Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
I can see some truth in it! Nafikiri haya mambo yanahitaji tafakari pana sana. I am almost confused. nafikiri ni vizuri sana kubaki neutral sometimes. Otherwise unaweza ukashabikia usichokijua. Lakini hata hivyo nina maswali machache kwako!
Je wewe ulikuwa kwenye kikao cha CDM jana na ukaona kwamba pendekezo la Zitto kupitia barua hii limekataliwa? Je Zitto alikuwa katika hali gani baada ya kukataliwa kwa hoja yake? Kulikuwa na mikwaruzano au walikubaliana kwa amani? Ninahamu sana ya kufahamu zaidi kuhusu jambo hili. maana linaonekana kuleta mfulugano.
swali zuri sana
 
Haya mwingine ameibuka kumsifia Lissu, hii ndio sababu kubwa ya wabunge kupigania posho.kuwanunua vijana sio gharama ndogo

ULITAKA AMSIFIE majebere! Lissu ni kiongoz wa chama, ana haki zote kupewa sifa kwa kazi zake. Ulitamani angesema Kikwete, Lowasa, Nape, Pinda, Makinda, Mwigulu majembe!! Ona ulivyopauka, dhaifuuu
 
Unajua siasa mbaya sana waulize chadema kilichiwapata ktk uchaguzi WA mabaraza ya katiba Jana igunga kilio kitupu pamoja na kwamba wanaongoza kata ya mjini wagombea wao mtaturu kapata kura moja,kijana kamanda WA chama kashanga kapata sifuri sasa kwa akili yako kunachama hapa usikimbilie matusi lets face facts at the political field
 
Ikifika hapo ndipo namkubali ZZK. Anasema ukweli bila kumung'unya maneno. Ukweli ni kwamba hicho kirusi kiko ndani kabisa ya CHADEMA na kirusi huenda ni kiongozi mmojawapo wa viongozi wakuu wa CHADEMA. Chunguza utabaini. Katika hili sakata ZZK ni mhanga; si alihusishwa na Msacky kwenye ile clip.

CC: Ritz


Vipi kama kirusi ni yeye mwenyewe au mtu wake wa karibu? kwani ZITTO hana motive za kuvujisha hiyo barua? uoni kama kuvuja kwa hiyo barua kunaweza mfanya yeye onekane tofauti na viongozi wa chadema kwa kuzingatia kwamba ile VIDEO ina chembe kwamba ni ya kweli, bila kujali ilichukuliwa vipi? chadema wako wrong kumtetea huyo jamaa kwa kutumia visingizio vya tarehe na mawasiliano ya wahusika, hoja ni kwamba ile video ni ya kweli au sio ya kweli? Kushinda na kushindwa kesi sio hoja, kuna issue ya moral authority,
Maelezo ya Tundu Lisu yanaashiria kwamba ile video ni halisi lakini kulikuwa na ujanja ya kuirecord, sasa mambo kama hayo sio sawa na cover up wanazofanya ccm kila siku?
ZITTO yawezekana ameliona hiyo hivyo anaweza kuwa na motivate ya kuvujisha msimamo wake
 
Please get to the end.... mbona unaishia njiani? Huna haja ya kuficha mkuu Froida. By the way Mtema tayari ni marehemu, na wewe unatumia id fake siyo jina lako halisi. Unamwogopa nani kuweka jina la huyo aliyetajwa na Mtema. Tutajie tafadhari.
Mara mbili mods wamenipiga ban kwa kumtaja
 
Mkuu binfsi naona kuna matatizo makubwa ndani ya CHADEMA, wanatakiwa kujipanda upya, haya matukio sio ishara njema kwa chama hata kidogo.

MWISHO

KWA DR SLAA
CHADEMA wajipande jinsi wanavyoendesha ofisi zao, lakini pia sasa ni wakati wa JOSEPHINE kutoshirikishwa mambo ya chama, naona toka Dr Slaa amejiushisha na huyu mama kumekuwa na majaabu mengi sana hapo kwenye chama, lakini pia nashindwa kuelewa kama JOSEPHINE alimsaliti mume wake wa kwanza tu Dr Slaa sioni kama naweza shindwa fanya hivyo zidi ya BILLS za ccm,
Dr Slaa anatakiwa ku REVIEW security protocol yake nazani ana compromise, regardless hiyo barua ya zitto inasema nini lakini siri za OFISI YA KATIBU MKUU kuwa mitandaoni sio mwanzo mzuri hata kidogo, tusiangalie upande mmoja tu wa nini kimeandikwa lakini pia tuangalie imepatikana je.


