Nimemkubali kweli Mama ni Mama wa shoka sio mchezo, kauli yake aliyo itoa Jana akiwa madhabahuni katika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la KKT alisema hivi
" Hakuna mtu au kikundi Chenye misuli ya kuligawa taifa hili, wala hakuna mwenye misuli ya kuliuza taifa hili.....hakuna....hakuna" alieleza hayo kwa kujiamini na akimaanisha hivyo.
Tunamuombea Rais wetu na wasaidizi wake wote wawe Imara zaidi ya chuma cha pua. Kamwe wasikubali kuyumba wala kuwa wanafiki. wasikubali kugonganishwa wala kuyumbishwa, wasimame imara kama timu moja nasi wananchi tupo pamoja na azama ya Serikali yetu katika uwekezaji katika Bandari yetu ili tunufaike na maendeleo yasonge mbele.
Washikamane, unafiki na uzandiki havitakiwi kwenye utendaji.