Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Safari hii CCM itawapiga wanawake zake wote kwa mkupuo kama ilivyokuwa 2015
 
Hueleweki nini unataka kwanini uliweka mgombea ilihali ukijua hana nguvu? Si mlipewa muda na utaratibu wa kuungana ... WE MPIGIE UNAEMUONA ANAFAA NA SISI TUTAMPIGIA TUNAEMUONA ANAFAA
 
Yeye kama yeye kadeclear kumpigia Lissu. Anawashaurije wafuasi wake?

Membe atampigia nani? Mbona kuna kigugumizi
kwenye hii issue? Chama kimeshindwa kuafikiana!?
Ameshasema tutampigia kura mpinzani ambae atakua na ushawishi kuliko wengine, so kwa maana nyingine hata chauma wakiwa na ushawishi kuliko vyama vyote vya upinzani Basi maelekezo ya Zitto yange apply
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Membe sasa hivi haamini macho yake kama hawa ndio watz wale wale wa mitandaoni waliomshabikia miezi kadhaa iliyopita.

Zitto ana zambi sana. Mlichomfanyia Membe Mungu atawalipa.
Kama alitumwa arudi akawaambie watanzania wameshtuka.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Shida itatokea pale Lissu akipata urais kila mtu atasema anataka uwaziri mkuu kwa sababu alimsaidia kuupata huo urais na ugomvi mkubwa utatokea miongon mwao
 
Ameshasema tutampigia kura mpinzani ambae atakua na ushawishi kuliko wengine..
Kasema hivyo kwa diwani na Ubunge ila hajasema hivyo kwenye Urais.

Kwenye Urais kasema YEYE atampigia Lissu then kawaacha nyie mtumie bongo zenu
 
MSIMAMO RASMI WA ACT WAZALENDO KUSHIRIKIANA NA CHADEMA.

Hivyo basi, baada ya maelezo hayo, natangaza rasmi kwa Wanachama, Wafuasi, wapenzi wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa Ujumla, kuwa:

1. Pale kwenye Kata ama Jimbo ambalo ACT Wazalendo tuna Mgombea, tunaomba Muwapigie Kura wagombea wa ACT Wazalendo.

2. Pale ambapo kwenye Kata au Jimbo la Uchaguzi hakuna Mgombea wa ACT Wazalendo, lakini kuna wagombea wengine wa Vyama vya Upinzani, ACT Wazalendo tunawaomba MPIGIE KURA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI mwenye nguvu zaidi ili kutokutawanya Kura.

3. Kwa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe NITAPIGA KURA YANGU kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai LISSU. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda Mgombea wa Chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa Wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo, pamoja na anayotaka kuyafanya kama Rais, ni mambo hayo ndiyo yaliyonipa msukumo wa kumpigia Kura Lissu.

Zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu. Ninaomba kila mpenda Haki na Mabadiliko nchini ampigie kura ya URAIS ndugu Tundu Lissu ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natanguliza Shukran kwenu

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bangwe, Kigoma Mjini
Oktoba 16, 2020
Mimi Simoni Siro maarufu kwa jina la Malcom xx hapa jamii forum natangaza kumpigia kura Lissu katika kiti cha urais wa Jamhuri ya muumgano wa Tanzania.

Pia familia yangu nayo imekubali kumpigia Lissu kura
 
MSIMAMO RASMI WA ACT WAZALENDO KUSHIRIKIANA NA CHADEMA.

Hivyo basi, baada ya maelezo hayo, natangaza rasmi kwa Wanachama, Wafuasi, wapenzi wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa Ujumla, kuwa:

1. Pale kwenye Kata ama Jimbo ambalo ACT Wazalendo tuna Mgombea, tunaomba Muwapigie Kura wagombea wa ACT Wazalendo.

2. Pale ambapo kwenye Kata au Jimbo la Uchaguzi hakuna Mgombea wa ACT Wazalendo, lakini kuna wagombea wengine wa Vyama vya Upinzani, ACT Wazalendo tunawaomba MPIGIE KURA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI mwenye nguvu zaidi ili kutokutawanya Kura.

3. Kwa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe NITAPIGA KURA YANGU kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai LISSU. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda Mgombea wa Chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa Wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo, pamoja na anayotaka kuyafanya kama Rais, ni mambo hayo ndiyo yaliyonipa msukumo wa kumpigia Kura Lissu.

Zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu. Ninaomba kila mpenda Haki na Mabadiliko nchini ampigie kura ya URAIS ndugu Tundu Lissu ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natanguliza Shukran kwenu

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bangwe, Kigoma Mjini
Oktoba 16, 2020
zito unatuchanganya sisi wapiga kura, maana sisi tunamtambua Membe sasa kimetokea nini ?! unapaswa utoe tamko rasmi na uelezee sababu za kufanya hivyo
 
Back
Top Bottom