ujinga, unafiki, na uwendawazimu ni sifa wanayoutaka na wanailinda kwa nguvu zao zote. Lakini mambo yale yaliyo muhimu, yanayoashiria werevu na ufahamu, wanayakimbia kwa sababu wamefunga ndoa za kudumu na unafiki na ujinga.
 
Zanzibar walipewa kihalali kabisa ardhi kubwa sana ya kupumzishia mifugo yao wanayoinunuwa bara kabla ya kuisafirisha kuipeleka Zanzibar.
Hilo nalo ni kosa kubwa, yaani kuwanyima fursa ya biashara na kipato wabara..
Inafaa wafanyabiashara wa mifugo wa Bara ndo wapeleke mifugo kuuza Zanzibar, siyo wao wenyewe kuja kununua kwa wenyeji.

Ukitaka Bara uende Zanzibar kulangua karafuu yao hawawezi kukuelewa wale, utazuiwa!
 
Umewahi hata kufika Zanzibar wewe? Hairuhusiwi mtu wa bara kumiliki kiwanja na kugombea uongozi wa aina yoyote huku
Kiwanja nakataa, nimekaa Znz miaka mitatu, kuna watu wengi wabara wanamiliki viwanja na wejenga, nimeoa huko pia mkuu
 
Kiwanja nakataa, nimekaa Znz miaka mitatu, kuna watu wengi wabara wanamiliki viwanja na wejenga, nimeoa huko pia mkuu
Kuoa rukhusa lkn kununua kiwanja hapana. Mm nimekaa miaka 6 maeneo ya Fuoni nikifanyia kazi zangu maeneo ya Daraja bovu na Kwerekwe
 
Kuoa rukhusa lkn kununua kiwanja hapana. Mm nimekaa miaka 6 maeneo ya Fuoni nikifanyia kazi zangu maeneo ya Daraja bovu na Kwerekwe
Mkuu wapo ndugu zangu ni watu wa bara na wamenunua maeneo huko,
 
Sasa tangu mwaka 1977 ni kwanini hamfanyi muendelezo wowote? Sheria inasemaje kama eneo lenye hati halijaendelezwa kwa zaidi ya miaka miwili?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…