PreGE2025 Zitto Kabwe: Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, Karibuni ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Zitto ni mpiga dili na wala hili si geni masikioni mwa watanzania.

NI kati ya wanasiasa vijana wasioaminika kabisa.
 



🤣
 
Kweli kabisa, kati ya makosa walivyofanya wanachama wa CUF ni kujiunga na ACT, binafsi ninaona kwa misimamo ya Wazanzibari walitakiwa wajiunge na CHADEMA
Priority ya CUF ya Maalim ilikuwa ni Zanzibar. Hilo CDM wasingekubali. Mojawapo ya sababu ya kutofautiana na Profesa ilikuwa hilo.

Amandla...
 
Anza kuwakarbisha mpox55 na m.kiti mwenza
 
Wale wa upande ule, maarufu kama G55 fursa hiyo

Achaneni na CDM inayowahurumia kuwapeleka kwenye Uchaguzi ambao Wana uhakika hamtatangazwa washindi hata kama mtashinda

Achaneni na CDM ambayo imechoka kuona damu inamwagika ili mshindi wa CDM atangazwe
 
1. Kama hayajanza leo na ni tabia iliyozoeleka wewe huoni CHADEMA wanafanya vizuri kurekebisha? Yaani unataka kutuambia kuwa kitu kibaya na chenye madhara kama kimezoeleka kinakuwa ni kizuri?
2. ACT (former CUF) hawana uwezo wa kuwa na viti Pemba kama CCM ikiamua kuwanyang'anya. Yes, haijalishi wananchi watampa nani kura, lakini bila CCM kuwaachia hawana uwezo. Ni kweli kura zikipigwa kihalali CCM haishindi lakini ukweli ni kwamba mambo hayako hivyo.
3. Kama hakutakuwa na reforms za maana basi ni bora kuwa nje ya bunge mpaka siku wananchi watakaelimika na kudai mabadiliko kwa nguvu. Kuna umuhimu gani wa kuwa bungeni kwa maigizo?
 

Nakazia
 

Kweli kabisa mkuu. Umeongea ukweli.
 
Lissu aliishasema kuwa mazungumzo yameanza na baadhi ya hao mnaowaita Covid-19. Kwa hiyo nae ni msaliti?

Amandla...

Acha upotoshaji. Sio mazungumzo wameandika barua ya kuomba msamaha. Ni wawili tu.
 
Wanataka kufanya siasa au wanataka vyeo? Jamaa huyu sijui aliwezaje kuwateka CUF wakaingia kwenye hamsini zake. Hawa watu kiu yao kubwa ni vyeo.
Kuna siasa ambayo haina vyeo?.Siasa ni mchezo wakunyang'anyana vyeo na madaraka kupitia mgongo wa wananchi.Wanasiasa wote duniani lengo lao ni moja.
 
CDM walichofanya , kilipaswa kufanywa na vyama vingine ili kuwamsha ccmu

Ila ACT WAZALENDO na wenzao wamefanya utoto ambapo ni kama watajipotezea ushawishi na mwaka 2030 wananchi hawatapepesa macho wataona bora ccmu kuliko hawa akina ACT
Unaposema wananchi jizungumzie wewe mwenyewe kwasababu ata hao waliomo Act ni wananchi pia na wataunga mkono chama chao.
 
Zitto ni mjanja na anajua mbinu na fitina za siasa zakiafrika.Anajenga chama polepole ila kijanja.Miaka michache mbele watu hawataamini hicho chama jinsi kitakavyokua na wafuasi.
 
Zitto ni mpiga dili na wala hili si geni masikioni mwa watanzania.

NI kati ya wanasiasa vijana wasioaminika kabisa.
Wasioaminika na nani?.Sema usiyemwamini kwasababu ya mtazamo wako.siasa ina mambo mengi sana.
 
si
tuliambiwa kuwa huyu kastaafu uongozi ACT, mbona kila siku anatoa matamko kwa niaba ya chama?
 
Sasa kumekucha sasa kumekucha dodoma kada wa zambarau apewe kura za ndio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…