Bei ya chakula ipo juu halafu mtu anasema Mama anaupiga mwingi

Mleta mada hali ingekua mbaya kama masokoni kungekua hamna vyakula na watu wana hela mifukoni ila mambo ni tofauti kabisa ukienda sokoni kila kitu kinapatikana tena mteja unagombaniwa hivyo wewe tafuta hela tu
 
Hakuna mkulima analia kua bei za mahind mchele zimepanda kila mkulima ana chakula na ambao hawana wajifunze kuhifadhi chakula, ukiona bei ya chakula ni ghali nenda shamba kalime
Wewe bado ni mvulana!

Hapa hapo kwa shemeji alipoolewa dadako ndio uje uandike huu uharo!
 
Unafanana na ID yako na avatar yako
 
Kwa nini udhibiti Bei ya vifaa vya ujenzi ? Kwenye soko huria hakuna kitu kama hicho, labda kwenye monopoly au state controlled economy. Isitoshe mnasingizia Bei za vifaa vya ujenzi, kwani mkulima anajenga kila mwaka?
Angalau kwa comment hii umeongea vema;

Sasa swali, ni faida ipi mkulima anaipata kutokana na upandaji wa bei wa vitu anapohitaji kununua khboresha hali zake?
 
Hakuna mkulima analia kua bei za mahind mchele zimepanda kila mkulima ana chakula na ambao hawana wajifunze kuhifadhi chakula, ukiona bei ya chakula ni ghali nenda shamba kalime
Ukilima, huvuni hapohapo 😝😝😝
 
Kaandika mwengine aibu naona mimi
 
Wewe bado ni mvulana!

Hapa hapo kwa shemeji alipoolewa dadako ndio uje uandike huu uharo!
Kwa kua unaishi kwa shemeji unadhani kila mtu anaishi kwa shemeji.

Tafuta hela bei ya vyakula sio kubwa kama mnavyopiga kelele huku mitandaoni na kama unaona bei ni kubwa nenda na wewe kalime uuze kwa bei ndogo
 
Mtu anakwambia mbona bei za vifaa vya ujenzi vinapanda hamlalamiki.

Ujenzi ni basic need?? Wewe ukipata af tano saizi utawaza kununua tofali? Au wenzetu shule ilikua mkiimba mabata madogo madogo mlijihisi mmemaliza. Hali ni mbaya ila mmekaa kulamba mananii tu wanaosema ukweli hamuwataki
 
Yaani Kwa maelezo haya unawaona wakulima wajinga Sana hawana akili, kuweka stoo yeye hawezi? Hao mnaowaita walanguzi huwa wanawashikia bunduki wakulima kwamba niuzie Kwa lazima mazao yako? Hebu fafanua apo na sie tuelewe.
 
Angalau kwa comment hii umeongea vema;

Sasa swali, ni faida ipi mkulima anaipata kutokana na upandaji wa bei wa vitu anapohitaji kununua khboresha hali zake?
Weka swali vizuri, kama naweza kununua gari la bei mbaya ambalo wewe huwezi kununua nitaita faida au niiteje hiyo.
 
Na wewe nenda kawe middleman sasa ufaidi. Middleman anapata na Mkulima naye anapàta. Mimi mwenyewe ninaandika hapa min shamba la mpunga Ubaruku. Nimeuza mchele wote palepale Ubaruku wala sikuleta Dar tofauti na miaka iliyopita.
Nimewahi kulima kule Mbarali estates miaka ya nyuma kabla watu wa share hawajafanya tunyang'anywe mashamba na mwekezaji[emoji52]
 
Kwenye kilimo kila mtu afunge mkanda kwa kweli !! Bei ikipanda ndio furaha ya mkulima !! Wakulima wameonewa sana miaka mingi !! Huwa wanaitwa washamba ! Maana yake ni wa mashambani hajui lolote na hana lolote ! Sasa basi Imetosha Ba ndugu kila mtu ashinde mechi zake !
 
Wewe unadhani kupanda bei ndio tija,
Tija ni kwa mtu kufanya uzalishaji na apate faida kulingana na uzalishaji wake.
Huko ulaya ikipanda Senti kumi au hasini watu wanaondoa viongozi wao madarakani nyie mnajisifia eti ni bei za mda mlefu.
Hata mkipandisha bado mnashindwa kuhimili maisha
Sasa hapo faida iko wapi kwa huyo mkulima?
Ni wakulima wangapi wamepandisha bei na wamenufaika na hizo bei?
 
Hizo bei hazisaidii mkulima maana akishauza nakutoa ghalama za uzalishaji mpaka nauli ya kufika sokoni anarudi bilabila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…