Pre GE2025 CCM wamchangia Lissu Milioni 5 atengeneze gari lake. Lissu azipokea
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hizi ni dalili muhimu sana toka CCM kuonyesha hofu yao kwa Tundu Lissu. Fikra zao zote wamezielekeza kwenye njia za kumbana Tundu Lissu sasa hivi;kwa sababu ni tishio kubwa kwao.
Iko wazi mbona? Huwa najichekea tu humu kuona vijana wadogo wadogo wakimpondea TL kwa kejeli kibao, ukweli ni kwamba hakuna kigogo yoyote wa CCM asiyeijua nguvu ya TL. mstaafu Kikwete na late Magufuli wakiongoza kufahamu hilo.

Kama kuna miamba pekee imebaki CDM ambayo CCM wanatamani sana kukamilisha usajili basi wa kwanza ni TL.. Ni mwanaharakati wa wakati wake, Mwanasiasa ambaye akianza kutoa somo la uraia mamia hutulia kumsikiliza bila influence ya kofia, khanga, Tshirt wala wasanii.

Ni wakipekee.
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanyia matengenezo gari yake.

Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa.

Kwa upande wake, Dkt Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.
Alipotafutwa kuzungumzia kitendo hicho kilichofanywa na CCM, Lissu amewashukuru CCM kwa mchango na kwamba atazipokea fedha hizo kama ambayo amekuwa akipokea kutoka kwa makundi tofauti ya watu.

"Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.


Mwananchi
Hiyo ni pole baada ya kupigwa na Polisi wa Ccm
 
Alikataa ile hongo ya Abdul sasa Msigwa kamtumia Nchimbi.

Kuna issue Ccm wana itega kwa Lissu. Soon ita kuwa wazi. Usishangae Lissu akaenda kupokelea huo mchango Lumumba

..wanasema wameingiza kwenye akaunti ya Lissu aliyoelekeza watu wachangiaji.

..ila hili na jambo la kusitisha kwamba wamechangia huku wakifanya kejeli.

..Mch.Msigwa haikumpasa kujidhalilisha kiwango hicho.
 
Watanzania ni wamoja, iwe CCM, CHADEMA, ACT, CUF, NCCR, .....
Hivyo kuchangiana siyo tatizo, changamoto ni wachache wanaowavuruga wananchi kwa nia na matendo yao maovu.
Tunatakiwa kujenga taifa lenye kuaminiana, kuheshimiana na kuthamiana kwa haki.
Utamaduni ulioasisiwa na baba wa taifa na wenzake kuwa sote ni ndugu uendelezwe na uheshimiwe.
 
SIASA = SI HASA

Sijawahi kumuamini Mwanasiasa na sintamwamini Mwanasiasa yeyote
 
Alikataa ile hongo ya Abdul sasa Msigwa kamtumia Nchimbi.

Kuna issue Ccm wana itega kwa Lissu. Soon ita kuwa wazi. Usishangae Lissu akaenda kupokelea huo mchango Lumumba
Na ataenda huyo jamaa.
 
Nampongeza sana katibu mkuu kwa wema wake kwa Lissu aliyetelekezwa na Mbowe.
 
Tofautisha kuchangiwa na watu individuals kimyakimya na kuchangiwa kwenye mkutano wa CCM kwa kuombewa na msaliti wa chama Msigwa na harambee kuitishwa na katibu mkuu wa CCM. hadi hapo huoni tatizo?

..kwasababu mchango huo umefanyika kwa UWAZI, na Lissu hakuwalazimisha wamchangie, sioni tatizo kwa upande huo.

..kitu ambacho sikukipenda ni KEJELI wakati wa uchangiaje huo. Lakini Lissu hana uwezo wa kuzuia viongozi wa CCM kumkejeli.
 
..kwasababu mchango huo umefanyika kwa UWAZI, na Lissu hakuwalazimisha wamchangie, sioni tatizo kwa upande huo.

..kitu ambacho sikukipenda ni KEJELI wakati wa uchangiaje huo. Lakini Lissu hana uwezo wa kuzuia viongozi wa CCM kumkejeli.

Manunuzi yapo ya siri na ya wazi

Hili la Lissu ni manunuzi ya wazi!

Hicho chama cha CCM mbona hakikuitisha harambee ya wazi kuchangia matibabu yake?
Lissu anadai bungeni mahela kibao stahiki za matibabu yake kama mbunge mbona CCM haiiagizi serikali yake kumlipa stahiki zake?

Wakati serikali ya CCM imewashushia viongozi wenzio mkong'oto na vijana kibao wa chama bado wako ndani hazijapita hata siku tatu CCM kupitia uombezi wa msaliti wa chama wanakupa hela ukanunue gari na unazipokea hizo hiyo kama siyo kukosa umakini wa kisiasa ni kitu gani?
 
Wanajaribu kuwahadaa mabeberu ili mali binafsi za viongozi wa ccm zisikamatwe na marekani kwa ushenzi walioufanya kina Sugu juzi. Wanataka ionekane yale ni makosa ya polisi na wao ccm hawahusiki hivyo wasionekane wabaya kumbe ndio mashetani wenyewe.
CCM wanajua kucheza na mindset za watu aisee kongole! kipindi cha uchaguzi wanaona 4R Awadh kazitibua lazima juhudi zifanyike kurejesha imani
 
Back
Top Bottom