Mwambie mwenyekiti wako nae ajiuzulu kwa kushindwa kuzuia siri ya mwanae kunusurika kunyongwa china
Honestly ninaomba msamaha kwa yeyote atakayeumia na hilli . ILa mimi ninaomba Zito pia aangaliwe kwa ukaribu. Inawezekana jamaa anatengeneza scenarios za kujipa umaarufu lakini pia akawa anatumikia ccm kwa kujua ama kutojua.
Kama unabisha kwa hilo, toa maelezo mbadala. Ukweli ni kuwa hata jaji Mkuu anamuota usiku na mchana, kama huamini ingia kwenye majalada ukasome.kwamba ccm yoote plus usalama wa taifa ni kidole kimoja tu cha Lisu!
Nimefuatilia Kwa makini kimbunga Cha Siasa Zetu Na Kama kawaida napenda kukusanya mlolongo wote wa matukio Na kutengeneza tafsiri Moja..
Tokea mchezo huu Wa kuwadhuru binaadam sisi watanzania wenzao, Na kuunganisha unyama huu Na mambo ya kisiasa uanze, kuna kila dalili ya fukuto hili kuzidi kutiwa chumvi Na kuvuma pasipo Sababu yoyote ya msingi ndani ya CDM.
Barua iliyomwagwa mtandaoni isiyosainiwa Kwamba Mhe Zitto alimwandikia Katibu Mkuu wa CDM juu ya clarification kadhaa zinazopaswa kuchukuliwa juu ya suala la ...Rwakatale Na Chadema Kwa Ujumla, wimbi la Baadhi ya wanachama wa CDM kuhongwa Na MIMTU ILIYOLAANIWA NA KULAANIKA, Kwamba watoe ushahidi wa dhulma juu ya Kesi ya Rwakatale, Clarification Za. mhe Zitto Juu ya Barua ile hapa mtandaoni na kuonyesha hofu yake Kwamba Ndani kabisa ya CDM kuna "nyokas" au VIRUSI wanaovujisha taarifa ni mwendelezo wa fukuto ambalo Lazima tushauri kama raia WA Nchi yetu tunaopenda mageuzi ya HAKI..
HAKUNA haja ya kumsaka "KIRUSI AU VIRUSI AKA NYOKAS" Ndani au NJE ya CDM, kuwekeza nguvu kuwasaka nyoka Wala hamtawamaliza, wapo, walikuwepo Na watakuwepo, vichaa huwezi kuwaondoa mjini ukawamaliza wote. Shambani tunajifunza mengi, unapolima Na kupanda mbegu zako Na magugu yanatend kuota sambamba Na mmea kusudio, ukipambana Na magugu Kwenye hali ya uchanga unahatarisha maZao mema, wacha mmea ukue, time will tell, gugu utaliadentify easily Na kuliondoa..
Chama chote kujikita kuongelea Rwakatale all days ni matumizi makubwa ya nguvu Za watu makini zisizo Na Sababu, JUKUMU Hilo analo Mhe jembe la Ukweli Tundu Lissu, aachiwe Yeye, Uwezo wa Tundu unatosha kabisa kuwakabili TISS, Polisi, Mahakama, Na CCM yote wakijumlisha Uwezo wao wanafit kidole tu Cha hili Jembe..
Ni Muda Muafaka sasa wa VIONGOZI kuiamsha serikali si mnajua serikali ya sasa inasubiri CHADEMA aseme jambo ndio watende?, sasa endeleeni kutema vitu, ni Muda Muafaka sasa wa kulichukua JIMBO LA IGUNGA, si mnajua serikali imeagiza zaidi ya kampuni moja wafanye Kazi usiku Na mchana kuhakikisha daraja la Mbutu linakamilika ndipo watangaze tarehe ya uchaguzi huo?.. Daraja wanakamilisha Na jimbo linaenda CDM.. Hivi nani ulimwengu we Leo ataichagua CCM honestly tell me..
Kuna kampeni zimeshaanza huku mitaani Za uongozi Wa serikali Za mitaa, 2014 imekaribia sana,, kuna move inayoendelea ya kusimika uongozi Wa kikanda, kuna M 4 C nk.
Yule ambaye Kwenye movement Na shamrashamra hizi Za kichama, hatajitokeza kuwa mstari wa Mbele mjue direct ndio KIRUSI mwenyewe Na ahukumiwe Kwa matendo yake ..
Adios..
Zitto anasema hivi: Nimeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni. Umeona hapo kwenye nyekundu? Soma vizuri post ya Zitto. Ni dhahiri kwamba barua iliyowekwa mtandaoni si barua halisi aliyoiandika Zitto bali ni mfano wa barua yake. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba hii barua ilisomwa kwenye kikao cha kamati kuu. Mtu mwingine aliyekuwa ndani ya kikao, akaandika barua ya mfano wa ile ya Zitto na kuiweka mtandaoni. Kama tungeona barua kama ile mikataba ya CCM ambapo unapata barua ambayo imetolewa kwenye faili na kuwa scanned, basi tungekuwa na sababu ya dhati ya kumtaka Slaa ajiuzuru. Lakini kwa kuwa ni mtu kaigiza, na ameshindwa hata kufoji sahihi wala mhuri wa mbunge, basi ni dhahiri siri ya ofisi haijavujishwa na Slaa.Lukolo unaniangusha ndugu yangu!!!
