Askari wawili wafariki kwa kupigwa na radi Simanjiro

Askari wawili wafariki kwa kupigwa na radi Simanjiro

Manyara na radi wapi na wapi? Tumezoea kusikia huko rukwa, katavi, shinyanga, simiyu na geita
 
Salaam!

Nichukue muda huu kutoa pole kwa askari wetu wawili waliopoteza MAISHA kwa kupigwa radi mkoani Arusha,

Imeripotiwa kuwa, askari mmoja anatokea Zanzibar na mwingine anatokea Mwanza.

Kilichoshangaza kuhusu tukio hili, ni aina ya radi iliyoangamiza ndugu zetu, ni kuwa, radi hii haikuunguza Jani wala mti karibu na eneo hili kama ambavyo tumezoea kusikiza matukio ya radi.

Wataalamu wa mambo haya, wake kutujuza kuhusu aina hii ya radi.

Source: Milard Ayo

Karibuni 🙏
Kama walibeba mwamvuli au bunduki wakawa wameilekeza juu ni shida
 
Eee Mungu nisamehe tu kwa mawzo yanayopita kichwani mwangu.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna msaidizi Mwandamizi SACP Ahmed Makarani amethibitisha kufariki kwa Askari wawili wa Kikosi cha usalama barabarani, waliofariki kwa kupigwa na radi wakati wakiendelea na majukumu yao ya udhibiti wa usalama.

Tukio hilo limetokea katika Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro ambapo askari waliofariki dunia ni Joseph Nyamoko na Issa Masoud na Kamanda wa Polisi Manyara ameeleza kuwa mipango ya kusafirisha miili ya askari hao inaendelea kwa uratibu wa Jeshi la Polisi na Familia za wahusika.

Kulingana na wanajamii wa Askari Polisi hao na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimahewa andrew Nyambo, amesema Nyamoko ameacha Mke na watoto wawili sawa na Issa ambaye pia ameacha Mke na watoto wake wawili.
Watu tumeshindwa la Kufanya sasa radi imeingilia kati
 
Kwa kweli Polisi ni Mashetani. Hawa ndio watesi wetu, hawa ndio wanaotuteka na kudhulumu haki yetu ya kuishi.

Acha tu radi iwape somo kidogo
 
Futa neno "NDUGU ZETU ' usilitumie vibaya hilo neno askari sio ndugu zetu, hao ndugu zao ni virungu,risasi,magari ya kuwasha nk ,watanzania hawana ndugu wa aina ya polisi wanao watesa na kuwaua kwa kiasi kinacho tokea safari hii nasisitiza futa neno NDUGU ZETU.

Chuki katika Jamii imefikia viwango vya juu zaidi kama vile ilivyokuwa kule nchini Rwanda miezi michache kabla ya kuanzishwa kwa Mauaji ya kimbari ya Mwaka 1994.
 
Back
Top Bottom