CAG aongea na waandishi wa habari - Aprili 8, 2021

Hizo hasara za utaliii itakua kigwangala ndio alilipa baada ya kukatazwa kukopa kwa mudy boda boda[emoji19]
20210406_181125.jpg
 
Na yule Dr. Abbas alikuwa mratibu wa hii kitu...
Sasa nimeelewa kwanini hakutaka vyombo vya habari vifunguliwe.
Kumbe Dr Abbas anahusika kwenye huu uratibu wa matumizi yasiyo na utaratibu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
CAG Kicheere anaongea na waandishi wa habari muda huu.

Updates;
========

CAG: NILIBAINI WAKALA NNE ZA SERIKALI ZILIKUWA ZINADAIWA BILIONI 783.39

TANROADS ilikuwa na deni kubwa lenye thamani ya bilioni 770.1 kutoka kwa wakandarasi na wahandisi washauri kutokana na kuchelewa kupata fedha za kutekeleza miradi kutoka hazina, wakala wa majengo bilioni 1, RUWASA bilioni 12 na TARURA milioni 125

-Ni madeni ya wakandarasi, watoa huduma na washauri katika hizo taasisi nne

CAG: MIRADI INAYOTEKELEZWA INA TOZO YA RIBA YA BILIONI 14.9

Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali(CAG) amesema miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ina riba ya bilioni 14.9 kama adhabu ya kuchelewesha kulipa hati za madai ya wakandarasi kinyume na masharti ya mikataba

-CAG amesema malipo hayo hayana tija kwani yangeweza kuepukika kwani baadhi ya pesa ni za wafadhili ambazo zipo lakini mlolongo mrefu wa malipo kwa serikali unakwamisha

MALIASILI NA UTALII

CAG: Nilifanya ukaguzi maalum wizara ya maliasili na utalii, nilibaini bilioni 6.8 zililipwa kutoka kwenye mfuko wa tozo ya maendeleo ya utalii bila idhini ya afisa masuuli kinyume na kanuni ya fedha. Pamoja na haya nilibaini matumizi ya jumla ya bilioni 16 yalifanyika bila kuwa na hati za malipo pia yalibainika matumizi ya bilioni 11 ambayo hayakuwa na nyaraka toshelezi na milioni 89 zilizotumiwa na makumbusho ya Taifa kwa matumizi yasiyoendana na shughuli za utalii.

Kwa maoni yangu mkurugenzi wa utalii na mhasibu waliokuwa wanahusika walitumia vibaya fedha za tozo ya utalii jumla ya Tshs Bilioni 34

CAG: BODI YA WAKURUGENZI YA ATCL HAINA MJUMBE MWENYE UZOEFU NA MASUALA YA ANGA

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema hayo na pia kuongeza kuwa Shirika linadaiwa hivyo inakuwa changamoto kuruka kwenye baadhi ya maeneo

Pia Viwanja vya Ndege vimetajwa kuwa na changamoto
Kama anaongea LiVE inakuwaje hakuna video bwaashee?!!!
 
You are a wildebeest carcas to say the least! Hizo ni tit bits za presser ya CAG kama unataka habari kamili weka bando nenda online mwenyewe kama ni kapuku huna bando keep your mandibles shut, the willing wanufaike na hizo nyepesi nyepesi! Narabuk!
😅😅😅😅
Eti "keep your mandibles shut" watu mna vituko!
 
clouds fm ililipwa milioni 600 bila mkataba, tbc milioni 200 bila mkataba wa tamasha la utalii. Kigwangala anatakiwa akamatwe kwa madudu yaliojitokeza kwenye tamasha la utalii festival
Nilikua naamini kipindi cha mzee huu mchezo usingelitokea kumbe wajanja wanafanya yao
 
You are a wildebeest carcas to say the least! Hizo ni tit bits za presser ya CAG kama unataka habari kamili weka bando nenda online mwenyewe kama ni kapuku huna bando keep your mandibles shut, the willing wanufaike na hizo nyepesi nyepesi! Narabuk!
... naona umekuja kwa id nyingine; mjinga!
 
