Arusha: Mzee Iddi Maganga abomoa nyumba zake mbili(200M) baada ya wanawe kuacha kufanya kazi na kusubiri urithi

1. Waheshimu baba na mama yako upate miaka mingi na heri duniani
2. Ishini na wazee wenu vizuri (waheshimu, watunze,...)
3. Ujana maji ya motoo
 

Mkuu, huyo mzee kwani ni mgonjwa?
 
Cha ajabu watu mnamsifia.

Hasira hasara.

Angeombea hata mkopo.

Baba mpumbavu watoto wapumbavu.
Hana upumbavu wowote, kimsingi zile nyumba hazina thamani ya milioni mia mbili chenye thamani pale ni kiwanja tu, hata kama mtu angenunua angevunja ajenge upya. Nyumba ya milioni mia mbili inavunjwa kwa sururu? Na nyundo?
 
Huyu mzee ana roho mbaya sana kisha hana hekima...kuliko kuharibu mali angeandika waraka akifa ziwasaidie wenye mahitaji maalum kama yatima nk

Labda wangefanya hivyo wangepata hasira Na husuda wangemuwahisha kabla ya wakati.

Afadhali sasa nyumba hazipo nafsi zitawatulia walau.
 
Kuna mjinga mwingine aliwahi kuja hapa Jamii forums naye anadai ana miaka sijui 37 anaomba ushauri kumshitaki babake eti ameuza nyumba na amekataa kugawia fungu lake. Ndo kama huyo mjinga wa Arusha kisa kuna vijifremu anapokea kodi kwa kushirikiana na mdogo wake wa kike kaona njia rahisi nikumfungia mzee ndani bila chakula ili afe warithi mali. Hii laana haitomwacha unamfungia babako ndani mpaka anakula mavi yake, majirani wameona huruma na kumpigia simu binti wa mzee mganga ambaye ni dada wa huyu mpumbavu, binti akaja na mme wake wamevunja mlango na kukuta mzee tayari amepoteza fahamu.

Ndo kumuahisha hosp ambako ameenda kuzinduka akiwa hajui nani kampeleka pale. Japo mzee amechukuwa uamuzi wa hasira lakini hatupaswi kumlaumu kwa sababu hatujui amepitia mangapi, alafu hizi jamii hawa wazee ********** sijui kwa nini zinaamini sana kwenye urithi badala ya kufanya kazi na kujiandalia maisha.
Ukikuta sana watu wanagombania nyumba za urithi mara nyingi utakuta wanyamwezi, wazaramo,wakwere na wale wa ujiji kigoma huko wale walioishi Kariokoo karioakoo miaka mingi.
Ni mara chache sana kukuta sisi wakurya tukigombania urithi wa nyumba.
 
Mitoto ya late 80s, 90s na early 2000!
Bure kabisa. Hawana tofauti na watoto wa Kino Migo Mwananyamala na Mbezi beach. Yenyewe ni kula kulala. Pombe siku nzima. Kuibia wazazi. Kuzaa hovyo hovyo na madawa ya kulevya.
Hovyo kabisa kabisa 😡🥵🤬
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…