Askofu Mkuu Jimbo Kuu Katoliki Mwanza awataka wanyonge kukataa wanaomtukana Hayati Magufuli

Mama awe makini na machawa wake watamgombanisha na Kanisa Katoliki. Izi kauli sio za bahati mbaya. Kanisa Katoliki litakuwa na manung'uniko chini chini na katika Siasa za kidola huwezi kuibeza nguvu ya kanisa katoliki
Yuda alikuwa Mtume na mfuasi wa Yesu lakini alipomsaliti Yesu mpaka sasa hivi hata Kanisa huwa linagoma kumbatiza mtu jina la Yuda,kumsema Magufuri kwa yale aliyoyafanya ya kuisaliti Katiba na Amani ya Tanzania hakuwezi kuigombanisha Serikali na Kanisa Katoliki kamwe.Kumbuka msimamo wa Magufuri kwenye Korona na msimamo wa maaskofu kwenye Korona vilikuwaje?Fr Kitima alisemaje?Askofu Bagonza alisemaje mpaka Magufuri akataka kumnyang'anya uraia.Yanasemwa mambo yaliyo ya wazi na si ya kubuni pamoja na kwamba kuna mambo alifanya vizuri lakini kutengenezea watu umaskini ilikuwa ni kosa la jinai ambalo Magufuri alilifanya,miaka mitano ya utawala wake bila ajira kwa wahitimu wa shule na vyuo mbalimbali lilikuwa kosa kubwa ambalo hatasamehewa kamwe,kutokuongeza mishahara kwa Wafanyakazi wa serikali lilikuwa kosa kubwa.Kuna mambo mengi alivurunda kabisa.
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande amesema wanyonge huwa wanatetewa na wachache sana lakini wanyonge huwa wanajisahau hata aliyekutetea wakati mwingine unasahau, anasemwa vibaya umesahau, lazima wakati fulani useme hapana bila shaka hiyo ni demokrasia pia eti kwani demokrasia lazima useme ndio tu bila shaka hata kusema hapana sivyo

Baba Askofu Nkwande kwenye Misa Takatifu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli iliyofanyika katika Madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Kawekamo Mwanza Jumamosi Tarehe 25/03/2023.

"Bahati mbaya kweli demokrasia hii wako wanatukana tukana,lakini hata huyu ambaye tumeona amefanya mazuri makubwa kwa nia njema kwa sadaka kubwa leo hii mfu lakini bado tunasemasema hawa watu wanatufundisha hatimaye kutujue na sisi kusema hapana, wanatoa funzo wanatukumbusha kwamba ikiwezekana ifikie mahali tuseme hapana" Askofu Nkwande

"sasa unataka kutuambia kwamba hiyo SGR kwamba hakuifanya na alifanya kwa ajli ya nini ya familia yake si kwa ajili yetu sisi hizo stendi hizo zinaingiza magari yake mle, hiyo treni linajengwa tayari ni la nani alafu leo mtuambie kwamba sasa ni mabaya ni mabaya ni mabaya" Askofu Nkwande

"Nilianza kwa kusema kwamba wanyonge huwa wanatetewa na wachache sana lakini wanyonge huwa wanajisahau hata aliyekutetea wakati mwingine unasahau, anasemwa vibaya umesahau, lazima wakati fulani useme hapana bila shaka hiyo ni demokrasia pia eti kwani demokrasia lazima useme ndio tu bila shaka hata kusema hapana sivyo" Askofu Nkwande

Nkwande analishwa na kuvalishwa bure na kati ya hao wanamvalisha wamepitia magumu ya utawala wa Magufuli. Kabla ya kutoa matamko hayo angeomba kuundwa kwa tume ya wazi ya kupokea malalamiko ya mambo waliofanyiwa. Kivipi anaweza kumkataza mtu kama Lissu akae kimya.
 
Huna lolote.

Yeye kuvalishwa au kulishwa, hakumfanyi ASISEME UKWELI.

Fala weee
 
Askofu atuambie alipo ben saanane aliyejaribu kuchunguza uhalali wa Phd ya ya yule mwehu na wengine wengi ambao maiti zao zilizokutwa kwenye viroba
Suala hapa ni Kazi nzuri alizofanya JPM.

Mwambie Mama Samia awambie Ben Saa nane yuko wapi.
 
Unyonge ni hali ya kutokuwa na nguvu, mamlaka ama madaraka.

Unapokosa hivyo automatically unakuwa mnyonge, whether you like.

Wanyonge ni wengi sana nchi hii, wanaonewa na Magufuli alikuwa mtetezi wao wa kweli.
Naona mmebeba kaneno 'Mnyonge'

Hoja ya Kiongozi, imewapigaaa , Sasa mmekoswa Cha kuongea.

HAMTAKA MKUBALIKE KWA KUMTUKANA JPM.
 
