Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Naona mbuni kajificha kwenye shamba la maharage, wacha maneno onyesha vyeti
 
ASANTE mleta mada historia nzuri sana... Mungu am bariki sana ili aendelee kuliweka jiji sawa sawa. ...... amwongoze ampe ujasiri madawa yaishe mtaani
 
Kwa hiyo wanaofaulu DSM wao wanatumia helicopter kwenda shuleni? acha mawazo mgando wewe, kama kiongozi lazima uongolee matokeo ya watoto/wanafunzi, RC wa Mtwara yeye ni Afisa Elimu? acha apambane na hali yake.
Kumbe akiongelea matokeo mitoto yenu iliyopata div zero hizo zero zitabadilika kua div one?
Kama ni ishu ya kila mtu kubeba mzigo wake basi nanyinyi bebeni mizigo yenu mpeleke VETA, vyuo mbuzi viko kibao ikasome hotel management na cookery[emoji23]
 
Mnalala mnaamka makonda tu hapo usikute hadi familia zenu zina migogolo ila mmekazania ya makonda tu.
Wewe inakuuma nini......?kama ni migogoro kwenye familia zao ni ya kwao....!kama ni mda wanapoteza ni wa kwao.....!inaonekana inakuuma sana Bashite akishughulikiwa.....!acha yamkute kama aliweza hata kukufuru Mungu kwa kusema yeye ni Mungu Dar......!
 
Na wewe inakuuma nini nikimtetea makonda! Wee mwenyewe kufuru
 
Wanajmvi nimekuwa nikiangalia na kuona MAWE anayotupiwa RC Makonda kuhusu madai yanayohusu uhalali wa MAJINA na ELIMU yake.

Ninapoandika hivi sisemi Makonda hana mapungufu katika maamuzi na utendaji wake hasa wa juzi juzi, hata hivyo tukiangalia upande mwingine wa SARAFU yaonekana kuna ZAIDI ya CHETI, bali ni kutaka huyu RC afukuzwe kazi, ili WENGINE WAFURAHI.

Kwanza kabisa PROFILE ya Makonda ILIVUJWA maksudi kwa sababu ya watu walio na SABABU zao mbaya ili aonekane mbele ya Mwajiri wake ambaye ni rais kwamba yeye ni MHALIFU mkuu.

Na hivyo KUJARIBU kum influence mwajiri wake indirectly kutumia BLACKMAIL ili AMFUKUZE kazi.

Jambo hili limeendelea kwa muda sasa. Swali langu wanajamvi. Kabla ya kumtupia mawe turudi NYUMA.Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa na issue kama hii, mbona ya Makonda kila mtu ANAMTUPIA MAWE?

Ni vizuri tusiwe na DOUBLE STANDARD katika kutoa haki bali tuwe FAIR/na USAWA. bila WIVU, UBAGUZI , na FITINA. Kama Waziri Mwigulu Nchemba HAKUJIUZURU basi TUMWACHE Makonda afanye kazi. Yeye si mkamilifu mara nyingi AMEJIKWAA je hilo ndo tumpe mob justice wampige mawe. ASIYE na DHAMBI na awe wa Kwanza kutupa JIWE!
Mmmh wewe bwana kunatofauti kubwa kati ya vyeti vya Mwigulu na Makonda.Kwamba Mwigulu alipofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mara ya kwanza hakuchaguliwa (ikumbukwe huko nyuma kupata nafasi ya kwenda sekondari halikuwa jambo jepesi hata kama alama zako zilikuwa zinatosha) alichofanya Mwigulu ni kurudia shule ili afanye mtihani wa darasa la saba kwa mara ya pili na ili kurudia shule ya msingi alilazimika kutafuta jina la mtoro mmoja katika shule fulani ili alitumie kwa kuwa serikali ilifuta utaratibu wa kurudia shule kuanzia mwaka 1979, lakini ikumbukwe kabla ya hapo watu wengi waliohitimu elimu ya msingi walikuwa wanarudia tena bila kuhitaji jina la mtoro wa shule bali ilikuwa unabadili jina tu. Kwa hiyo Mwigulu katika awamu hii akapata bahati akachaguliwa kuendelea na shule hadi alipo komeshea ingawa mpaka sasa huyu bwana bado anaendelea kujisomea. Inavyosemwa kwa Makonda ni kwamba alipofanya mtihani wake wa kidatu cha nne akataga kwa maana hiyo mlango wake kwa ajili ya elimu ya juu ulikuwa umefungwa vinginevyo ilikuwa ni kurudia mtihani wa kidatu cha nne akiwa mtahiniwa wa kujitegemea,badala yake inasemwa ametumia mlango wa mtu mwingine kuendelea na shule jambo ambalo haliruhusiwi kiutaratibu na ndipo shida inaanzia.Alichofanya mwigulu watu wengi walioko madarakani na maofisini walifanya nakumbuka kuna jamaa mmoja alirudia na kufanya mtihani wa darasa la saba mara 3, hii ya tatu akabahatika kuchaguliwa na miaka ya karibuni amehitimu degree akitokea kibaruani.
 
