Shenzi hii itakutafuna maisha yako yote! Just wait and see!
Kardinali angebalance kidogo kwa kuionya pia serikali kuwachagulia maoni wananchi
Ukardinali siyo daraja katika kanisa katoliki. Daraja ni upadre, ushemasi, uaskofu. Kardinali aweza kuwa mlei, padri au askofu. Nchi kama Brazili kuna kardinali ambao ni mapadre.
sheria za kanisa katoliki kila askofu mkuu wa jimbo ndo mkuu katika jimbo lake. Baba mtakatifu naye ni askofu mkuu wa jimbo la Roma. Pengo anajua kuwa yeye siyo mkuu wa kanisa katoliki Tanzania. Lakini kwakuwa wengi hawajui sheria za kanisa basi anakaa kimya kwakuwa anapenda makuu.
Rais wa Baraza la Maaskofu akisema jambo kwa niaba ya kanisa, basi huo ndo msimamo wa kanisa. Pengo alituvuruga sana siku kanisa liliporushiwa bomu Arusha. Kwa kupenda makuu alitoa kauli anbayo alielekezwa na ccm kwamba lile bomu karusha mkatoliki mwenzetu. CCM wakamkamata kijana maskini wa bodaboda na kumweka ndani.
i kuweka record sawa ilibidi rais wa TEC atoe tamko rasmi la kanisa ambalo lilipingana na tamko la Pengo.
Pengo ana matatizo na huku kutukanwa anajitakia.
Hakuna aliyenidanganya, na ninafahamu kuwa yupo chini ya TEC, lakini ukisoma Canon Laws utapata picha ya kwa nini nimesema ni mkuu.
Kuwa mkuu haimaanishi kuwa na mamlaka juu ya TEC, waweza kuwa mkuu kiheshima lakini si kimaamuzi ndiyo maana Mwadhama Kardinali Pengo hakuwa na mamlaka ya kuzuia waraka huo usisomwe makanisani licha ya kuwa aliona una mapungufu ndani yake.
Na ieleweke wazi, katika kikao kilichotoa waraka huo Pengo hakuwepo, alikuwa India kwenye matibabu, pengine angekuwepo kwa influence aliyonayo, na heshima aliyonayo ndani ya Maaskofu angeweza kutoa hoja zake na wakamuelewa.
Tukiacha hayo, hata kama Pengo kakosea, bado si sahihi kwa mtu anayejiita kiongozi wa dini kumtukana mtu tena akiwa madhabahuni.
Si sahihi hata kidogo na wala biblia haisemi hivyo. Alichokifanya Gwajima ni kinyume kabisa na maadili ya kichungaji. Kama ana hoja za kupingana na Pengo alipaswa azitoe kwa njia iliyo sahihi na si kwa kutukana.
Duu huyu ni mwehu si mchungaji! Naomba Pengo asimjibu amsamehe ni wazi dish limeyumba hakika.
Ngwajima ni mgonjwa hakika
Baada ya kusikiliza kwa makini gwajima nimejiridhisha sasa kuwa asilimia kubwa ya wahubiri wa kilokole madishi yameyumba
Kama kweli hiyo audio ni ya huyo mtu anayeitwa Gwajima, namshauri Mwadhama Kadinali Pengo asijibizane naye. Ni kichaa aliyevuka wendawaximu wa kawaida. Na kwa hakika huyu, hana hata chembe ya ulinganifu na Kadinali Pengo, iwe kwa heshima mbele ya jamii, uchaMungu na hata akili au hekima ya kawaida ya mwanadamu. Na hata kama tuchukulie Kadinali Pengo alifanya kosa kubwa saana, hayo majibu ya gwajima hata mvuta bangi na mpumbavu was kawaida tu asingezungumza hivo. Nakusii Kadinali Pengo usijibizane nae..
Chinga, usiwe na ghadhabu. JF ni sehemu ya elimu. Ndio maana nimekuomba urejee kwenye ukweli ndipo utakapojua kwamba Kardinali Pengo si Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania. Nakupa homework hiyo ili umtafute na umjue kuanzia leo.
Hivi watu wanaenda na familia zao kusikiliza anachoongea huyu 'mchungaji'? Nisingevumilia hata dakika kumi ningetoka na kwenda nyumbani. Cha ajabu watu wanapiga makofi kabisa?
Is it true that Africans and the whole continent has some sort of a curse?
Hawa manabii feki wamechanganya watu kwa vile stress za maisha zimeongezeka, umasikini na kutaka utajiri, maradhi yasiyotibika na huduma mbovu zinawafanya waweze kutushawishi.
No matter what Cardinal Pengo said, Gwajima had no right to use vulgar language against him in public.
Zitto tulimvumilia sana. Asante makamanda kwa kulifukuza joka, Zitto.We mwenyewe huna nafasi yoyote ndani Cdm, hata ujipendwkeze vp kama sio ukoo wa Mtei wewe ni wakutumiwa na wakikuchoka utaitwa msaliti.
Kwanini unajiamini kiasi hiki kwa kitu ambacho hujui..??Ni bora kuuliza kama huelewi Pengo ndiye kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania na Sio Tz tu Hata Kenya na Uganda hazina makadinali hivyo Pengo ni msimamizi pia. Watu wanashindwa kuelewa hoja ya Msingi alichokisema Pengo ni maoni yake binafsi na sio kosa mtu kutoa maoni yake binafsi