Zanzibar: Hekta 6,000 zilizopo Bagamoyo ni mali yetu
Uzalendo wa mtu uko moyoni mwake!. Nimeishi UK, nikahamia US, wife na watoto wakabaki kule, mimi nikarejea Bongo kwa uzalendo tuu.

Nikatubu kwa kosa gani?.

Ni kweli kuna kauli zinaumba, kabla ya kuitwa njaa, nilikuwa na 6 government contracts za Publicity, nikilipa kodi ya mishahara ya RC na DC. Baada ya kuitwa njaa, contracts zikafutwa njaa ikanitembelea kweli. Uchumi wa Magufuli: Sekta Binafsi ina-Suffer. Yalianza Maduka, Yakafuata Mashirika, Sasa ni Zamu ya Media Ina-suffer

Ni kweli tulikuwa tunafahamiana vizuri kabla hajawa rais nikienda pande zile nafikia kwake!. Ni mimi ndiye mtu wa kwanza ile 2014 kueleza humu kuwa JPM ndie anakwenda kuwa rais wetu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, ni mimi nilieleza humu kuwa JPM ni dikiteta Tanzania iliyomuhitaji Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania ilihitaji Dikiteta, tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!, ni mimi niliyeeleza humu the consequences ya udikiteta wake Elections 2015 - If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's pray for him! . Ni mimi nilieleza nia ovu ya mabeberu kumuondosha US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali? nikawaeleza wake jamaa zetu kuhusu mpango huu Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya? hawakusikia!, watu wa kazi zao wakafanya yao!, bado ni mimi ndio nimeelezwa mahali alipo sasa Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani hivyo namjua inside out!.

P
Kwanini mkuu unatetea Zanzibar kuwa na ardhi bara na wakati sisi haturuhusiwi? mbona unaruhusiwa kumiliki ardhi Dar au Mwanza na siyo Zanzibar? hakuna muungano hapo ni fake na tunanyonywa sn, wanzibari hatuwataki waondoke warudi kwao
 
Siyo fake , tena naona kama hizo alizosema zimebaki kidogo.

Zanzibar walipewa kihalali kabisa ardhi kubwa sana ya kupumzishia mifugo yao wanayoinunuwa bara kabla ya kuisafirisha kuipeleka Zanzibar.
Walipewa kihalali kabisa

Na ilikuwa inatumika kama ranchi

Ya kuwekea mifugo yao

Na vibao vya alama vilikuwepo

Labda kama watu waviondoe

Kwa watu wengine hii siyo kitu kigeni

Ova
 
Uzalendo wa mtu uko moyoni mwake!. Nimeishi UK, nikahamia US, wife na watoto wakabaki kule, mimi nikarejea Bongo kwa uzalendo tuu.



P
Kwanini hutetei maslahi ya bara mara unasifia mafisadi yanafilisi nchi? why zamani hapa JF ulikuwa unasifiwa na wazalendo wote kwanini sahihi watu wanakuona mtu wa ajabu? jitafakari mkuu
 
Watu hamfuatilii mambo kwa undani. Tokea kifo cha Magufuli na baada ya kuondolewa Lukuvi wizara ya ardhi sasa hivi kila mahali nchi nzima ni migogoro ya ardhi kuanzia Mabwepande hapo DDC na NSSF wameibuka wanasema eneo lao, huko Bagamoyo Fukayosi wanasema ranchi ya Taifa, SMZ nao wanataka eneo lao huko Bagamotyo, Mbarali nako vijiji zaidi ya 29 eti vipo hifadhini, Morogoro watu wamevunjiwa nyumba kabisa, Kigamboni nako hakujatulia, Kibamba nako kunafukuta na huyu mdudu anayeitwa DDC hapo nikitaja maeneo machche tu maana migogoro ni mingi mno kipindi hiki.

Kwa aliye karibu na raisi Samia amwambie tu kama kuna kitu kitakachomuangusha yeye na chama chake kwenye chaguzi zote zinazokuja hivi karibuni kuanzia wa serikali za mitaa mwaka 2024 basi ni hii migogoro ya ardhi kwani ardhi ndio urithi kwa masikini baada ya elimu.
Kwanza hatumtaki akaongoze Zanzibar si tumemchoka
 
Sishangai, kwa sababu Nchi ina Raia wapumbavu haijawahi tokea, kutwa nzima ni Yanga na Simba unategemea nini? Yaani watu ni Yanga na Simba huku watawala wakiineemeka na keki ya ncni

Wakitoka kwenye Simba na Yanga, na kwenye ushabiki wa CCM, mara ooh CCM ni chama dume, CCM itatawala milele, upinzani hauna impact, hakuna wa kumtoa Tulia pale Mbeya! Unabaki unashangaa na kujiuliza, kama kweli hawa watu wana akili au ni punguani. Hivi CCM kutawala milele au Tulia hata awe mbunge wa maisha, inakusaidia nini?