Kumbe akiongelea matokeo mitoto yenu iliyopata div zero hizo zero zitabadilika kua div one?
Kama ni ishu ya kila mtu kubeba mzigo wake basi nanyinyi bebeni mizigo yenu mpeleke VETA, vyuo mbuzi viko kibao ikasome hotel management na cookery[emoji23]
Mkuu Davi ni broo nini?
 
Mkuu nadhani hizi post hua hazifutiki humu, baada ya miaka kadhaa tukijaaliwa uzima utakuja kusoma Uzi huu sikutishi Ila huwa yanatokea kweli.
Ila natanguliza pole kwa lolote lotakalo kusibu.

Hayanikuti. Wewe nani kuacha kuombea mvua kipindi cha ukame ujisumbue kuniombea mimi?
Tatizo una ujinga wa Daudi kila anaekukosoa muuza madawa.
Hahahaa
 
Mnalala mnaamka makonda tu hapo usikute hadi familia zenu zina migogolo ila mmekazania ya makonda tu.
Kama familia zetu zina migogoro haki itumike tu hamna namna.. Hatuwezi kua na double standards kwenye sheria, Watumishi waliogundulika kughushi vyetiwa mechukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria iweje huyu Bashite yeye bado yuko ofisini?
 
vyeti vinahakikiwa....mwambie akanushe usimsemee !
Alishahakikiwa vyeti vyake na mamlaka husika hawezi kujibizana na mitandao yetu yenye maneno ya kweli na mengine yasiyo ya kweli.
 
Hiyo sio sababu wala haina uhusiano mkuu
Kwani tangu Makonda awe RC ni muda gani umepita? Je unaamini Makonda ndiye mwenye dhamana ya kufanya wanafunzi wafaulu?

Mitoto yenu inashindia kwenye kucheza singeli na kunyoa viduku mtalaumu sana[emoji23]

Maslahi ya walimu serikali haitaki kuboresha alafu mnalalama [emoji23]

Usafiri wa mjini shida, maisha magumu hata wazazi wanakosa muda wa kufatilia maendeleo ya watoto wao maana wako bize kutafuta japo ugali na dagaa mchele[emoji23]

Walimu wakiongezewa matatizo na serikali mnashangilia eti ngoja wakome tena bodi ya mkopo isikate 15% iongeze iwe 20%[emoji23] [emoji23]
Sasa mtakoma nyinyi, msidhani mtoto wa Magufuli atasoma Bunju secondary school ni watoto wetu maskini, kwa hyo mnaposhangilia matatizo ya walimu mjue mnashangilia watoto wenu kufeli
Muacheni Makonda ale bata historia yake inaonesha alipata tabu sana

Hivi sheria inasemaje kuhusu mtu anayeghushi au kutumia vyeti visivyokua vyake? Ni sheria tu hapo inatakiwa kufanya kazi hayo mengine mnayajua ninyi.. na wala ukaguzi wa vyeti kwa watumishi wa uma haukuanzishwa na sisi, serikali yenyewe ndio ilianzisha.. sasa iweje sheria na taratibu zibague?
 