Kama watanzania ni wanyonge kwanini kanisa linataka sadaka zao? Kwenye jumuia michango kibao mpaka sabuni ya kumfulia padri chupi wanatoa wanyonge mjinga kabisa huyo askofu!
Mmejikita kwenye Unyonge.

Nyundo alizowapiga, mmepagawa
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande amesema wanyonge huwa wanatetewa na wachache sana lakini wanyonge huwa wanajisahau hata aliyekutetea wakati mwingine unasahau, anasemwa vibaya umesahau, lazima wakati fulani useme hapana bila shaka hiyo ni demokrasia pia eti kwani demokrasia lazima useme ndio tu bila shaka hata kusema hapana sivyo

Baba Askofu Nkwande kwenye Misa Takatifu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli iliyofanyika katika Madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Kawekamo Mwanza Jumamosi Tarehe 25/03/2023.

"Bahati mbaya kweli demokrasia hii wako wanatukana tukana,lakini hata huyu ambaye tumeona amefanya mazuri makubwa kwa nia njema kwa sadaka kubwa leo hii mfu lakini bado tunasemasema hawa watu wanatufundisha hatimaye kutujue na sisi kusema hapana, wanatoa funzo wanatukumbusha kwamba ikiwezekana ifikie mahali tuseme hapana" Askofu Nkwande

"sasa unataka kutuambia kwamba hiyo SGR kwamba hakuifanya na alifanya kwa ajli ya nini ya familia yake si kwa ajili yetu sisi hizo stendi hizo zinaingiza magari yake mle, hiyo treni linajengwa tayari ni la nani alafu leo mtuambie kwamba sasa ni mabaya ni mabaya ni mabaya" Askofu Nkwande

"Nilianza kwa kusema kwamba wanyonge huwa wanatetewa na wachache sana lakini wanyonge huwa wanajisahau hata aliyekutetea wakati mwingine unasahau, anasemwa vibaya umesahau, lazima wakati fulani useme hapana bila shaka hiyo ni demokrasia pia eti kwani demokrasia lazima useme ndio tu bila shaka hata kusema hapana sivyo" Askofu Nkwande

Breaking:Wanaomtukana Marehemu JPM ni hawa hapa:1.Mafisadi papa waliokomeshwa na JPM:2:Waliofoji vyeti nya kidato cha nne na kufukuzwa kazi 3:Majambazi na wezi wa kutumia bunduki 3:Machawa 4:Viongozi waliopita ,walio na wivu na kazi nzuri za JPM. 5:Wapinzani waliodhibitiwa na JPM na kukosa ajenda.
 
Mimi ni mwumini wa Kanisa Katoliki, na nimekuwa karibu sana na baadhi ya viongozi wa Kanisa kama maaskofu na mapadre Lakini niwe mkweli wa nafsi yangu, kuwa taasisi hii kubwa, licha ya mwongozo wake ulio thabiti, lakini inaongozwa na wanadamu. Na mwanadamu, siyo wakati wote anakuwa sahihi. Kuna wakati hulka ya mtu haimwachi kwa sababu yupo kwenye nafasi fulani, na kuna wakati ushawishi wa mwili unazidi nguvu ya Roho. Na ndiyo maana utasikia mengi pia yasiyopendeza yanayowagusa viongozi wa Kanisa. Na hiyo siyo kwa Kanisa Katoliki pekee, bali ni kwa taasisi zote za dini.

Lililo jema kwa Kanisa Katoliki, ni taasisi, siyo Kanisa la mtu mmoja. Hivyo kukitokea makosa ya mtu mmoja au kikundi fulani, makosa hayo yanaweza kudumu kwa muda tu, na baadaye husahihishwa.

Wakati wa utawala wa marehemu Magufuli Kanisa liliyumba sana. Na hiyo siyo kauli yangu. Kauli hii ilitamkwa na Askofu mmoja (siwezi kumtaja), mbele ya mapadre wake wawili, na mimi nisiye padre nikiwepo.

Alisema hivi:

