Askofu wa KKKT Dkt. Alex Malasusa atangaza kumsamehe Mchungaji Kimaro

Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama ameomba msamaha kwa Kanisa zima la KKKT, Maaskofu, Wachungaji na Waumini wote

Askofu Malasusa amemtangazia msamaha

Askofu awataka Waumini waache Ushabiki kwa sababu wanaligawa Kanisa na huo siyo Ukristo

Tukio lilikuwa mubashara KKKT Kinyerezi

Chanzo: Upendo TV

View attachment 2522599

=====

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt Alex Gehaz Malasusa leo kupitia Ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kinyerezi ametangaza msamaha kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama Dr. Eliona Kimaro ambaye January 16, 2023 Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ilimpa likizo ya miezi miwili bila kuweka wazi sababu za likizo hiyo.

Licha ya kupewa likizo ya miezi miwili, Kimaro alitakiwa kuripoti Makao Makuu pindi likizo yake itakapomalizika, jambo ambalo liliibua taharuki kwa Waumini wa Kanisa hilo na hata baadhi ya Waumini wa KKKT Kijitonyama wakaandamana wakiomba Uongozi wa Kanisa hilo umrudishe Kimaro.

Askofu Malasusa leo amenukuliwa akisema “Sote ni Wakristo lakini wengine tumeitwa ili tuwaongoze katika kazi ya Mungu na hawa ni Wachungaji, tuwatunze, tuwasaidie, tuwaombee na tuwapende, Mchungaji Kimaro, Ndugu yangu kama ulivyoomba na Mimi nasema kwa niaba ya Washarika umesamehewa”

Kuhusu kusimamishwa kwake, soma: Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu
Kwani kosa lake lilikuwa lipi?
 
Malasusa amekutana na kigingi kizito, kakubali yaishe, alizoea kuoneaonea wachungaji, Sasa ameweka ugoko, Kimaro kaweka Jiwe la Mbinguni, wachungaji wajiandae kumuangusha katika nafasi yake ya uaskofu, wasamehe lakini wasisahau anayewaangamiza
Screenshot_20230219-124906.jpg
 
Wakristo waache unafiki, msamaha kwani alikosa? Alipewa likizo na kuripoti makato makuu Sasa wapi hapo inaonesha alikosea, kama walikoseana sirini iweje Leo msamaha uwekwe hadharani?
Nadhani Bango la Morocco linahusika!
 
Mchungaji Kimaro wa KKKT Kijitonyama ameomba msamaha kwa Kanisa zima la KKKT, Maaskofu, Wachungaji na Waumini wote

Askofu Malasusa amemtangazia msamaha

Askofu awataka Waumini waache Ushabiki kwa sababu wanaligawa Kanisa na huo siyo Ukristo

Tukio lilikuwa mubashara KKKT Kinyerezi

Chanzo: Upendo TV

View attachment 2522599

=====

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dkt Alex Gehaz Malasusa leo kupitia Ibada ya Jumapili katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kinyerezi ametangaza msamaha kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama Dr. Eliona Kimaro ambaye January 16, 2023 Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ilimpa likizo ya miezi miwili bila kuweka wazi sababu za likizo hiyo.

Licha ya kupewa likizo ya miezi miwili, Kimaro alitakiwa kuripoti Makao Makuu pindi likizo yake itakapomalizika, jambo ambalo liliibua taharuki kwa Waumini wa Kanisa hilo na hata baadhi ya Waumini wa KKKT Kijitonyama wakaandamana wakiomba Uongozi wa Kanisa hilo umrudishe Kimaro.

Askofu Malasusa leo amenukuliwa akisema “Sote ni Wakristo lakini wengine tumeitwa ili tuwaongoze katika kazi ya Mungu na hawa ni Wachungaji, tuwatunze, tuwasaidie, tuwaombee na tuwapende, Mchungaji Kimaro, Ndugu yangu kama ulivyoomba na Mimi nasema kwa niaba ya Washarika umesamehewa”

Kuhusu kusimamishwa kwake, soma: Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu
NAOMBA MSAMAHA

Askofu Malasusa amemtangazia msamaha

Askofu awataka Waumini waache Ushabiki kwa sababu wanaligawa Kanisa na huo siyo Ukristo
Yeye Malasusa ni msafi? Mbona anatajwa kwa kashfa kadhaa hajitokezi hadhaeani kuomba msamaha
 
Kwa mwenyehekima kuomba msamaha hata kama huna kosa ni kujishusha, jambo ambalo MUngu hupenda. Kuomba msamaha ni kutafuta roho ya mapatano kwa maana hata kama una haki kujikweza hakuleti upendo wa Mungu maana unyenyekevu ni jawabu la roho. Utii ni bora kuliko dhabihu
Mentality hii ni kujenga Taifa la mafala...unaombaje msamaha kwa kitu usichokijua?....tabia ya kijinga sana hii...
Ni muhimu mtu ajue kosa ili arekebishe alipokosea...huu ujinga wa kuomba omba msamaha unatengeneza roho ya inferiority sana...
 
Hili kanisa limepoteza kabisa mwelekeo, Dayosisi zimekuwa sehemu za malumbano, vitisho, majigambo, fitina, ushirikina, wizi, ubadhirifu nk
 
Malasusa amekutana na kigingi kizito, kakubali yaishe, alizoea kuoneaonea wachungaji, Sasa ameweka ugoko, Kimaro kaweka Jiwe la Mbinguni, wachungaji wajiandae kumuangusha katika nafasi yake ya uaskofu, wasamehe lakini wasisahau anayewaangamizaView attachment 2522759
Kimaro ameomba msamaha sasa hapo nani kakubali mziki

USSR
 
Malasusa amekutana na kigingi kizito, kakubali yaishe, alizoea kuoneaonea wachungaji, Sasa ameweka ugoko, Kimaro kaweka Jiwe la Mbinguni, wachungaji wajiandae kumuangusha katika nafasi yake ya uaskofu, wasamehe lakini wasisahau anayewaangamizaView attachment 2522759
Do! umeandika kishabiki sana labda mimi sijakuelewa
 
Asubiri kupangiwa majukumu mengine
Hawezi kurudishwa pale palipo mpa kibri
 
Back
Top Bottom