Baba anatoa nyumba yake ya Kariakoo wakfu iwe mali ya msikiti, huku watoto wake wamepinga hawana urithi, why Watu weusi hatujui Generational wealth

Ahaaa hakika na hii mentality imewaharibu Sana vijana wa Pwani .
 
Asante sana mkuu. Na msimamizi wa mirathi anapatikanaje? Je, wajukuu wasipofikia muafaka na kukubaliana ni nani awe msimamizi itakuwaje? Na yule mjane ana nafasi yoyote kwenye kutoa maamuzi ya msimamizi wa mirathi awe nani?
Hata yeye mjane akitaka anaweza kwenda kuomba usimamizi. Akiona hao wajukuu wanabishana bishana yeye aende kuomba usimamizi. Kama ni Dar hapa, atafute cheti cha kifo cha Mzee Babu halafu aende Mahakama Jumuishi Temeke, afungue mirathi, anaweza kufanya kesi mwenyewe ila kwa usahihi zaidi anitafute nimsaidie
 
Elimu ni kitu cha lazima kwa mtoto ili akuze ufahamu atakaotumia kwenye kuendeleza urithi atakoachiwa na mzazi wake kama ukiwepo.
Elimu siyo urithi, wazazi msikwepe majukumu yenu kwa vizazi vyenu.
Hizi ideology za Elimu ndo urithi utazikuta kwa maskini tu tena waafrika...
Kama umebahatika kuufuta ujinga na una kauwezo jitahidi familia yako izalishe kitu endelevu.
 
Ndugu yangu katika imani Leo umeongea kama mtaalamu mahiri wa masuala ya uchumi.

hongera ndugu yangu katika imani.
 
Masikitiko
Unajua kuna mambo yapo hidden.

Pale Temeke kuna mzee mmoja alikuwa Anaitwa Mzee Mdowe (RIP)

Alikuwa amepata watoto wakubwa age 30+ ,40+

Hao watoto wake wakubwa walikuwa wamemtupa baba yao nikisema kumtupa walikuwa hawana habari nae .

Ila mzee alikuwa pia na watoto wadogo age 12+ 9+

Sasa hawa watoto wadogo wa uzeeni ndo walisimama na Baba yao mpaka anafariki mwaka 2021.

Mzee alichofanya ile Nyumba potential na ndo hiyo alikuwa nayo pekee aliwapa wale watoto na akasema MTU asisogelee na aliweka hizo document kisheria kabisa sasa wale watoto ndugu zao wakubwa na wajinga walimtupa baba yao wapo wanapambana kutaka kuipata hiyo Nyumba .


So na huyo mzee kuna uwezekano Ana watoto Ila ndo wale watoto wajinga wasiojitambua
 
Tafuta mali yako mkuu acha kulialia

Yeye anamaamuzi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…