Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Wakuu
CHADEMA wamemjibu Makamu Mwenyekiti wa chama chao, Tundu Lissu
=====
Hivi karibuni kumeibuka tena wimbi la hoja mbalimbali ambazo zilishawahi kuibuka siku za nyuma na ambazo zimesababisha wanachama, wapenzi wa Chadema na Wananchi kwa ujumla kutaka ufafanuzi rasmi wa Chama;
1. Chadema haijawahi kuletewa hoja ya kugawana madaraka kutoka Chama chochote au kutoka kwa Serikali wala hoja ya kupewa Majimbo ya Uchaguzi au kugawana nafasi za madaraka katika muundo wa Serikali.
Aidha, ieleweke kuwa kwa mujibu wa Katiba iliyopo sasa nafasi ya Makamu wa Rais hugombewa na haitolewi mezani, vilevile nafasi ya Waziri Mkuu hutokana na Chama chenye wabunge wengi Bungeni.
2. Chadema katika vikao vyake vyote rasmi haijawahi kujadili, kutoa au kupokea mapendekezo yeyote ya kitu kinachoitwa "Serikali ya nusu mkate". Jambo hili kama linavyopotoshwa halijawahi kuwa Sera ya Chadema.
3. Chadema haijawahi kupokea wala kujadili au kubeba au kuwa na agenda na Serikali katika vikao vyote vya Chama au vile vya maridhiano kuhusu hoja hizo tajwa hapo juu.
4. Ikumbukwe kuwa vikao vyote vya maridhiano vilifanyika mwaka 2022 na vikahitimishwa 3 Januari 2023 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alizungumza na Taifa kupitia Vyama vya Siasa na Wadau mbalimbali kuondoa katazo haramu la shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano. Tarehe 30 na 31 May 2023 palifanyika vikao vya mwisho ambapo tulishindwana. Baada ya hapo hakuna kikao chochote cha siri au hadharani kimefanyika baina ya CCM na Chadema.
5. Kwa kipindi chote cha mwaka 2023 na 2024 hadi sasa, Chama kimekuwa kwenye program mbalimbali zenye lengo la kukiuhisha Chama kufuatia miaka 7 ya Chama kupitishwa kwenye "Bonde la Uvuli wa Mauti" na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mtandao na Uongozi wa Chama katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye Vitongoji, Mitaa na Vijiji. Shughuli zilizofanyika ni pamoja na ziara mbalimbali maeneo kadhaa ya nchi kwa ajili ya mikutano ya hadhara, maandamano, mafunzo, usajili wa wanachama kidigitali, chaguzi kuanzia ngazi za vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata, Majimbo, Wilaya, Mikoa hadi Kanda. Chaguzi hizi za ndani zitahitimishwa na Uchaguzi Mkuu ndani ya Chama.
+ Benson Kigaila: Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi anafanya kazi ya CCM

Pia, Soma:+ Benson Kigaila: Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi anafanya kazi ya CCM