Askari wawili wafariki kwa kupigwa na radi Simanjiro

Askari wawili wafariki kwa kupigwa na radi Simanjiro

Kuna mkufunzi wetu wa ATC aliwah kutuambia kwamba radi haiwez kukupiga eti kisa unatumia kifaa cha electronic

Lakin ajabu nimeshaona matukio kama matatu watu wanapasuliwa na radi kisa redio na simu
Upo sahihi Mkuu, hawa wataalam wanasoma theory badala ya kufanya tafiti. Simu ni hatari sana kwenye maeneo ambayo ni lightening prone
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna msaidizi Mwandamizi SACP Ahmed Makarani amethibitisha kufariki kwa Askari wawili wa Kikosi cha usalama barabarani, waliofariki kwa kupigwa na radi wakati wakiendelea na majukumu yao ya udhibiti wa usalama.

Tukio hilo limetokea katika Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro ambapo askari waliofariki dunia ni Joseph Nyamoko na Issa Masoud na Kamanda wa Polisi Manyara ameeleza kuwa mipango ya kusafirisha miili ya askari hao inaendelea kwa uratibu wa Jeshi la Polisi na Familia za wahusika.

Kulingana na wanajamii wa Askari Polisi hao na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimahewa andrew Nyambo, amesema Nyamoko ameacha Mke na watoto wawili sawa na Issa ambaye pia ameacha Mke na watoto wake wawili.
Kifo ni kifo tu
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna msaidizi Mwandamizi SACP Ahmed Makarani amethibitisha kufariki kwa Askari wawili wa Kikosi cha usalama barabarani, waliofariki kwa kupigwa na radi wakati wakiendelea na majukumu yao ya udhibiti wa usalama.
Hiki kitu kiwakute na wale waliohusika kutekwa na kupotea kwa Mdude
 
Comments za watu humu zinakufanya ucheke tu hata kama jambo halichekeshi
 
Back
Top Bottom