Amos Makalla amshambulia Freeman Mbowe mbele ya Rais Samia
Ndiyo huyu huyu alituambia mabadiliki ya Hali ya hewa sio sera ya CCM ni mpango wa MUNGU mabwabwa kukosa maji na CCM haihusiki,tulishangaa!!
 
Rais Samia Kuna watu eti wanakukosoa kwa maboresho ya Bandari zetu ilhali umefanya jambo hilo kwa uwazi Bungeni kama Azimio. Yeye Mbowe (Freeman) hasemi kama wameanza kupokea ruzuku tena kachukua Bilioni 2 na kusweka mfukoni kwake kimya kimya. Sasa nani muwazi kati Yako na yeye?
Ukiangalia kwa jicho la tatu, haya ni maneno ya Samia anamwambia Mbowe kupitia kinywa cha Makala.

Hii ni kauli ya kimkakati, haikutoka bahati mbaya....Makala ni punda mbeba mzigo.
 
Makala ameyasema hayo Mwanza ambako Rais Samia anashiriki Tamamasha la Bulabo kuwa, Mbowe alifanya siri kusema kuwa wameanza kupokea ruzuku wakati Rais Samia amepeleka Mkataba bungeni wazi kabisa kwa wabunge kujadili na kupitisha.

Makalla akaendelea kuwa wengine hata haya mambo madogo wanafanya siri, kama wakipewa nchi si hatari? Na kwamba Rais anatakiwa kutembea kifua mbele kwani wananchi wana imani sana na yeye.
Wananchi gani anaosema wanampwnda Samia.
 
Katika hatua ya kuonesha kujipendekeza kulikopitiliza, RC Amos Makalla amesema:

"Rais Samia Kuna watu eti wanakukosoa kwa maboresho ya Bandari zetu ilhali umefanya jambo hilo kwa uwazi Bungeni kama Azimio. Yeye Mbowe (Freeman) hasemi kama wameanza kupokea ruzuku tena kachukua Bilioni 2 na kusweka mfukoni kwake kimya kimya. Sasa nani muwazi kati Yako na yeye".

Makalla amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan katika tamasha la utamaduni Bulabo hapa Mwanza.

Chanzo: TBC1
 
Mkuu.wa mkoa sio mwanasiasa ni kiongozi wa serikali

Alitakiwa kumpa Raisi ripoti za utendaji kazi mkoani mwake, maendeleo yaliyofanyika changamoto za mkoa zinazohitaji ufumbuzi wa Raisi

Sio hizo porojo zake za akina Mbowe hizo aachie viongozi wa CCM na jumuiya zake Mwanza na wilaya zake
 
Makalla kulinda heshima yako, umri wako na elimu yako, suala kuuzwa kwa Bandari muachie aliyesaini mikataba.

Ukiligusa mwanza utapaona pachungu brother
 
Kweli linapofikia suala la Wizi wa mali za Umma, Makada wote wa Chama Tawala huwa wamoja.

Walianzia Bungeni na sasa wateule wa Rais.

Watanzania kuna haja tukaungana kukemea huu Wizi wa hawa Mabwenyenye wanaoshinda Kutwa kula na Kuvaa kwa Kodi zetu.

Walianzia kwenye Ngorongoro, Gesi ya Mtwara, Viwanda vyote kama Urafiki n.k na Sasa wamehamia Kwenye Bandari

Tukiendelea kukaa kimya hawa Watu watakuja kutuuza Watanzania wote
 
Ukiangalia kwa jicho la tatu, haya ni maneno ya Samia anamwambia Mbowe kupitia kinywa cha Makala.

Hii ni kauli ya kimkakati, haikutoka bahati mbaya....Makala ni punda mbeba mzigo.
Kwa hiyo Samia anawambia Watanzania kuwa anagawa hela yao kiholela bila kufuata taratibu. Haya endeleeni kumpaka kinyesi huyo Hangaya wenu.
 
Back
Top Bottom