kwa zitto
: Majibu yako kuhusu kirusi yaweza kukuhusu pia, utetezi wako ni dhaifu kwenye hiyo area, yawezekana ukasababisha huo UVUJAJI wa barua, nakushawishi team up na viongozi wengine wa chama, nimesoma maelezo yako yamejaa nafsi ya tatu au wao, hakuna uliposema SISI VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHAMA yawezekana tuna kirusi, uwezi sema kirusi kwa mpokeaji tu wakati hata mtumaji anaweza kuwa na KIRUSI. Na kushawishi uchunguze mambo yako pia, yawezekana unatobo sehemu usilolijua au unalolijua,
Huu uvujaji wa barua ya viongozi wa chadema nyie wote mnawajibuka, chadema kama chama makini basi wekeni mfumo bora wa mawasiliano,
Mwisho kuwa makini na tetezi zako zinaongeza kasoro, kwa mimi nimeona huna uhusiano mzuri na Dr Slaa, maana kama ni barua inasemekana ilikwenda kwa zaidi ya kiongozi mmoja, sasa kwa nini unataja ofisi ya KATIBU MKUU peke yake

Analysist wa JF saa nyingine inabidi uwe makini sana kuwasoma hiyo barua sio copy halisi lakini tumeambiwa maudhui yake ni kama hiyo sasa iweje Katibu Mkuu awajibike asiwe aliyeeandika kwamba kivuli cha barua kkakilusha humu tena kwa ku badirisha hata majina yake iwe kwenye mtandao
Josephine ni victim of circumstances, sijawahi kufika chadema lakini sina uhakika kama ana ofisi pale Makao Makuu au yeye ana mkono wa shetani kwamba anafanya kazi pale bila kuonwa
 
Nakwambia Jana igunga huwezi amini wametoka patupu licha ya vurugu chadema wamepata sifuri Kata zote sifuri chezea ccm wewe,nyie tukaneni na pigeni propaganda mkimaliza mnanyolewa na kuendelea kulia kama ndugu yenu Odinga ccm Wako kwa watu nyie mmejaa kwenye mitandao kupiga propaganda,irak haikuokoka kwa propaganda za alsaef aliyekua anaitangazia dunia kuwa tumewachinja wamarekan elfu Huku wanaume wakiteka viwanja vya ndege,ndo chadema mlivyo propaganda nyingi ccm bado Tishio
 
ahsante na MUNGU atasimamia chama .
Nimefarijika sana na msimamo huu natumai na viongoz wengine wanaliona hili.
kua makini na promo za magamba ni mbinu za kuwagawa na kuleta chokochoko
 
Mh. Zitto bana,
Kila mara akija JF huacha maswali mengi badala ya majibu. Hii barua yake ukiisoma utagundua kama CHADEMA kuna matatizo mengi zaidi ya tujuavyo sisi tulioko nje ya pazia.

Kwanza barua inadhibitisha kama HAKUNA unofficial communication kati ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu pamoja na kwamba utendaji wao unategemea sana kuwa na hizi channel mbili za mawasiliano. Sitashangaa kusikia kama, hata kipindi ambacho Katibu Mkuu alisafiri kwenda nje ya nchi, hakukabidhi madaraka yake kwa Naibu Katibu Mkuu wake.

Interesting point, ni hii sentensi ambayo Zitto anaweka alama ya KUSHANGAA kuonyesha kama makubaliano yaliyofikiwa na Kamati Kuu ya Chama kuhusu msimamo wa chama kwa Lwakatare ulimshangaza au hakubaliani nao.