Hivi muhimu ni kuwa na chama kinachotawala milele na wabunge wa milele au kuwa na chama kinachoweza kuunda Serikali adilifu, serikali bunifu na ilivyo na uwezo wa kusimamia mipango na rasilimali kikamilifu kwa kufuata sheria na taratibu, ili vyote kwa pamoja viisaidie nchi na wananchi kupata maendeleo au mradi tu unachama kinachotawala milele?

Hivi ni muhimu kuwa na wabunge wa milele au wabunge wanaojirambua, wakweli wa nafsi, wasio na unafiki wa kujikomba kwa Serikali ili tu matumbo yao yawe na uhakika wa kushiba huku wakivizia teuzi kutoka kwa watawala?

Wapo watu wengi kwao ujinga, unafiki, na uwendawazimu ni sifa wanayoutaka na wanailinda kwa nguvu zao zote. Lakini mambo yale yaliyo muhimu, yanayoashiria werevu na ufahamu, wanayakimbia kwa sababu wamefunga ndoa za kudumu na unafiki na ujinga.
 
Zanzibar walipewa kihalali kabisa ardhi kubwa sana ya kupumzishia mifugo yao wanayoinunuwa bara kabla ya kuisafirisha kuipeleka Zanzibar.
Hilo nalo ni kosa kubwa, yaani kuwanyima fursa ya biashara na kipato wabara..
Inafaa wafanyabiashara wa mifugo wa Bara ndo wapeleke mifugo kuuza Zanzibar, siyo wao wenyewe kuja kununua kwa wenyeji.

Ukitaka Bara uende Zanzibar kulangua karafuu yao hawawezi kukuelewa wale, utazuiwa!
 
Umewahi hata kufika Zanzibar wewe? Hairuhusiwi mtu wa bara kumiliki kiwanja na kugombea uongozi wa aina yoyote huku
Kiwanja nakataa, nimekaa Znz miaka mitatu, kuna watu wengi wabara wanamiliki viwanja na wejenga, nimeoa huko pia mkuu
 
Kiwanja nakataa, nimekaa Znz miaka mitatu, kuna watu wengi wabara wanamiliki viwanja na wejenga, nimeoa huko pia mkuu
Kuoa rukhusa lkn kununua kiwanja hapana. Mm nimekaa miaka 6 maeneo ya Fuoni nikifanyia kazi zangu maeneo ya Daraja bovu na Kwerekwe
 
Kuoa rukhusa lkn kununua kiwanja hapana. Mm nimekaa miaka 6 maeneo ya Fuoni nikifanyia kazi zangu maeneo ya Daraja bovu na Kwerekwe
Mkuu wapo ndugu zangu ni watu wa bara na wamenunua maeneo huko,
 
Leo nimekutana na clip ya Chars Hilary akiongea akitanabaisha kuwa kuna hekta elf 6 wilayani Bagamoyo ni mali ya serikali ya Zanzibar na mtu kutoka bara haruhusiwi kufanya shughuli za aina yoyote ndani ya ardhi hiyo kwani sio mali ya serikali ya Tanzania bara.

Jambo hili limenisikitisha sana and sijajua inakuwaje wazanzibari wawe na ardhi yao Tanganyika wakati mtanganyika ukifika Zanzibar ni sawa umeenda Kenya tu.

======
Msemaji wa Serikali ya Zanzibari, Charles Hillary amesema Shamba la Zaba lililoko Makurunge wilayani Bagamoyo ni mali ya Serikali ya Zanzibar hakuna mtu anayeruhusiwa kufanya shughuli yoyote eneo hilo.

Msemaji amesema Zanzibar imemiliki eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 6000 tangu mwaka 1977. Na amesema yoyete atakayeuziwa eneo katika ardhi hiyo hatalipwa fidia.

Sasa tangu mwaka 1977 ni kwanini hamfanyi muendelezo wowote? Sheria inasemaje kama eneo lenye hati halijaendelezwa kwa zaidi ya miaka miwili?
 
Back
Top Bottom