"Mnakumbuka tulitoa waraka wa Kwaresma, na tukaigusa Serikali. Tulieleza kuzorota kwa haki na demokrasia, tukstaja matukio kadhaa: kushambuliwa kwa risasi Tundu Lisu, watu kutekwa, maiti kupatikana kwenye viroba, na mengine yasiyopendeza. Baada ya waraka ule watawala hawakupenda, na hasa Rais. Mambo mengi ya hovyo yakaanza. Vitu vya Kanisa na taasisi za Kanisa vinavyotoka nje tukaambiwa tulipie kodi. Kanisa Katoliki la Tanzania miaka yote limefurahia uhusiano mzuri na Serikali zote. Haya sasa yakawa mapya. Kwa hiyo kipindi cha Askofu Ngalelikumtwa kilipoisha, kulikuwa na mjadala mkali juu ya nani awe Rais wa TEC. Ndipo likatolewa pendekezo lililokubaliwa kuwa atafutwe mtu ambaye ana ukaribu au tuseme urafiki binafsi na Rais. Na kazi yake ya kwanza iwe ni kutafuta kurudisha uhusiano mzuri na Serikali. Lilifanyika hivyo. Na baada ya hapo, kodi zote kwa vitu vinavyotoka nje kwaajili ya Kanisa na taasisi zake, ikaondolewa. Sisi wengine, tuliona kuna ukakasi mkubwa lilipotolewa pendekezo lile la kumchagua Rais wa TEC kwa kigezo kuwa awe ni mtu mwenye urafiki binafsi na Rais. Lakini ikawa hivyo, kwa sababu Kanisa halijazoea purukushani dhidi ya Serikali"

Nimeyaweka haya, ili tufahamu kuwa japo hawa maaskofu na mapadre ni mababa wetu wa kuroho lakini kuna wakati matashi yao binafsi yanawaondoa kwenye ukweli.

Sitarajii Askofu au Padre au shekhe, asimame na kusema kuwa lazima usiku na mchana tumseme marehemu yeyote yule kwa sababu alifanya ubaya fulani. Dini zote zinafundisha kusamehe. Lakini pia kumsifia mtu fulani kuwa aliwapigania wanyonge, wakati huo huo kuna waraka wa TEC unaoonya juu ya matendo yasiyofaa dhidi yake, siyo sahihi.
Mkuu katika watu ambao wako humble na fair ni huyu kama unakumbuka wakati wafuasi wa chadema wanakamatwa kanisani st. Joseph Mwanza kwa kisingizio walifanya fujo Askofu lenatus Nkwande alipambania watoke na kulalamika wazi wazi mbele ya vyimbo vya habari.
Between sikatai kanisa catholic ni taasisi inayoongozwa na watu na tusifichane kuna watu wanavyama vyao licha ya kuwa ni vionozi wa kanisa kama father kitima katibu wa TEC yule ni chadema damu damu toka yuko sauti university.
Askofu lenatus Nkwande hajawahi kuonyesha yuko upande wa Magufuli akiwa hai tofauti na Kardinal Pengo logic yake ni kumsema mtu ni mbaya kila siku as if hakuna alicho fanya sio fair between kwa imani ya ki-catholic na ya kikristo in geral mtu akifa sio sawa kumsema vibaya achilia mbali Magufuli amekufa akiwa amepata sacrament ya kitubio na mpako wa mafuta matakatifu.
Logic yake ni kuwa kama kuna watu wanamsema vibaya Magufuli basi sio mbaya wale wanao msema vizuri waonekane wabaya
 
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Mhashamu Baba Askofu Renatus Nkwande amesema wanyonge huwa wanatetewa na wachache sana lakini wanyonge huwa wanajisahau hata aliyekutetea wakati mwingine unasahau, anasemwa vibaya umesahau, lazima wakati fulani useme hapana bila shaka hiyo ni demokrasia pia eti kwani demokrasia lazima useme ndio tu bila shaka hata kusema hapana sivyo

Baba Askofu Nkwande kwenye Misa Takatifu ya kumuombea aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli iliyofanyika katika Madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Kawekamo Mwanza Jumamosi Tarehe 25/03/2023.

"Bahati mbaya kweli demokrasia hii wako wanatukana tukana,lakini hata huyu ambaye tumeona amefanya mazuri makubwa kwa nia njema kwa sadaka kubwa leo hii mfu lakini bado tunasemasema hawa watu wanatufundisha hatimaye kutujue na sisi kusema hapana, wanatoa funzo wanatukumbusha kwamba ikiwezekana ifikie mahali tuseme hapana" Askofu Nkwande

"sasa unataka kutuambia kwamba hiyo SGR kwamba hakuifanya na alifanya kwa ajli ya nini ya familia yake si kwa ajili yetu sisi hizo stendi hizo zinaingiza magari yake mle, hiyo treni linajengwa tayari ni la nani alafu leo mtuambie kwamba sasa ni mabaya ni mabaya ni mabaya" Askofu Nkwande

"Nilianza kwa kusema kwamba wanyonge huwa wanatetewa na wachache sana lakini wanyonge huwa wanajisahau hata aliyekutetea wakati mwingine unasahau, anasemwa vibaya umesahau, lazima wakati fulani useme hapana bila shaka hiyo ni demokrasia pia eti kwani demokrasia lazima useme ndio tu bila shaka hata kusema hapana sivyo" Askofu Nkwande

Angewaasa watanzania wote na sio kuchagua kale kakikundi ka wanyonge pekee!!
 
Back
Top Bottom