Kuna mengi tutasikia.
Msimamo wa chama umetolewa na Kamati Kuu iliyomaliza vikao vyake jana siku ya ijumaa tarehe 5 Aprili 2013. Huo ndio msimamo wangu pia!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ni kwamba haina signature. Inawezekana mtu ameinakiri na kuifyatua bila signature? Kama ilikuwa ni siri basi huyo anaweza kuwa mtu aliyetumiwa hiyo barua ya siri ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama. kwa hiyo aliyeitoa hiyo barua ni kitrusi ndani ya CHADEMA na madhara ya kirusi yanajulikana wazi!
Ni kweli mkuu,soma hii posti ya Lukolo utaona ametumia procces niliyoizungumzia ya "elimination"
Lukolo said:
Zitto anasema hivi: Nimeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni. Umeona hapo kwenye nyekundu? Soma vizuri post ya Zitto. Ni dhahiri kwamba barua iliyowekwa mtandaoni si barua halisi aliyoiandika Zitto bali ni mfano wa barua yake. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba hii barua ilisomwa kwenye kikao cha kamati kuu. Mtu mwingine aliyekuwa ndani ya kikao, akaandika barua ya mfano wa ile ya Zitto na kuiweka mtandaoni. Kama tungeona barua kama ile mikataba ya CCM ambapo unapata barua ambayo imetolewa kwenye faili na kuwa scanned, basi tungekuwa na sababu ya dhati ya kumtaka Slaa ajiuzuru. Lakini kwa kuwa ni mtu kaigiza, na ameshindwa hata kufoji sahihi wala mhuri wa mbunge, basi ni dhahiri siri ya ofisi haijavujishwa na Slaa.
So possibility ya barua kuwa original ni "eliminated",kuna uwezekano aliyeiweka hapa aliiformulate baada ya kusikia contents zake pengine kwenye kikao.

Again,"pengine"
 
Analysist wa JF saa nyingine inabidi uwe makini sana kuwasoma hiyo barua sio copy halisi lakini tumeambiwa maudhui yake ni kama hiyo sasa iweke Katibu Mkuu awajibe asiwe aliyeeandika kwamba kivuli tena kwa badirisha hata majina yake iwe kwenye mtandao
Josephine ni victim of circumstances, sijawahi kufika chadema lakini sina uhakika kama ana ofisi pale Makao Makuu au yeye ana mkono wa shetani kwamba anafanya kazi pale bila kuonwa

Nimeeleza yaliyo yangu, lisemwalo lipo kuna sababu za kuwa na usikivu, unajua kuna watu hawakubaliki sio kwa sababu wametenda kosa lakini wakati mwingine ni kukosa mvuto kwa watu [ charisma ] kuna kila sababu huyo mama kukaa mbali na chama, ila awe karibu na familia yake.
Tusiwe wapiga makofi tu, yawezekana Dr Slaa hatumtazami kwa umakini, tuwe makini na viongozi wote wa chama
 
Zitto umeweka mambo vizuri. Tuna imani na CDM, tuna imani na wewe. Jana nilipata taabu sana kuamini kwamba ww unaweza kuandika barua yenye mantiki vile halafu usiiwekee sahihi. Haikuniingia akilini, mwishowe nikaamua nisiiamini kabisa. Nashukuru ilikuwa vivo hivyo kwa wanaJF wengi.
 
Mkuu siyo kwamba mimi nahisi kuwa ni wewe na Dr Slaa,ila nadhani wapinzani wenu wa kisiasa watasema hivyo.Kuna mtu alisema ulialikwa kwenye kikao na barua imeleak mara baada ya kikao,na ni barua ambayo Zitto kasema kuwa aliiandika directly kwa Dr Slaa na kwamba ilikuwa ni ya siri.

Sasa hapo mkuu unategemea masalia waseme ni kina nani?

Kuna Samson na Delillah ndani ya CHADEMA I suspect.
 
Mkuu siyo kwamba mimi nahisi kuwa ni wewe na Dr Slaa,ila nadhani wapinzani wenu wa kisiasa watasema hivyo.Kuna mtu alisema ulialikwa kwenye kikao na barua imeleak mara baada ya kikao,na ni barua ambayo Zitto kasema kuwa aliiandika directly kwa Dr Slaa na kwamba ilikuwa ni ya siri.

Sasa hapo mkuu unategemea masalia waseme ni kina nani?
Hivi hakuna mtu mwingine ambaye ame CC kwenye hiyo barua?
Kuna Samson na Delillah ndani ya chadema I suspect.
Though Zitto amemlenga Ben pale alipojaribu kutaja kipindi ambacho barua ime leak.
 
Umerudisha imani yangu kwako tena kisiasa, GO ON ZITTO
 
Teh teh karibu lunch hapa Calabash....njaa mbaya sana..naona unapiga mihayo tu!

Asante sana mwenye shibe.....we kula tu,me nipo na mama yeyooo tunapika hapa nyuma
huku tukiskiza live band ya calabash.
 
Mara zote nimeamini kuwa BILA CHADEMA imara, CCM itakuwa kama simba aliyekabidhiwa bustani yenye swala! Itafuja kila kilicho mbele. Chadema ikiwa imara, Tanzania itakuwa imara.

