Aibu kubwa kwa Taifa taa za uwanja wa Benjamini Mkapa kuzimika mechi ikiwa inaendelea
Kwa mjibu wa sheria za CAF! Zikipita dakika 10 bila umeme kutengamaa, basi yanga ataaga mashindano hayo leo!

Hii ni mara ya pili baada ya ile mechi ya Taifa stars na Uganda, shida ni nini?

Tukienda tu kwa kubembelezana kama ilivyo kwa Waziri wa Nishati! Iko siku tutapata bonge la Aibu zaidi ya hili la umeme kuwa mdogo kwenye uwanja wa Mkapa mechi ya kimataifa inayohusisha Timu za Yanga na Rivers!

Halafu sijui ni kwa nini huwa inakuwa hivi!

Kila mtu aliyewahi kulalamikiwa sana na wananchi kwenye tawala hizi, mtu huyo huja kuwa sababu ya serikali kufeli vibaya na kuwa ya hovyo hovyo tu

Nchi nzima kwani imekosa watu makini hadi iwe yuleyule tu aliyefeli hata kabla ya kuanza?

Hivi majuzi kwenye ziara ya Rais kabisa kule Arusha! Umeme ulikatika mbele yake na bado mh Januar Makamba bado aliendelea kuwa waziri

Mfano

Makonda!
Imejibiwa.
TANESCO.: HAWAHUSIKI.
 
Acha mahasira na msongo wako wa mawazo hapa,mh Rais na serikali Yake wanapaswa kupongezwa Sana kwa hapa walipotufikisha kimaendeleo mpaka kupigiwa mfano na kila mtu,

Usitake kumpangia mh Rais wa kufanya nae kazi, yeye ndio anafahamu afanye kazi na Nani katika kuwaletea na kuwapatia huduma Bora watanzania katika kila eneo,

Suala la habari au hitilafu ya umeme kwa muda mfupi tu Ni masuala na changamoto ndogo ndogo ambazo zinatokana na masuala ya kutamalaki tu.

Uwe na shukurani na moyo wa kupongeza na kukubali pale kazi nzuri inapofanyika, serikali hii imekuwa ikijitahidi kwa kila namna kupambana na kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mbele yetu Kama Taifa.

Wapo majirani zetu kwa Sasa Ni shida na changamoto kulipa mishahara ya watumishi wake wa umma, vipi ingekuwa ndio Tanzania? Ungesemaje? Ungeandika mangapi? Lakini kwa ushupavu na uimara wa serikali yetu tunaona watumishi wa umma wakipokea mishahara mapema kuliko ilivyo kawaida Hadi wao wenyewe wanamshukuru mh Rais na serikali yake,.

Vichangamoto vidogo vidogo visitufanye tukawa watu wa kuropoka ropoka maneno mabaya kuelekeza kwa serikali yetu
 
Mkuu sio watu wa pwani wote wapo hivyo ni hulka ya mtu tuu.... Na inawezekana hizo hitilafu za taa kupungua nguvu zinatokea sana hata kwenye mechi za ligi kuu bara na michuano ya fa ila nachelea kusema marefa wetu na hata sisi tunaotazama hatunote hiyo kitu! Hawa marefa wa kimataifa wanajua kazi zao haswa mkuu.
 
Magufuli hakupenda ujinga kama huu wa uwanja wa taifa lakini ukali wake ulipitiliza na akashindwa kuweka mipaka ya hukumu alizotoa kwa wakosaji.

Kibaya kingine JPM alikuwa anafurahi anapoona mtu au kundi la watu wanapitia hali ngumu ya kimaisha. Aliyafurahia mateso ya wakosaji wake kama vile sio rais wa nchi, kama sio rais wa wote milioni 60. JPM alipenda kuona sadism na urais wake ulifurahisha wengi lakini ulimuuza wachache.
 
IMG_0527.jpg
 
Matendo ya hovyo yanayoendelea nchini ni dalili kuwa hii nchi inaongozwa na watu wasiostahili. Haiwezekani taa za uwanja wa taifa zinapata hitilafu kwa mara ya pili ndani ya miezi 3. Uongozi sio kuahidi mamilioni baada ya ushindi huku miundombinu haisimamiwi ipasavyo.

Hebu tumia mamlaka yako ya Urais kuwawajibisha wasiotaka kuwajibika.
Aisee
 
Mimi nalitizama tofauti Huyo Waziri Muhusika ndio apewe lawama ama ajiwajibishe mwenyewe saa ingine unaongea kwasababu uko nje ukiingia ndani unaufyata mkia...let's not blame her over evereeethng na japo Mama asitumie tena kauli ya hili nalo mkalitizame inakuwa inasound kama nyama choma bila chumvi na pilipili.....
 
Naona wabongo ni full kulalamika
[emoji1]

Ova
 
January Makamba, Nape Nnauye na wengine waliokataliwa na JPM wamerejeshwa na Samia, leo ni mara yapili taa za uwanja wa taifa zinapata hitilafu, huu uwanja ni mali ya serikali, inaelekea serikali haikujali aibu ya sikuile na leo wameirudisha tena aibu hiyo. Amakweli huwezi mbebesha mtoto wa pwani gunia la kilo 100, atakufa tu.
Serikali tukufu
 
Back
Top Bottom