Bandari na Usalama wa Taifa, Rais Samia hujui hata hili?

Bandari na Usalama wa Taifa, Rais Samia hujui hata hili?

JWTZ ibinafsishwe kwa Wagner PMC.

HAKUNA tunachoweza
 
Uzi huu hauhusiani na uzi mwingine, ni alert mahsusi kwa Rais Samia.

Mh Rais inamaana wewe na wabunge hamfahamu kuwa vifaa vingi vya ulinzi na usalama huingia nchini kupitia bandari?

Vipi endapo kampuni itakayopewa kuendesha bandari ikiajiri bila kujua majasusi wa nchi jirani kuwa watumishi wake, huoni utakuwa unatoa siri za uwezo wa jeshi lako bila kujua?

Huoni utawaanikia magaidi taarifa zako muhimu? Unakodisha vipi kitovu cha uchumi wako?

Kuna mikataba mingine hayati JPM alisema inaweza kusainiwa na vichaa tu.

Nimekwambia kwa nia njema kabla hayajakufika.
Liufupi tuna raisi dhaifu sana. Nina mashaka hao wasaidizi wake wanamuingiza chaka ili 2025 asiwepo. Kiongozi dhaifu huleta shida kwenye taifa
 
Umefikiria kienyeji sana,hivi umewahi ona pesa zinaposafirishwa si ndio? Huwa zinapekuliwa? Huwa unajua kiasi? Ila unajua ni msafara wa pesa bila shaka..

Hata huko Bandarini vifaa vya kijeshi vinaweza ingia na hakuna wa kukagua,kukodisha Bandari sio kukodisha exclusive rights za Nchi na mara kadhaa tumeshuhudia misafara ya majeshi wakisafirisha zana zao usiku au mchana ila huwezi jua aina ya zana unless wewe ni mtaalamu wa mambo ya jeshi..

Hata huko Nchi zilizoendelea tunaona silaha zinasafirishwa na maadui wanajua ila huwezi jua quantity hata zana zote kiujumla.

Mwisho kwamba Nchi ambazo hazina Bandari basi wewe unajua aina ya silaha zoote walizonazo si ndio? Tuacheni ujuaji usio na msingi na kuwafanya viongozi wajinga..
Hapa uliposema UNLESS uwe mtaalamu wa masuala ya Kijeshi tayari umekubali kuwa haishindikani kupandikizwa Majasusi wa aina hiyo.

Usimrushie mtu madongo kuwa anajifanya mjuaji ilihali alichofanya ni kufikiria nje ya boksi na kuweka tafakuri yake.

Tujifunze kuheshimu mawazo ya wengine.
 
Hapa uliposema UNLESS uwe mtaalamu wa masuala ya Kijeshi tayari umekubali kuwa haishindikani kupandikizwa Majasusi wa aina hiyo.

Usimrushie mtu madongo kuwa anajifanya mjuaji ilihali alichofanya ni kufikiria nje ya boksi na kuweka tafakuri yake.

Tujifunze kuheshimu mawazo ya wengine.
Acha blaa blaa wewe hata Sasa majasusi wapo Wala haihitaji kuwepo bandarini
 
Hivi hatujifunzi kutokana na makosa, serikali ilibinafusisha viwanda na vyote vilikufa, iweje leo iwe bandari inayofanya kazi.
 
Spika wa Bunge, Tulia Akson amesema ni taarifa za Uongo na kesho Bunge litatoa hatma ya mkataba huo. Swali linakuja kama Rais kaunga hoja huko na Bunge linaweza ikosoa hoja ya Rais?
Majibu yapo kesho Bungeni tarehe 10 June.
 
Lakini kwenye Mkataba Waziri Mbarawa inaonekana ameghushi sahihi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kuna wino wa Kijani wa kalamu ya Waziri alafu hapo hapo kuna wino wa bluu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba humu tunalisha FAKE News!!.
Hapa kuna mambo kadhaa.
1. Kuna watu wanatupatia FAKE news kwa masilahi yao ya kisiasa na uanaharakati na huenda upande mmoja unawatumia.
2. Kuna alert ya wizina janja janja ya watumishi wa umma na mikataba isiyo wazi yenye kuligharimu taifa.
2. Scramble of Africa imekuja tunagombaniwa kama mpira huku walioko juu kwenye maamuzi ni walafi wa maisha ya chini ya miaka 30 wakiwa na madaraka na kuiibia kizazi kijacho
3. Vyombo vya Usalama havina weledi, Wasomi wabobezi, Wenye uthubutu wa kusimamia UKWELI au ni Wezi na wanatumika na Wanasiasa au Viongozi aidha kwa kuandaliwa au kujikomba. Na hili ndio TATIZO.
4. Demokrasia na uhuru wa mawazo kwa siasa za Kiafrika HAITUTOI maana sasa tunapewa asali na shubiri kwa mkupuo tunashindwa kuchuja taarifa maana kila kitu kwetu ni Classified Innformation hata mikataba ya nchi ya kuuza mali za umma.