Mkuu Davi ni broo nini?
Hata kabila langu na lake ni tofauti wala simjui kwa namna yoyote tofauti na kumuona kwenye TV.

Ninachosema Mimi tangu mwanzo, sitaki kumshutumu mtu this time, nilichangia kumshutumu lowassa wakati anaitwa fisadi mwisho wa siku muvi likaja kubadilika 100%
Hii michezo ya kisiasa ni michezo ya kipuuzi sana sitaki kutumika tena, Mimi ntakua wa mwisho kuamini kwamba Paul Makonda alinunua vyeti baada ya kupatikana ushahidi tosha otherwise haya maneno ya mitandaoni nayaacha kama yalivyo[emoji23] [emoji23]
 
Wanajmvi nimekuwa nikiangalia na kuona MAWE anayotupiwa RC Makonda kuhusu madai yanayohusu uhalali wa MAJINA na ELIMU yake.

Ninapoandika hivi sisemi Makonda hana mapungufu katika maamuzi na utendaji wake hasa wa juzi juzi, hata hivyo tukiangalia upande mwingine wa SARAFU yaonekana kuna ZAIDI ya CHETI, bali ni kutaka huyu RC afukuzwe kazi, ili WENGINE WAFURAHI.

Kwanza kabisa PROFILE ya Makonda ILIVUJWA maksudi kwa sababu ya watu walio na SABABU zao mbaya ili aonekane mbele ya Mwajiri wake ambaye ni rais kwamba yeye ni MHALIFU mkuu.

Na hivyo KUJARIBU kum influence mwajiri wake indirectly kutumia BLACKMAIL ili AMFUKUZE kazi.

Jambo hili limeendelea kwa muda sasa. Swali langu wanajamvi. Kabla ya kumtupia mawe turudi NYUMA.Waziri Mwigulu Nchemba alikuwa na issue kama hii, mbona ya Makonda kila mtu ANAMTUPIA MAWE?

Ni vizuri tusiwe na DOUBLE STANDARD katika kutoa haki bali tuwe FAIR/na USAWA. bila WIVU, UBAGUZI , na FITINA. Kama Waziri Mwigulu Nchemba HAKUJIUZURU basi TUMWACHE Makonda afanye kazi. Yeye si mkamilifu mara nyingi AMEJIKWAA je hilo ndo tumpe mob justice wampige mawe. ASIYE na DHAMBI na awe wa Kwanza kutupa JIWE!
Naona umetumwa.Huwezi kubadilisha huu upepo,tunataka ajitete mwenyewe kwa kuonyesha vyeti vyake halisi.Kama vya nchemba ni fake unajua wewe siyo sisi.ole wako akusome humu.
 
Hata kabila langu na lake ni tofauti wala simjui kwa namna yoyote tofauti na kumuona kwenye TV.

Ninachosema Mimi tangu mwanzo, sitaki kumshutumu mtu this time, nilichangia kumshutumu lowassa wakati anaitwa fisadi mwisho wa siku muvi likaja kubadilika 100%
Hii michezo ya kisiasa ni michezo ya kipuuzi sana sitaki kutumika tena, Mimi ntakua wa mwisho kuamini kwamba Paul Makonda alinunua vyeti baada ya kupatikana ushahidi tosha otherwise haya maneno ya mitandaoni nayaacha kama yalivyo[emoji23] [emoji23]
Hata mimi siwezi kuamini kama kweli amefoji lakini kuna mtu ambaye wanatoka naye kijiji kimoja kasema hivyo! simple tu atowe vyeti watu waone kama alivyofanya Mwigulu Nchemba. Over
 
Back
Top Bottom