Nilikua naamini kipindi cha mzee huu mchezo usingelitokea kumbe wajanja wanafanya yao
Mwendazake alikuwa mpenzi wa mapambio na yeye Kigwangala akamjulia, ikawa kumsifia ngonjera na mashairi, kumbuka alipeleka mpaka sanamu lililokuwa linafanana na kinyago cha mpapure??😂

Jamaa walijua kula na kipofu, aisee!

Ndiyo maana binafsi nilikuwa kujengwa mifumo imara, siyo mtu kujijengea misifa!

Everyday is Saturday.............................😎
 
Watu wanapiga tu mpunga halafu wanatuambia sisi tujiajiri
Maaniineeer zao wallah!
Kwenye majukwaa vijana mjiajiri msitegemee serikali, hii nchi tajiri!

Kumbe utajiri wanaujua wao na wanauweka majumbani mwao.
Kwa taabu niliyoipata miaka miwili hii, nafikiri report ya CAG isiwe hadharani, leo nimeumia SANA, mijibwa mijizi hii!!
Kutwa kutuminya sisi kodi kodi ili tuwatajirishe wao??

Everyday is Saturday................................😎
 
Kumekucha, salaaalee!! Ngoja waje wale jamaa 🤣
CAG Kicheere anaongea na waandishi wa habari muda huu.

Updates;
========

CAG: NILIBAINI WAKALA NNE ZA SERIKALI ZILIKUWA ZINADAIWA BILIONI 783.39

TANROADS ilikuwa na deni kubwa lenye thamani ya bilioni 770.1 kutoka kwa wakandarasi na wahandisi washauri kutokana na kuchelewa kupata fedha za kutekeleza miradi kutoka hazina, wakala wa majengo bilioni 1, RUWASA bilioni 12 na TARURA milioni 125

-Ni madeni ya wakandarasi, watoa huduma na washauri katika hizo taasisi nne

CAG: MIRADI INAYOTEKELEZWA INA TOZO YA RIBA YA BILIONI 14.9

Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali(CAG) amesema miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ina riba ya bilioni 14.9 kama adhabu ya kuchelewesha kulipa hati za madai ya wakandarasi kinyume na masharti ya mikataba

-CAG amesema malipo hayo hayana tija kwani yangeweza kuepukika kwani baadhi ya pesa ni za wafadhili ambazo zipo lakini mlolongo mrefu wa malipo kwa serikali unakwamisha

MALIASILI NA UTALII

CAG: Nilifanya ukaguzi maalum wizara ya maliasili na utalii, nilibaini bilioni 6.8 zililipwa kutoka kwenye mfuko wa tozo ya maendeleo ya utalii bila idhini ya afisa masuuli kinyume na kanuni ya fedha. Pamoja na haya nilibaini matumizi ya jumla ya bilioni 16 yalifanyika bila kuwa na hati za malipo pia yalibainika matumizi ya bilioni 11 ambayo hayakuwa na nyaraka toshelezi na milioni 89 zilizotumiwa na makumbusho ya Taifa kwa matumizi yasiyoendana na shughuli za utalii.

Kwa maoni yangu mkurugenzi wa utalii na mhasibu waliokuwa wanahusika walitumia vibaya fedha za tozo ya utalii jumla ya Tshs Bilioni 34

CAG: BODI YA WAKURUGENZI YA ATCL HAINA MJUMBE MWENYE UZOEFU NA MASUALA YA ANGA

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amesema hayo na pia kuongeza kuwa Shirika linadaiwa hivyo inakuwa changamoto kuruka kwenye baadhi ya maeneo

Pia Viwanja vya Ndege vimetajwa kuwa na changamoto
 
Ila hii sio fair hii nchi ni yetu sote kwanini wachache ndio wafaidi keki ya nchi tena kwa kufisadi aargh!
 
Back
Top Bottom