Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Mungu Mwenyewe Ameingilia kati Baada ya Maombi ya Mtumishi Kimaro na Waumini Kumlilia Yesu Mwenyr Kanisa Lake![emoji123][emoji106]
 
Unajua heshima yako JF ni kubwa, ukianza kuandika hovyo hovyo kama majibu haya, you are ruining your well built credibility on JF!
ni mfano tu, anaweza pangiwa pahala popote lakini pia anaweza rudishwa KIJITONYAMA;
So long as ni muajiriwa wa KKKT basi tutegemee lolote, lakini kwa ushauri , wampangie tu kwengine, sometimes inaweza mjengea mtu kiburi, sometimes.
 
Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama ameomba msamaha kwa Kanisa zima la KKKT, Maaskofu, Wachungaji na Waumini wote

Askofu Malasusa amemtangazia msamaha

Askofu awataka Waumini waache Ushabiki kwa sababu wanaligawa Kanisa na huo siyo Ukristo

Tukio lilikuwa mubashara KKKT Kinyerezi

Chanzo: Upendo TV

View attachment 2522599

=====

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt Alex Gehaz Malasusa leo kupitia Ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kinyerezi ametangaza msamaha kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama Dr. Eliona Kimaro ambaye January 16, 2023 Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ilimpa likizo ya miezi miwili bila kuweka wazi sababu za likizo hiyo.

Licha ya kupewa likizo ya miezi miwili, Kimaro alitakiwa kuripoti Makao Makuu pindi likizo yake itakapomalizika, jambo ambalo liliibua taharuki kwa Waumini wa Kanisa hilo na hata baadhi ya Waumini wa KKKT Kijitonyama wakaandamana wakiomba Uongozi wa Kanisa hilo umrudishe Kimaro.

Askofu Malasusa leo amenukuliwa akisema “Sote ni Wakristo lakini wengine tumeitwa ili tuwaongoze katika kazi ya Mungu na hawa ni Wachungaji, tuwatunze, tuwasaidie, tuwaombee na tuwapende, Mchungaji Kimaro, Ndugu yangu kama ulivyoomba na Mimi nasema kwa niaba ya Washarika umesamehewa”

Kuhusu kusimamishwa kwake, soma: Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu
😅😅😅 Kanyooka karudi kuomba msamaha,hakuna mkubwa zaidi ya Taasisi dadeki hahahah.mbona hakuanzisha kabisa lake? Samaki ana Kasi akiwa majini tu,ukimtoa nchi kavu kwisha habari yake.Na akae kwa kutulia sasa,Wala wasimpe cheo Tena hapo kanisani,au wamemwamishia kinyerezi nini?
 
Kinyerezi amealikwa tu kwenye ibada ndio akakutana na msamaha wa MALASUSA.
 
Atapangiwa Kituo kipya
ana kipaji cha kupendwa naturally, na huko atawavuta waumini kumpenda na kummwagia mihela 😀 😀 😀 😀 😀 😀 na kuahatarisha uaskofu wa malasusa kwenye uchaguzi huru na haki ambao haujasimamiwa na CCM/tume ya uchaguzi😀😀😀😀
 
😅😅😅 Kanyooka karudi kuomba msamaha,hakuna mkubwa zaidi ya Taasisi dadeki hahahah.mbona hakuanzisha kabisa lake? Samaki ana Kasi akiwa majini tu,ukimtoa nchi kavu kwisha habari yake.Na akae kwa kutulia sasa,Wala wasimpe cheo Tena hapo kanisani,au wamemwamishia kinyerezi nini?
tumeshaambiwa amesema mwenyewe ni yale mahubiri ya kusema vijana waislam ni waaminifu kutuzidi
 
ana kipaji cha kupendwa naturally, na huko atawavuta waumini kumpenda na kummwagia mihela 😀 😀 😀 😀 😀 😀 na kuahatarisha uaskofu wa malasusa kwenye uchaguzi huru na haki ambao haujasimamiwa na CCM/tume ya uchaguzi😀😀😀😀
Yeye anapenda Kijitonyama kwa sababu mko Wengi mle meku!
 
Yeye anapenda Kijitonyama kwa sababu mko Wengi mle meku!
Hujui lolote:
Alikuwa KKKT KARIAKOO , kipindi kaingia Kariakoo kanisa lilikuwa limeoza na hakuna washirika, hakuna vyombo wala kwaya, KIMARO kaleta yote hayo na kanisa likafurika Matajiri akina Kimario, Saba General, Mzee Mushi, Mzee Kessy yule wa Maduka ya vitenge na badhi ya wakinga, na watu walitoka mbezi na kibaha kuja kusali Kariakoo, WAKAMTOA na kumpekeka Kijitonyama, ndio akaanzisha MAHUBIRI KAMA YA YESU na kuachana na liturujia za mafarisayo na masadukayo ,dhahabu ukiificha hata kwenye tope ina angaza.
 
Hujui lolote:
Alikuwa KKKT KARIAKOO , kipindi kaingia Kariakoo kanisa lilikuwa limeoza na hakuna washirika, hakuna vyombo wala kwaya, KIMARO kaleta yote hayo na kanisa likafurika na watu walitoka mbezi na kbaha kuna kusali KAriakoo, WAKAMTOA na kumpekeka Kijitonyama, ndio akaanzisha MAHUBIRI KAMA YA YESU na kuachana na liturujia za mafarisayo na masadukayo ,dhahabu ukiificha hata kwenye tope ina angaza.
Kijitonyama wakati wa Mchungaji Hiza ndio Katibu mkuu wa CCM mzee Makamba alikuwa anakuja kuabudu na kuchukua ile mistari ya Biblia

Kijitonyama imejitambua kitambo sana kabla hawajahamia akina Macha!
 
Back
Top Bottom