NB. Matokeo yake ndio haya.
1. Taharuki na chuki kati ya raia na serkali au viongozi wao bila hata kuwa na sababu za msingi au kuwaonea.
2. Kila mtu anatumia fursa anapopata nafasi ni kupiga kwa kwenda mbele. Opportunity never come twice.
3. Nchi kuwa shamba la bibi.
4. Mgogawanyiko na kuleta utengano wa kikabila, kanda, hadhi au madaraja ya kiuchumi.( Hii ni mbaya mnooo).
5. Kukosekana kwa Uzalendo na kuenea usaliti na kutumika na nchi zenye nia ya kujinufaisha.

Afrika kwa mara nyingine tukiwa na wasomi waliosomo mitaala ya wazungu tunaingia kile kilitokea karne ya 18 na 19. TUMEISHAAA
 
Hapo vipi?

Binafsi haya maswala yanaendelea ndani ya nchi yetu ni inatoa tafsiri rahisi kwa ulimwengu dhidi ya uwezo wa majeshi ya yetu kulinda nchi na usalama wa nchi kwa ujumla.

Simaanishi majeshi yetu sio imara, ila najiuliza maswali kwanini wanafumbia macho maswala mbalimbali? Nchi nyingine kuuziwa eneo na kutawala eneo fulani fulani na kuwa na mamlaka kwenye eneo hilo ndani ya nchi yetu ni hatari kwa usama wao na nchi kwa ujumla.

Hakuna Mtanzania asiyefahamu issue ya Loliondo, taifa nyingine kuwa na utawala na mamlaka yakufanya chochote katika eneo hilo. Hili jambo halikubaliki hata kidogo katika taifa linalojielewa.

Hii tabia emeendele kumea na kukua kwa kasi, sasa tunasikia bandari inabinafsishwa kwa taifa lingine na kwa aina ya mkataba wa ubinfsishaji ni sawa na kuuza bandari kwa taifa lingine na kuipa mamlaka ya kufanya chochote ndani ya bandari zetu.

Bandari katika nchi ni sawa na mlango wa kuingilia ndani kwako, usalama wa nchi upo wap? Huu si ukoloni unaorudi kwa njia ya kuzidiwa akili na wale wale waliotutawala kwa nyakati zile.

Yaani hapa naandika huku machozi yakinitoka!
 
Nipo hapa kusoma comments na kupataa maarifa zaidi.
 
Hapo vip!!
Binafsi haya maswala yanaendelea ndani ya nchi yetu ni inatoa tafsiri rahisi kwa ulimwengu dhidi ya uwezo wa majeshi ya yetu kulinda nchi na usalama wa nchi kwa ujumla.

Simaanishi majeshi yetu sio imara ila najiuliza maswali kwanini wanafumbia macho maswala mbalimbali,nchi nyingine kuuziwa eneo na kutawala eneo fulani fulani na kuwa na mamla kwenye eneo hilo ndani ya nchi yetu ni hatari kwa usama wao na nchi kwa ujumla.

Hakuna mtanzania asiyefahamu issue ya loliondo taifa nyingine kuwa na utawala na mamlaka yakufanya chochote katika eneo hilo.Hili jambo halikubaliki hata kidogo katika taifa linalojielewa.

Hii tabia emeendele kumea na kukua kwa kasi,sasa tunasikia bandari inabinafsishwa kwa taifa lingine na kwa aina ya mkataba wa ubinfsishaji ni sawa na kuuza bandari kwa taifa lingine na kuipaa mamlaka ya kufanya chochote ndani ya bandari zetu..Bandari katika nchi ni sawa na mlango wa kuingilia ndani kwako,usalama wa nchi upo wap..huu si ukoloni unaorudi kwa njia ya kuzidiwa akili na wale wale waliotutawala kwa nyakati zile..yaani hapa naandika huku machozi yakinitoka.
Unajua maana ya nchi kuuzwa?
 
Atajulia wapi jumapili kama hii yupo zake nyumbani anasuka zakr mkeka uku taarabu kwa mbaaali suburi jua lizame akale urojo.
 
Back
Top Bottom