Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Anayejua Rais Samia Suluhu anatupeleka wapi atuambie, naona kama tunapotea

Ahaaa timu magu mnateseka sana sasa hivi na bado mtaumia sana tulie wakati wenu umepita
 
Mimi namshangaa sana Mama.....cheap popularity itammaliza
Wewe nikilaza mkubwa sisi asipotekeleza Yale ya kwenye ila sawa sasa hivi tunataka faraja kwa madhila tuliyopitia miaka mitano ya jitu lile lenye roho mbaya utafikiri hakuzaliwa na mwanadamu
 
1. Kodi ni two way traffic kuna makosa ya watoza kodi na hakuna anayesema wanaokwepa kodi!![emoji1787]


2. Wawekezaji lazima wawe monitored cautiously, kinyume chake ni kilio


3.Serikali inaenda kutegemea matajiri na wawekezaji kwenye kuomba misaada, kuikopesha serikali n.k


4.Mwako wa kila mtu achume kwa nafasi yake kwa any loose statements za sasa zitakuwa kubwa, matajiri wanaenda kuwa matajiri zaidi na maskini kutoboa kazi sana


5.Relaxation kubwa inaenda kutokea na uwajibikaji utapungua maofisini, trust me


6.Social media, magazeti n.k yataumiza sana watu binafsi kwa kuandika scandal nyingi, uzushi mwingi...JK na ze utamu ni mhanga wa era ya sasa ya social media


7.Kutaka kujenga urafiki na wageni yahitaji umakini sana


8.Kuruhusu madini kuchimbwa serengeti inahitaji umakini mkubwa


Tunaweza kuwalaumu sana wale wasifia sifia za kizembe na za kumkufuru Mungu ambazo kuna nyakati JPM aliwashushua...na hawa tunawaita MATAGA sio? lakini ukweli ulio dhahiri MATAGA no. 1 ni Samia Suluhu mwenyewe


watu wakimchoka na aki mess up..atadhalilishwa sana na hizo media!!! akidhalilika next time anaweza kubadilika ....


Natamani sana na namwombea twende vizuri, ila ile era ya JK ilikuwa na WALIOKAMATA NJIA KUU ZA UCHUMI wanarudi.....kwa nguvu zaidi
 
Wale tuliokua tunawaita nyumbu naona sasa ndo wako na mama. Maneno yao ya kejeli na ushabiki tu. Kinachonisikitisha hakuna chama cha upinzani serious ila kama kitakuja kuwepo ntakupigia kura za hasiraaaa
Sisi wote ni watanzania tunataka Tanzania yenye furaha na amani kwa watu wake bila kujali vyama vyetu sio kule alikokuwa anatupeleka yule tapeli wa siasa
 
Sasa moja kwa moja kwenye mada husika,tangu huyu Mama aingie madarakani nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mwenendo wake,ingawa kweli ni mapema sana kuanza kumtolea hukumu,lakini nachelea kusema huyu Mama HATUFAI hata kidogo especially kwa wale tunaotaka kuona Tanzania inapiga hatua za kweli za kimaendeleo na sio siasa,

Kwa sasa nisingependa kuongea mengi ila ninachoweza kusema ni kwamba HAJUI Taifa hili linataka nini ili kujikomboa,anaonekana ni mtu wa KUFURAHISHA watu tu,bila kujali hii inchi inaathirika au inafaidika vp na anachokifanya,nauona mtindo wa utawala wa Kikwete ukijirudia kwa kasi sana nchini,

Ni dhahiri mpaka sasa huyu Mama anafanya mambo kwa kupangiwa au kuchukuliwa na upepo tu wa kwenye mitandao ya kijamii lakini yeye binafsi hana mipamgo na maono yoyote ya kueleweka juu ya Tanzania.
Umetoa tuhuma kubwa sana, bila hata kuitetea.

Unapotoa tuhuma, ujue unachafua jina la mtu, ni bora utoe na utetezi wa hiyo tuhuma, watu wapime maneno yako.

Kama huwezi kutoa utetezi wa tuhuma yako, ni bora ukae kimya tu.

Sijasema Rais anaweza au hawezi, ila kitendo chako cha kutoa tuhuma za kimbeambea tu kinanichefua.
 
Wee ukianza kutongoza Mwanamke kumuoa unaanza kumshawishi kwa kutaja furaha za ndoa au changamoto?

Sasa hivi tuna changamoto kubwa ya kurudisha Uwekezaji na njia bora ni kuwaaminisha mazingira kuwa yameboreshwa sio kuanza kuwapa maangalizo
Wapo watu waliamishwa kwamba tupo kisiwani. Hatupo kisiwani. Nilofarijika sana kisikia kabidi siyo wazir wa mambo ya nje. Ni mpumbavu tu awezaye kuhubir kuhisu Ubeberu leo.
Tupo kwenye utandawazi ubeberu ni neno kongwe lenye uhafidhina ndani take.
Aende mwana kwenda
 
Wawekezaji wakubwa amekiri wameshaanza kumpigia simu yeye DIRECTLY huko ikulu, what the https://jamii.app/JFUserGuide is this. Anajua mtego anaonasa hapa au kafanya makusudi kwa kigezo cha anakaribiaha wawekezaji?
 
[emoji28][emoji28][emoji28]mama kawashika pabaya[emoji116]
IMG_20210329_112523.jpg
 
Wawekezaji wakubwa amekiri wameshaanza kumpigia simu yeye DIRECTLY huko ikulu, what the **** is this. Anajua mtego anaonasa hapa au kafanya makusudi kwa kigezo cha anakaribiaha wawekezaji?
Hakuna mtego wowote sababu yeye sio muamuzi wa mwisho,mambo yatajadiliwa kama hayatufai tunaachana nayo,na ndio sababu watu walikuwa wanahimiza kupatikane taasisi strong sio mtu strong maana watu tunapita lakini taasisi zinabaki,hiki sasa ni kidagaa kimewa....
 
Back
Top Bottom