Kwanini unaishia hapo? Bila kumwajibisha msamamizi mkuu wa ofisi iliyovujisha siri ya barua ya Zitto itakuwa ni kufuga virusi kwenye chama. Tafadhali liangalie hili...
Hata kuingia mikataba 17 kwa siku moja kulipa fadhila ni uzushi sindioeHiyo " siri" ulipoipata mmelisaidia vipi Taifa kutatua matatizo yake, Kama Chadema kueneza uzushi huo basi iaminike hakuna wa kuing'oa CCM, ccm ina matatizo mengi sana kiasi cha kuwaeleza wananchi wakaelewa hakuna haja ya kuzusha uzushi ambao maadui zenu watautumia kuuthibitishia UMMA kuwa nyie ni wazushi sana, Ridh wan abebe unga yeye Mwenyewe je wale vijana wake wa Yanga Family na UV CCM wabebe nini? tena eti abebe kichwa kichwa
mimi naamini barua imevujia mikononi mwa Zitto, sidhani kama hicho kirusi kingekua jirani na Dr.Slaa kingejihangaisha kufuta saini ya Zitto.!!
‘kwamba kuna kirusi ndani ya chama kilicho karibu sana na viongozi wa chama chenye kazi moja tu, yani kuonyesha kuwa CHADEMA hapako shwari, kuna migogoro na hatimaye kusambaratisha chama'. Kirusi hiki lazima kina nafasi andamizi au kipo karibu sana na viongozi waandamizi. Inawezekana kabisa kirusi hiki kinahusika na suala zima la Lwakatare katika kupanga, kuendesha na kutekeleza mpango mzima. Maswali kama ‘kwanini Dennis Msacky na Zitto ndani ya Video ya ‘Lwakatare' lazima sasa yaanze kutafutiwa majawabu.
Asanteni
Mkuu siyo kwamba mimi nahisi kuwa ni wewe na Dr Slaa,ila nadhani wapinzani wenu wa kisiasa watasema hivyo.Kuna mtu alisema ulialikwa kwenye kikao na barua imeleak mara baada ya kikao,na ni barua ambayo Zitto kasema kuwa aliiandika directly kwa Dr Slaa na kwamba ilikuwa ni ya siri.jmushi1,
Sipendi kuandika sana mambo yanayonigusa moja kwa moja kwenye mtandao.Huwa ninakereka sana na kusingiziwa huku kunakotokana na jitihada za watu ambao wako frustrated.
Sijui ni kwanini mtu anihisi katika hili. jmushi1,sijajua ni kwanini umenihisi.Pengine una vigezo
Naelewa una uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja.Na huku JF tumepambana sana pamoja tukiwa na Kichuguu na @Rev.Kishoka.
Wewe si mtu muoga,hebu sema hii conclussion umefikiaje
Kwa wanajamvi:
-Mimi sijahusika kwa lolote
-Mimi ni miongoni mwa watu wanaopinga maswala senstive ya chama kuwekwa public
-Kuna watu ambao hawaoni aibu katika hili.Akina my web , TUNTEMEKE, rais wa tano, Fringe, nice2 MsemajiUkweli , Shonza n.k wanajua huu mchezo wa kuanika vitu ambavyo havipo for public consumption humu.Hawa niliowataja ni ID za kundi fulani mahsusi
-Sijawajahi kupata access ya barua au docoment nyeti za chama changu na hata nikikutana nazo kwa sababu yoyote ile siwezi ku-ziweka public.Nakipenda chama changu,CHADEMA ni mti wenye matunda ambao nimekalia tawi lake.Siwezi kulikata kwa namna yoyote ile,ni bora nife kwa risasi,tindikali n.k kuliko kuvunjika kiungo cha mwili kwa upumbavu wa kukata tawi nililokalia.
Nawaachia wanaocheza michezo hii waicheze.CHADEMA tuendelee kuwa imara
mnajua kwamba nusu ya usalama wenu wa taifa wanareport kwake
mimi naamini barua imevujia mikononi mwa Zitto, sidhani kama hicho kirusi kingekua jirani na Dr.Slaa kingejihangaisha kufuta saini ya Zitto.!!
Hki kirusi hiki
hukijui kabisa au unayo majina una suspect but u cant share?
Inafanana na ya kweli,Kumbe Barua ilikuwa ya kweli, basi tusubiri mengi....
@ZITTO
imeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni.
Naamini na ntaendelea kuamini kuwa aliye post ile video Zitto anamfahamu na naamini pia yeye ndo aliye mpa hii barua aje kuipost hapa.