Aprili 1, 2024: Gridi ya Taifa yapata Hitilafu, TANESCO waomba radhi
Wanatuomba radhi au wanatakiwa kuomba kazi sehem sehemu nyingine watuache na TANESCO yetu.
 
Wameona mgao pekee haitoshi wakaamua kuzika kabisa nchi nzima dah....
 
TANESCO hizo hitilafu kwenye Grid ya TAIFA zinatakiwa zitafutiwe muarobaini....kwani naona kama zinajirudia rudia walau ndani ya miezi miwili. Tusizoee kuishi na matatizo...
Hata hivyo sijui kama kuna Shirika la Serikali lenye kuleta faida limefanikiwa kujiendesha kwa faida ya kueleweka?
ATC, TTCL, BRT, General tyres, nk nk nk... naona kama yote yana boronga tu....
Hivi General Tyres Bado Ipo?
 
Hiyo itilafu ilisubiri kwanza Pasaka iishe kisha ndio itokee.

Nadhani hiyo ni itilafu nzuri
 
Watakapourudisha wa tupunguzie na bei ya unit
Maana unit tunanunua bei kubwa halafu bado tunakula hasara kwenye bidhaa zetu
 
Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan,Doktor Honoris causa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania., kwa kuniwezesha kuiona nukuu ya Mshana Jnr kuhusu katizo la umeme wa TANESCO tangu saa 8:22 usiku. Hakika anaupiga mwingi na Kazi iendelee.... 😳
 
hakuna mgao,
ni hitilafu ya kawaida katika grid ya Taifa, na tatizo linahughulikiwa kwa nguvu zote na muda usio kua mrefu hali itarejea itarejea na kua kama kawaida 🐒

kua mustahimilivu kua na subra 🐒
Kama si mgao basi nakuomba tembelea Mbagala Rangitatu siku yoyote uipendayo wakati wa asubuhi, kisha uje uniambie kama ni hitilafu kwani juzi, jana asubuhi umeme haukuwepo, na kesho hautakuwepo.
 
Kama si mgao basi nakuomba tembelea Mbagala Rangitatu siku yoyote uipendayo wakati wa asubuhi, kisha uje uniambie kama ni hitilafu kwani juzi, jana asubuhi umeme haukuwepo, na kesho hautakuwepo.
unayo ratiba ya mgao apo tujiridhishe 🐒
 

Attachments

  • IMG-20240401-WA0006.jpg
    IMG-20240401-WA0006.jpg
    79 KB · Views: 1
Back
Top Bottom