Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Kupitia mtandao wa X, GODBLESS LEMA ameandika kuwa wameamua kusitisha safari ya kutembelea wahanga wa mafuriko kateshi wilayani Hanang kutokana na vikwazo vikali wanavyokutana navyo tokea waanze safari ya kuelekea huko

---
Tumekatisha safari ya kuelekea Katesh- Hanang kuona waanga wa mafuriko kutokana na vikwazo vingi tulivyo kutana navyo kuanzia tunaingia Mkoa wa Manyara na zaidi vikwazo vikali tulipotaka kusalimia wagonjwa Hospital ya Rufaa Mkoa wa Manyara.Tunaendelea kuwapa pole sana wakazi wote wa Mkoa wa Manyara.Tutaongea na vyombo vya habari kwa taarifa ya kina zaidi.


Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe pamoja na viongozi wa Kanda ya Kaskazini wamefika kituo cha Polisi mkoa wa Manyara kilichopo Babati mjini. Mwenyekiti na ujumbe wake wamepitia kituoni hapo na kupokelewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamanda George Katabazi wakiwa njiani kuelekea wilaya ya Hanang.
Pia soma > Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 63


 
CCM wamejimilikisha mpaka maafa. Tukisema wao ndo chanzo cha maafa wasikatae. Miongoni mwa waliopatwa na maafa wamo wanachama wa vyama tofauti. Unamzuiaje kiongozi wa Chama kwenda kuona Watanzania wenzake? Hapo wanataka wakiitisha kimkutano waseme ni CCM pekee ilikuja kuwaona.
 
Nlijuwa tu lazima wataletewa figisu

Ova
 


Kama tulivyotarajia tangu awali , Serikali ya Tanzania imekizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo , kuwafariji watu wa Hanang , ambako viongozi wake wamekatazwa hata kutembelea Wagonjwa hospitalini .

Hapa ndipo siasa za kishamba za ccm zilipofikia .

 
Masela wa matukio wanajua mkuu wa nchi alipanga tarehe hiyo nao wakapanga tarehe hiyo makusudi ili watafute sababu na huruma chadema kwa sasa hakuna mikakati!
 
Acheni visingizio, mmekosa michango ya kupeleka!!

Mkaweka picha ya Mfalme Mbowe kama yeye ndo kafa kwenye mafuriko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…