Safi kaka hiyo ni dhahiri kwa yeyote anayeipenda Tanzania
 
Nimefuatilia Kwa makini kimbunga Cha Siasa Zetu Na Kama kawaida napenda kukusanya mlolongo wote wa matukio Na kutengeneza tafsiri Moja..

Tokea mchezo huu Wa kuwadhuru binaadam sisi watanzania wenzao, Na kuunganisha unyama huu Na mambo ya kisiasa uanze, kuna kila dalili ya fukuto hili kuzidi kutiwa chumvi Na kuvuma pasipo Sababu yoyote ya msingi ndani ya CDM.

Barua iliyomwagwa mtandaoni isiyosainiwa Kwamba Mhe Zitto alimwandikia Katibu Mkuu wa CDM juu ya clarification kadhaa zinazopaswa kuchukuliwa juu ya suala la ...Rwakatale Na Chadema Kwa Ujumla, wimbi la Baadhi ya wanachama wa CDM kuhongwa Na MIMTU ILIYOLAANIWA NA KULAANIKA, Kwamba watoe ushahidi wa dhulma juu ya Kesi ya Rwakatale, Clarification Za. mhe Zitto Juu ya Barua ile hapa mtandaoni na kuonyesha hofu yake Kwamba Ndani kabisa ya CDM kuna "nyokas" au VIRUSI wanaovujisha taarifa ni mwendelezo wa fukuto ambalo Lazima tushauri kama raia WA Nchi yetu tunaopenda mageuzi ya HAKI..

HAKUNA haja ya kumsaka "KIRUSI AU VIRUSI AKA NYOKAS" Ndani au NJE ya CDM, kuwekeza nguvu kuwasaka nyoka Wala hamtawamaliza, wapo, walikuwepo Na watakuwepo, vichaa huwezi kuwaondoa mjini ukawamaliza wote. Shambani tunajifunza mengi, unapolima Na kupanda mbegu zako Na magugu yanatend kuota sambamba Na mmea kusudio, ukipambana Na magugu Kwenye hali ya uchanga unahatarisha maZao mema, wacha mmea ukue, time will tell, gugu utaliadentify easily Na kuliondoa..

Chama chote kujikita kuongelea Rwakatale all days ni matumizi makubwa ya nguvu Za watu makini zisizo Na Sababu, JUKUMU Hilo analo Mhe jembe la Ukweli Tundu Lissu, aachiwe Yeye, Uwezo wa Tundu unatosha kabisa kuwakabili TISS, Polisi, Mahakama, Na CCM yote wakijumlisha Uwezo wao wanafit kidole tu Cha hili Jembe..

Ni Muda Muafaka sasa wa VIONGOZI kuiamsha serikali si mnajua serikali ya sasa inasubiri CHADEMA aseme jambo ndio watende?, sasa endeleeni kutema vitu, ni Muda Muafaka sasa wa kulichukua JIMBO LA IGUNGA, si mnajua serikali imeagiza zaidi ya kampuni moja wafanye Kazi usiku Na mchana kuhakikisha daraja la Mbutu linakamilika ndipo watangaze tarehe ya uchaguzi huo?.. Daraja wanakamilisha Na jimbo linaenda CDM.. Hivi nani ulimwengu we Leo ataichagua CCM honestly tell me..


Kuna kampeni zimeshaanza huku mitaani Za uongozi Wa serikali Za mitaa, 2014 imekaribia sana,, kuna move inayoendelea ya kusimika uongozi Wa kikanda, kuna M 4 C nk.

Yule ambaye Kwenye movement Na shamrashamra hizi Za kichama, hatajitokeza kuwa mstari wa Mbele mjue direct ndio KIRUSI mwenyewe Na ahukumiwe Kwa matendo yake ..
Adios..
Mkuu pengine ungekuwa na IQ ya kukutosha usingeandika hilo nililo highlight .
Matatizo ya watu kama ninyi ni ku infer kitu chochote mradi kina kidhi mapenzi yako.
Kwa taarifa yako mpango wa mradi wa Mbutu ni umetayarishwa siku nyingi kuwaendeleza watanzania kufikia kiwango cha kitaifa na kimataifa.
Siasa zenu za njaa, mradi unatukuza chama chenu zinaashiria upeo mdogo sana wa imformative data na hivyo kupendelea hisia zaidi kukitukuza hicho chama chenu.

Kwa hakika sifa za utelezi wa mgongo wa chupa hazitawafikisha mbali sana.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom