Kama zipo kesi kadhaa na zote zinafanana bado tu hatujaliona tatizo liko wapi?

Kwamba kesi nyingi Kama zake wanashikwa then baada ya muda wanaachiwa, hapa bado pia tunajifanya vipofu hatuoni kabisa adui aliyesimama kati yetu wananchi na vibaka ni nani?


Sijawahi kujua kwanini hatupendi kabisa kuwajibika na badala yake tunatatua changamoto zetu kwa kutumia matokeo na sio vyanzo/mizizi.
 


Maajabu sasa ya hii jamii yetu ni kwamba bado tumegoma kuwajibika kwenye uhalisia.

Tumekua wataalamu wa kuyachonga mavinyago ya kutisha na mwisho wa siku yanaanza kututisha wenyewe wahunzi.
 
Kwa ile maneno ya karuka kwenye defender ikiwa mwendo ni Chai siyo? [emoji12]
 
Nasisitiza angalia sehemu nimesema wengine hutoroka mikononi mwa vyombo vya sheria. Siyo wote Wana achiwa huru.
Kumbuka wengi wa hawa ni wahalifu sugu ambao hawaogopi kifo wanajaribu kukimbia mbele ya askari wenye bunduki.
Hawaogopi kifo sababu wameshauwa zaidi ya mara moja.
 


Tuangalie case ya huyu Allay Dangote.

Angalia size yake na size ya hao Askari aliojaribu kuwatoroka.

Tuangalie kwa u ndani hayo mazingira na namna ya ukamataji unaoshindwa kumdhibiti mtoto wa miaka 19 akiwa chini ya ulinzi mpaka apate mwanya wa kutoroka.

Na mwisho tuangalie kwanini watuhumiwa wote wanaojaribu kutoroka ni lazima wauawe kabisa badala ya kuvunjwa miguu (kwa risasi) ili kumaliza hizo mbio?



Tukubali tu ni jamii tuliyoshindwa. Mitaa inawatengeneza kina Ally Dangote then mamlaka zinazopaswa kudeal nao kwa kufuata utaratibu tuliojiwekea sisi wenyewe, zinafanya maamuzi ya kutumia njia ya mkato kumaliza tatizo jambo ambalo badala litoe matokeo chanya linaleta matokeo tofauti na hatimaye a circle of misery is created.
 
Nani kakuambia

Mbona Dar vibaka wezi wakabaji

Washasulubiwa sana

Ova
Muulize kama anaujua mtaa wa Congo wa mwanzoni mwa miaka ya 2000 mpaka katikati mwa miaka hiyo kuanzia juu kule mpaka stendi ya Mwananyamala kama mtu alikuwa anapita mtaa ule na wallet mfuko wa nyuma. Leo hii ni shwari kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…