Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Ameomba msamaha kwa makosa yepi? Ni muhimu ili waliokua wanamfuata wajue. Kwa maoni yangu Kimaro alikua akienda kinyume na mafunzo ya kilutheri.

Sisi walutheri ibada zetu zinaongozwa na liturgia yetu yenye msingi wa mafunzo ya martin luther. Waluther original hatupendi mifumo na style za kipentekoste 'kilokole' kochosha waomini kwa makelele na concepts za imani za mtu binafsi badala ya zile za kanisa.
Hakuna mlutheri wa ajabu hivi, eti wapentekoste ni "makelele"? jifunze kuwa na religious tolerance and respect for others.
 
Angeandika mwingine nisingeuliza mara mbili, wewe hapa jf ni mwandishi muda mrefu iweje utulishe matango pori?

Ndio ameomba msamaha!! Kwa kosa lipi? Mchungaji alikosea nini mpaka kuomba msamaha?
Yeye ameomba msamaha bila kutaja kosa kwa sababu msamaha mkuu ulishatolewa msalabani

Askofu amemtangazia msamaha ambao ulishatolewa msalabani

Wakristo tunalielewa Hili vizuri kwa sababu hatuamini katika kisasi

Kutajiana makosa hadharani ni Mambo ya Agano la Kale
 
Huyo askofu anamsamehe kama nani au kwa niaba ya nani? Kosa kama ametenda Mungu atamuadhibu kwa wakati wake, wenyewe wamrudishe pale au wameona mapato yameshuka
 
Huyo askofu anamsamehe kama nani au kwa niaba ya nani? Kosa kama ametenda Mungu atamuadhibu kwa wakati wake, wenyewe wamrudishe pale au wameona mapato yameshuka
Akina johnthebaptist walikua wanataka wale hela za kile kigango cha kijitonyama ndo jamaa akawagomea wakaamua kumtoa sasa mapato yameshuka aibu kwao
 
Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt Alex Gehaz Malasusa leo kupitia Ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kinyerezi ametangaza msamaha kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama Dr. Eliona Kimaro ambaye January 16,2023 Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ilimpa likizo ya miezi miwili bila kuweka wazi sababu za likizo hiyo.

Licha ya kupewa likizo ya miezi miwili, Kimaro alitakiwa kuripoti Makao Makuu pindi likizo yake itakapomalizika, jambo ambalo liliibua taharuki kwa Waumini wa Kanisa hilo na hata baadhi ya Waumini wa KKKT Kijitonyama wakaandamana wakiomba Uongozi wa Kanisa hilo umrudishe Kimaro.

Askofu Malasusa leo amenukuliwa akisema “Sote ni Wakristo lakini wengine tumeitwa ili tuwaongoze katika kazi ya Mungu na hawa ni Wachungaji, tuwatunze, tuwasaidie, tuwaombee na tuwapende, Mchungaji Kimaro, Ndugu yangu kama ulivyoomba na Mimi nasema kwa niaba ya Washarika umesamehewa”
 
Kumbe Kimaro aliomba msamaha kama nimekuelewa kwenye aya ya mwisho japo kichwa cha habari yako hukusema so zilekelele za wafia Kimaro hawakujua kuwa nguvu ya mamba kumayi

USSR
 
Unafki hauangalii dini bali tabia nmeuliza kaomba msamaha kwa kosa gani nasi waumini tujue. Maana ya unafki ni kuitikia tu bila kujua sababu.
Ungekuwa muumini ungeijua sababu. Acha longolongo..!!! Wakati anapewa likizo uliuliza sababu? Back to square one, wameombana msamaha wenyewe, wewe usiyehusika na kanisa lao inakuumiza kivipi?
 
Back
Top Bottom